G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,596
- 36,018
Vigogo watano waliosimamishwa kazi kutoka Bohari kuu ya madawa (MSD) pamoja na halmashauri mbili nchini wameula katika sekta binafsi huku wakilipwa mishahara ya kuanzia milioni mbili na nusukwa mwezi (take home). Aidha vigogo hao bado wameendelea kulipwa asilimia hamsini ya mishahara yao serikalini.
Hayo yanajiri huku kigogo mwingine aliyesimamishwa kazi TTCL akitarajiwa kusaini donge nono katika kampuni moja ya uzalishaji hapa nchini. Vigogo hao ambao majina yao yanahifadhiwa, wote kwa pamoja wanaendelea kulipwa nusu ya m ishahara yao ya awali pamoja na stahiki nyingine kama kawaida wakati ambapo tayari wameajiriwa ndani ya sekta binafsi.
Aidha kigogo mwingine wa TRA aliyesimamishwa kazi kwa kudaiwa kuhusika na wizi mkubwa wa mapato ndani ya shirika hilo naye ameula ndani ya kampuni moja kubwa ya madini nchini huku mshahara wake ukikadiriwa kufika milioni kumi na tano kwa mwezi!
Kuna haja ya kuliangalia upya swala hili!!!