Vijana 69 waitosa CHADEMA Mbeya

CCM kwa miaka hamsini imedanganya wananchi kuwa ni kazi ya Diwani au Mbunge kuwajaza wananchi pesa!!

Sasa Mary Mwanjelwa mwizi wa MATAULO atawasaidiaje zaidi ya kuwafundisha wizi!!

Mbeya mtatandikwa milele!!
 
Maneno ya cdm ni matamu sanaaa. Tutawapa ajira, maisha safi, elimu bure mpk chuo kikuu. Kwenye utekelezaji ni ziroooo. Kila heri vijana

Hayashindi utamu wa CCM:


 

Badilisha kichwa cha habari isomeke Omba Omba 69 waitosa CHADEMA. Nyie CCM mbona mnapenda sana siasa za kutumia njaa za wananchi kujiimarisha>??

Ila mkae mkijua 2015 hata mmalize tembo wote mbugani, hamtakuwa na hela ya kutuhonga vijana milioni 35 wa nchi hii, na kwa kuwa tutakuwa tumeelimika kwenye shule za kata, hongo ya kanga na tshirt na kofia hakuna atakayechukua.
 
asante sana TandaleOne aka mwenezi kwa taarifa, endeleeni kujifariji wakati safari ikielekea ukingoni
 
Diwani Lucas Mwampiki ndiye Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini.
Mimi nilikuwepo kwenye kuwakabidhi Kadi za CCM vijana hao.
Diwani Mwampoiki amekuwa mtu wa kutoshiriki shughuli za Kijamii na akiulizwa anatoa majibu ya kshfa na dharau kwa vijana na wapiga kura.
Pia aliwaahidi vijana hawa kuwa atawasaidia kuwatafutia mitaji ili waweze kujiajiri na kufanya ujasiliamali.
Pia jana nlikuwa na Interview pamoja na Mwampiki kwenye Radio Station inaitwa ROCK FM hakika huyu mtu hana sera wala mipango endelevu kwa vijana na jamii yake zaidi ya Propaganda tu.
 

Kama wanataka ndarama wakapange foleni Lumumba ama waende nyumbani kwa msomali muua tembo
 
Unapenda sana Namba 69 wee kijana. Angalia usije ukauguwa kansa ya koo kama Michael Doglas.


Chadema Kata ya Mwakibete, jijini Mbeya imepata pigo baada ya vijana wake 69 kuamua kukitosa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
 
Vijana wamejitambua.

...yaaa wametambua kwamba chadema haihongi mtu kama anavyotaka kufanya mwigulu huko arusha. vijana wa hivi wengi tu watakuja kwenu sisi ni uzalendo kwanza na si pesa kwanza. tunachangia chama hatulipwi au kuchongewa dili kwa jina la chama...
 
Wakizungumza mbele ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya, Dk Mary Mwanjelwa walisema Diwani Mwampiki amekuwa kikwazo kwao katika kujiinua kiuchumi na kuondokana na Utegemezi.

MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia CCM mkoani hapa, Mary Mwanjelwa amepinga kutoa kauli za kuonesha nia ya kukihama chama hicho na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).


Tamko la Mwanjelwa alilolitoa kwa waandishi wa habari jana, limetokana na gazeti moja la nchini kumkariri kuwa ana nia ya kuihama CCM kutokana na Rais Jakaya Kikwete kuteua
wabunge ndani ya muda mfupi na kuwapa nafasi ya uwaziri.


Gazeti hilo lilimkariri mbunge huyo ambaye ameingia bungeni mwaka 2010 baada ya Uchaguzi Mkuu, akisema uteuzi wa Rais Kikwete kwa mawaziri haukumridhisha kwa kuwa wapo wabunge akiwamo yeye waliopaswa kupewa wadhifa huo kwakuwa wabunge wa muda mrefu.
 
Ngoja warudi walikotoka.
Hao bado hawajajikomboa fikra.
CCM ndo iliwaambia wajiunge vikundi wapewe pesa mamilioni JK.pesa za nchi alizochota akasema za JK.
Tena warudi kwao wataambulia t-shirts.kofia.kanga na buku tano kila ifikapo uchaguzi.nafikiri hiyo itasaidia kikundi chao.
 

Wakakope wapi wakati kila mkutano wa chadema viongozi wanakusanya harambee,kama nia yenu kusaidia kwanini msiwakopeshe hayo mabilioni ya harambee acheni hizo mtabainika tuu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 

Kama kila Mtanzania anacheza na mawazo ya mwenzake ili apate pesa hatutapata dira ya kutupeleka kwenye maendeleo. Siku hizi watz wanabadili hata dini kutafuta pesa hawa nao wasije kuwa walikuwa wanavizia pesa mahali zimekosekana sasa wanabadili muelekeo. Na huko nao wanawapokea bila kuijua dhamira yao ya dhati. Mimi siyo mtaalamu sana wa elimu ya tabia ya binadamu lakini???
 

walewale hawa, hawataki kufanya kazi wanakimbilia kwenye mikutano ya Ma...ba na kujidai upinzani hauna lolote ili wapate chochote kutoka huko.

Hivi hawa wamejiuliza zile ahadi lukuki alizoahidi JK enzi za kampeni zake ametekeleza ngapi hadi sasa?
Tulisikia bungeni kuwa hizo ahadi zinatekelezwa na serikali kupitia bajeti, basi na ahadi za huyo diwani zitatekelezwa na bajeti ya serikali. Sio kila ahadi zinaweza kutekelezwa na madiwani.
 

Tengua kauli usitutafutie ban,Mbeya vijana wanajituma sio ombaomba kama mlitaka mtubuluze kwakua hatuna misingi ya biashara wambie wajinga wenzio imekula kwenu,tunaitaji maendeleo ya watu na mji kwa ujumla,vizuri muwaachie wenye uwezo wa kubadilisha maisha ya vijana wa Mbeya,uchekbob na usharobaro wenu mwisho Moro

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
ata hivyo hao si walipandikizwa na magamba, kwan nan hafaham trick za kitoto kama hizo? Kama cdm imedhubutu kuwatimua madiwan wanafiki ndan ya chama kitu ambacho magamba hawajawahi kukifanya toka wawe madarakan, itakuwa hao tone moja ktk bahari.
 

Huoni hata aibu kuja hapa kujinadi kuwa unahitaji kuletewa maendeleo na mtu mwingine. MaCCM wamewaacha watu wa Mbeya mnaogelea tu kwenye mavumbi miaka yote we kwa akili yako ya samaki unahisi watawaendeleza leo. Maendeleo yanaletwa na wewe binafsi, kama huna business skills unasubiria kuletewa na CHADEMA au MaCCM huo ni ujinga wako binafsi, ambao CCM ndio wanautumia kuwadanganya. Subiri upewe Tshirt na Khanga kijana.
 
lile kontena lenye tshirt na kadi feki za chadema lilishaingia.
mwaka huu tutasikia wakisema hata wabunge wa chadema wamerudi CCM
tuliambiwa watrui wengi tu ktk mkutano wa Miwgulu Kibaha
inawezekana ni vijana wa CCM wenyewe wamejiunga na CCM kwa kupewa kadi feki za chadema
kama mwigulu kaweza kumfuata diwani mtarajiwa arudi CCM watashindwaje kutangaza habari za kisandiki kama hizi?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…