Vigogo wa Serikali wakamatwa kuhusiana na uhalifu nchini Ethiopia

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Ethiopia imewakamata watu 63 wanaotuhumiwa kwa ufisadi na kukiuka haki za binadamu, wakiwemo maafisa wa upelelezi, wanajeshi na wafanyabiashara.

Kamata kamata hiyo ya vigogo ni matokeo ya amri ya waziri mkuu Abiy Ahmed ya kufanya uchunguzi wa miezi kadhaa, kuhusu uhalifu uliofanyika chini ya utawala wa watangulizi wake.

Mwendeshamashitaka mkuu wa serikali amesema baadhi ya waliokamatwa wanashutumiwa kuwatesa wafungwa wakiwalazimisha kukiri makosa, kuwabaka watu, kuwatesa kwa kutumia nyaya za umeme na hata mauaji.

Wengine wanakabiliwa na tuhuma za kutumia vibaya raslimali za kampuni ya vyuma inayomilikiwa na jeshi, ambapo mabilioni ya dola yaliporwa.

Katika operesheni hiyo, mkuu wa zamani wa ujasusi anatafutwa kwa kuhusika katika jaribio la kumuuwa waziri mkuu Abiy Ahmed tarehe 23 Juni. Tangu alipoingia madarakani mwezi Aprili, Abiy amewaachia maelfu ya wafungwa na kufanya mageuzi mengine makubwa ya kisiasa.
 
Salary Slip
 
Back
Top Bottom