Vijana CHADEMA wamshukia Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana CHADEMA wamshukia Lowassa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Jan 14, 2012.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  BARAZA la Vijana wa Chadema (Bavicha ) limemtaka Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, kutoingilia masuala ya chama hicho huku likitamba kuwa nguvu ya umma ndiyo iliyotumika kupambana na mafisadi na kuchangia ongezeko la kasi ya uwajibikaji serikalini.

  Kauli ya vijana hao imekuja siku chache baada ya kiongozi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, kukaririwa akikemea matumizi ya nguvu ya umma, yanayoendeshwa na baadhi ya vyama vya siasa nchini kushinikiza mambo mbalimbali, na kuonya kuwa tabia hiyo hailifikishi taifa popote badala yake nguvu hiyo ingetumika kuhamasisha maendeleo.


  

  Akijibu kauli ya Lowassa jana, Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, John Heche, alitamba kuwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya ufisadi nchini, yametokana na nguvu hiyo ya umma inayobezwa na Lowassa.

  Alisema nguvu ya umma ndio iliyotumika kuanika orodha ya watuhumiwa wa ufisadi mwaka 2007 katika Viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam na kusababisha baadhi yao wawajibishwe.

  Katika orodha hiyo ya Chahema iliyokuwa na majina 11, Lowassa ni miongoni mwa wanasiasa waliotanjwa na chama hicho kikuu cha upinzani.

  Heche alisema kutokana na vitendo hivyo, wananchi waliweza kuonyesha nguvu zao kwa kuwataka mafisadi kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kujiuzulu nafasi zao, jambo ambalo lilifanyika.

  Lowassa alijiuzulu Uwaziri Mkuu Februari 2008, kutokana na kashfa ya Mkataba wa Richmond baada ya Bunge la Tisa kuunda Kamati Teule, chini ya Mbunge wa Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe, kuchunguza suala hilo na kutoa mapendekezo yake.Heche alisema, Bavicha itaendelea kutumia nguvu ya umma ili kuleta maendeleo kwa wananchi na kumulika mafisadi, ikiwa ni pamoja na kuwaanika hadharani ili wananchi waweze kuwatambua na kuwachukulia hatua stahiki za kisheria.

  Alifafanua kwamba, kufanya hivyo si kutishia amani ya nchi bali amani ya watuhumiwa wa ufisadi ndiyo inakuwa shakani kutokana na matendo yao maovu.

  Heche aliongeza kwamba wananchi wanapandwa hasira juu ya viongozi wenye matendo kama hayo, kwa sababu wanachangia kuliingiza taifa katika dimbwi la umaskini kwa kujali maslahi yao binafsi.

  Kwa mujibu wa Heche,Lowassa anapaswa kuonyesha mfano hai kwa wananchi ili aweze kujenga imani, jambo ambalo linaweza kuwabadilisha taswira.

  Alisema, kama Lowassa anaamini nguvu ya umma inapaswa kutumika katika kazi za maendeleo alizozitaja, basi awe wa kwanza kufanya hivyo yeye na chama chake badala ya kuzunguka katika nyumba za ibada na kuchangia fedha nyingi, ambazo vyanzo vyake havijulikani na Watanzania wangependa kujua hilo.

  ::Mwananchi
   
 2. N

  Nyalutubwi JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 572
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Kwa nini huyu Bwana Lowasa analazimisha watu wamheshimu wakati ni yeye mwenyewe aliikataa heshima hiyo?.
  Ni Tanzania tu ambako watu wa aina ya Lowasa ambao sifa yao ni kuhujumu MASLAHI ya Taifa na raslimali zake na bado wakapita mitaani kwa ujasili na kuyasema haya.
  Lakini Lowasa asidhani dhihaka zake kwa Watanzania zitaendelea kuvumiliwa ajue iko siku atawajibika kwa ufisadi wake na matendo maovu anayo wafanyie wale wote wanaobainisha maovu yake.
   
 3. Mlingwa

  Mlingwa JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 382
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Enzi ama dhama za watawala kutumia majukwaa na mawakala wao kuwarubuni wananchi zimepitwa na wakati
  wananchi wa leo ni tofauti sana na wale wa dhama za 2005.
   
 4. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ukirusha jiwe gizani na mmoja akapiga kelele ujue limempata (CDM
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,435
  Likes Received: 418,957
  Trophy Points: 280
  nguvu ya umma ndiyo demokrasia kwa hiyo Mhe E.L amaanisha ya kuwa udikteata ndiyo sera mpya ya chama cha magamba?
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kelele za Ufisadi zinamgusa huyu Manywele moja kwa moja, ndiyo maana anakosa usingizi!!
  Inabidi akina Regia wakipanga awamu ya pili ya Maandamano ianzie Monduli safari hii, hakyanani tutatoka Arusha mjini kwenda kuhudhuria!
  Lowassa hana hoja anayoweza kuinua mdomo akawasema nayo cdm, hana guts hizo...angekuwa na washauri wangemkataza katakata asiingilie kauli yoyote ya cdm, coz its well well above his capacities, and his reputation power is such low that it deters him from uttering a word !
   
 7. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #7
  Jan 14, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Jamani samahanini kidogo kama kuna mtu yeyote mwenye wasifu wa Heche humu ndani anipatie tafadhali..mana namsikia sikia tu sijajua ni nani hasa na anafanya nini hapa duniani..
   
 8. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,635
  Likes Received: 4,743
  Trophy Points: 280
  Fisadi Lowasa atamaliza sarakasi zote lakini urais hapati ng'o, mahali anapostahili ni jela tu nakufilisiwa mali alizofisadi.
   
 9. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kumbe kuna mafanikio yaliyopatikana katika kupambana na ufisadi eeeh!hii nilikua siijui,kumbe secretariet ya kina nape imefanya kazi nzuri kwa kushirikiana indirectly na chadema na wao kulivalia njuga suala la ufisadi,wazidi kukaza buti kwa kushiriakiana mpaka magamba mawili yavuke,moja lile la igunga tayari
   
 10. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hivi Mbowe na Slaa wakiwasikia BAVICHA kuhusu hili itakuwaje?
   
 11. M

  MALAGASHIMBA Member

  #11
  Jan 14, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Mapambano dhidi ya ufisada bado hayajafanikiwa hata kidogo,kilichoongezeka ni uelewa wa wananchi kuhusu ufisadi ndio umeongezeke
   
 12. L

  LOYAL TZN Member

  #12
  Jan 14, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wasifu wa heche kwanza na je amewashirikisha wakubwa zake akina dr. Na mbowe?
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Jan 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  lowasa amewashika pabaya.hapa kila siku mnamsifia kuwa ni shujaa leo kawaambia ukweli mnaanza nyodo.af heche sio saizi ya lowasa.yeye atatoa tamko,lowasa anakula na kunywa na kina slaa na mbowe meza moja.
   
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  Jan 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  alimaliza kidato cha nne shule ya sekondari tarime mwaka 1998 baada ya hapo akaenda kusoma cheti cha ualimu daraja la 111A chuo cha ualimu nshumba kwa sasa yuko mtaani anaganga njaa.
   
 15. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #15
  Jan 14, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,635
  Likes Received: 4,743
  Trophy Points: 280
  Wananchi wakiwa na ufahamu juu ya ufisadi na wakaelewa kuwa chanzo cha dhiki yao ni ufisadi unaofanywa na viongozi wao ni jambo la maana sana kwani wao ndiyo mahakama ya juu kuliko zoote kuwaadhibu viongozi mafisadi na taasisi zao.
   
 16. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #16
  Jan 14, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Labda nimkumburhe mwisho wa ubaya ni aibu nayo aibu iko njiani kumjia na atatamani ardi ipasuke ili afiche uso wake na itashindikana
   
 17. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #17
  Jan 14, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Unamaanisha limempata lowasa?
   
 18. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #18
  Jan 14, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wamekwisha kuanza kuitumia
   
 19. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #19
  Jan 14, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Akina nape wangekuwa wamefikia sehem nzuri ya kukabiliana na mafisadi wangeweza kuwavua gamba akina Lowasa na Gamba kiunoni siyo tu kuwavua kwa maneno na siyo vitendo
   
 20. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #20
  Jan 14, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hiyo nayo ni moja ya mafanikio na sasa tutaendelea na step nyingine
   
Loading...