GE2025 Musa: Nitatoa ajira kwa vijana wa Mbarali

GE2025 Musa: Nitatoa ajira kwa vijana wa Mbarali

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
424
Reaction score
566
Katika kupunguza tatizo la ajira kwa vijana wa kata ya Lugelele, Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Mgombea Udiwani wa Kata hiyo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Musa Musa ameahidi kutoa ajira kwa vijana wa kata hiyo endapo atapewa idhini ya kuwa Diwani.

Musa ametaja ajira kwa vijana kama kipaumbele chake cha kwanza endapo atachaguliwa kuiongoza kata ya Lugelele, huku akiahidi kuifanya sekta ya afya na watumishi wake kuongeza ubora wa huduma kwa wananchi wa kata hiyo.

"Tukija kwenye suala la afya, hatuwezi kufanya kazi kama hatuna afya. Muda mwingine mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan anatuletea madawa, lakini ukienda muda mwingine unaambiwa dawa hakuna. Hiyo hospitali kama ipo ndani ya kata yangu, wale madaktari kama wapo ndani ya kata yangu basi wajiandae kufanya kazi kisaikolojia na mimi" Alisema Musa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbarali, Marry Mbwilo amepongeza jitihada za Mgombea udiwani Musa katika kata hiyo, huku akiwaomba wananchi wa kata ya Lugelele na Mbarali kiujumla kuwachagua wagombea viongozi wa CCM kuanzia Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Ubunge Bahati Ndingo na Musa Musa.

Ikumbukwe Musa Musa ni mgombea pekee wa Nafasi ya Udiwani, ambaye anahitaji kura za Ndio kutoka kwa wapiga kura wa kata ya Lugelele, ambapo kwa hatua nyingine Ndugu Musa Musa amewaomba wananchi wa kata hiyo kuwachagua Dkt Samia Suluhu Hassan na Mgombea Ubunge Bahati Ndingo.

 
Sasa badala ya kusema nitafanya angetwambia ni vipi atafanya ili hata asipokuwa au kabla hajawa tuanze kuyafanyia kazi mawazo yake....

Au yeye ndio ufunguo bila yeye hio Switch ya Ajira haifanyi kazi ?
 
Back
Top Bottom