Viongozi mashuhuri wa CUF wamejitoa katika chama hicho leo.Viongozi hao ni aliyekuwa meneja kampeni wa Urais wa Lipumba Bw Said Miraji na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Temeke kupitia CUF Bw Kadawi Lucas Limbu.Viongozi hao kwa pamoja wamesema wanajitoa CUF rasmi leo kutokana na vurugu kubwa zinazoendelea ndani ya chama hicho na pia wasingependa kuona chama hicho kikizikwa wakiwa bado wanachama.SOURCE: CHANEL TEN