mrangi
JF-Expert Member
- Feb 19, 2014
- 96,542
- 138,496
Alisema baadhi ya bodaboda wamekuwa wakipita kwenye taa nyekundu, kupakia ‘mishikaki’ na kutovaa kofia ngumu hatua ambayo huwasababishia vifo, kujeruhiwa na kupata ulemavu wa kudumu.
Hivyo aliwaagiza makamanda wote wa mikoa kuwakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria wote wasiofuata sheria za usalama barabarani ama kujihusisha na vitendo vya uhalifu.
Hana jipya ni mbwembwe za kawaida.Isiishie kwa bodaboda tu hata mabasi ya masafa marefu na kati, NOAH, Hiace wote hawa wanazidisha abiria na kuwasababishia madhara pindi zinapotokea ajali kwakuwa abiria wanaozidi hawafungi mikanda ya usalama
Jeshi la Polisi liwe na ukurasa maalumu kwenye tovuti yao kwaajili ya raia kufikisha malalamiko yao moja kwa moja kwa IGP, unakuta mtu amefungua jalada polisi, ili mpelelezi ainuke kwenye kiti lazima apewe booster