Mkapa kinachotakiwa ni sheria kuchukua mkondo wake. Apelekwe mahakamani na labda huko ndiko akajitetee.
Mzee wazo lako ni zuri sana ... lakini ni chombo gani cha dola ambacho kiko tayari kumpeleka BWM mahakamani?
Mahakama zenyewe ndiyo hizi za Jaji Ramadhani ambazo mtu akipeleka kesi under private prosecution anatakiwa atoe evidence kwamba vyombo vya dola viligoma kushughulikia kesi hiyo na hivyo wanatumia vibaya fursa ya private prosecution (nina refer hukumu ya kesi ya Chitalilo).
Je, Mahakama zetu ni kweli ziko huru katika kushughulikia kesi nzito kama ya BWM? Kwanini Jaji Mkuu mstaafu Bwana Samatta aliropoka kwamba uhuru wa mahakama una walakini baada ya yeye kustaafu? Kwanini hakusema hayo wakati akiwa bado yuko ofisini?
The msg was clear kwamba katika mfumo wa kimahakama katika nchi nyingine ujaji mkuu unaenda kwa kufuata seniority na kwamba Rais hawezi kupingana na hilo na hivyo Rais anafanya kazi ya kuteua tu na hivyo jaji mkuu akiteuliwa na Rais haingiliwi katika utendaji kazi wake. Kwa case ya Tanzania hilo halipo (nina refer mahojiano ya Samatta na Gazeti la Tanzania Daima) hii ina maanisha kwamba kuna politics katika kuteua majaji na Jaji Mkuu.
Kwa mantiki hiyo Jaji Mkuu yeyote akiteuliwa lazima aende sambamba na matakwa ya serikali na hata ikibidi kupindisha sheria basi itapindishwa kwa kuwa hakuna chombo kingine kilicho na uwezo wa kutafsiri sheria za nchi zaidi ya mahakama na mahakama ya juu kabisa ndani ya nchi ndiyo yenye mamlaka ya mwisho ya kutoa tafsiri na hukumu ya kisheria. Whether sheria ilipindishwa kwa maslahi ya wachache au serikali hakuna tena anaeweza ku-question hukumu ya mahakama hiyo yenye maamuzi ya mwisho. Ndiyo maana kwenye case sensitive sana ambazo serikali ina maslahi, uteuzi wa majaji wa kusikiliza kesi hizo huwa unafanywa kwa makini sana na ikiwezekana kuweka majaji ambao ni pro-serikali ili wasije wakatoa maamuzi ya kuimaliza serikali! Je, kwa mtindo huu unategemea haki itendeke kwa Mkapa kushitakiwa kwenye mahakama ipi?
Kwenye hii issue ya Mkapa ninaona kuna ka-vicious circle fulani ambako kana ugumu fulani katika kukavunja. Swala la kwanza ni kwamba kwanini Mkapa alionyesha side yake wazi wakati wa mchakato wa kusaka mgombea urais mwaka 2005? Hotuba ya Mkapa ya Chimwaga kwenye Mkutano Mkuu kama mtu ukiisikiliza kwa makini ilikuwa na clear msg kwa wapiga kura ... Leo hii unategemea JK awaruhusu PCCB au Polisi wamchunguze Mkapa? Hata kama PCCB watamchunguza na kupeleka recommendations kwa DPP, bado DPP ana mamlaka makubwa sana ya kusema jalada halina kesi ya kujibu! Bado hata ukienda mahakamani under private prosecution unaweza kukumbana na kiini macho cha matumizi mabaya ya private prosecution. Hiyo vicious circle kuivunja ni kazi ngumu, kuna complications nyingi zaidi kwa kuwa kuna dalili zote za kulindana na JK alishasema wazi kwamba hana nia ya kuanza kuwachunguza marais wastaafu, kwanini atoe kauli kama hiyo kama utawala wake ni utawala wa sheria???????
Lakini yote haya yana mwisho na iko siku tutaona mwanga mwisho wa tanuru japo hajui urefu wa tanuru lenyewe!