Vigogo kitengo cha ‘fraud’ wang’olewa

Vigogo kitengo cha ‘fraud’ wang’olewa

Mie Sirro simuheshimu sana kutokana na utendaji na kauli zake za huko nyuma vilivyonifanya nijiulize kama kweli ana busara za kumfanya awe kiongozi wa juu wa jeshi la Polisi.

Labda anaweza kuji-redeem.

Ushauri wangu wa bure kwa Sirro ni kwamba, akitaka afanikiwe sana na kulibadili jeshi la Polisi liwe na ufanisi wa hali ya juu Tanzania, Afrika na hata duniani, basi aongee na Raisi Magufuli kwamba ikiwa kweli Raisi una nia mie nikomeshe uhalifu nchini, basi uliache jeshi la Polisi liwe huru na lisitumike kabisa kisiasa. Sirro akilifanya jeshi la polisi liwe neutral na kuwatumikia Watanzania wote kwa usawa bila kujali itikadi zao za kisiasa, basi atafanikiwa sana na kupata ushirikiano wa juu wa wananchi utakaofanya iwe rahisi sana kukomesha uhalifu la kukuza hali ya usalama nchini.

Sirro (nilishasema sintamuita kamanda kwa kuwa kwangu hastahili kuitwa hivyo bado) anapaswa kujua kwamba karibu 70% ya Watanzania wanawachukia sana Polisi. Hawawaoni polisi kama wapo kwa ajili yao. Basi hana budi kuligeuza jeshi la Polisi lisiwe jeshi la Polisi la serikali ya Tanzania, bali Jeshi la Wananchi la Polisi (JWP). Akifanikisha hilo nitaanza kumuita Kamanda Sirro.

La sivyo Sirro umekuja utapita na baada yako tutakuwa na IGP mwingine na mambo yaleyale ya upuuzi mwingi wa polisi pamoja na kugombana na raia na wanasiasa wa upinzani na kukitumikia chama tawala.

Na Sirro, wambie askari wako wa trafiki kwamba kuanza kujenga uhusiano mwema na raia si lazima kila gari wanalolismamisha watafute kwa udi na uvumba losa la kutoza faini. Wanaweza kumsimamisha mtu, kuwasalimu vizuri watu walio kwenye gari, na kutoa ushauri tu juu ya makosa madogo madogo na kuwatakia safari njema. Unaweza kukuta ni indiketa moja imekufa - mwambie tu dereva unajua indiketa yako moja haifanyi kazi - ukifika nyumbani jitahidi uibadilishe isije ikakuletea madhara. Utashangaa impact itakayoletwa na hili ikiwa watalitekeleza. Si kila kosa linarekebishwa kwa fimbo - na fimbo zikizidi zinazaa kiburi na chuki.
Umewaza vizuri lakini sahau, Siro ni yule yule wa jana leo na hata kesho.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Umewaza vizuri lakini sahau, Siro ni yule yule wa jana leo na hata kesho.

Basi hata yeye sababu zilizomfanya IGP Mangu asifanikiwe na kutumbuliwa ndizo zitamfanya asifanikiwe na kutumbuliwa. It is just a matter of time - mwaka mmoja, miwili, na akijitahidi sana sana, mitatu!
 
Basi hata yeye sababu zilizomfanya IGP Mangu asifanikiwe na kutumbuliwa ndizo zitamfanya asifanikiwe na kutumbuliwa. It is just a matter of time - mwaka mmoja, miwili, na akijitahidi sana sana, mitatu!
Hatofika 2020 nakwambia, labda alambe miguu ya Bashite muda wote.
 
Sirro yupi aliyekua anatumikishwa na Makonda au sirro yupi IGP ni cheo tu akiri yake hiko vile vile
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Amebadilika sana, alitaka kufukuzwa na Bashite lakini sasahivi ni ndiyo kwa kila jambo.
Bashite alimuandama sana siro name siro alijishusha.
Lakini kitendo cha mkulu kumteua siro kuwa IGP,bashite ajiangalie.
 
Naona kamanda ameanza kulipa fadhila kwa 'marafiki zake' na kushusha rungu kwa 'mahasimu wake'... Safi, kiongozi yeyote aliyezaliwa na mwanamke angefanya vivyo hivyo... Hata ingekuwa mimi...
 
Polisi wajirekebishe wajenge ukaribu na raiaa

Ova
Kama hawa
92fdac7e985474259a2a72f936ddc038.jpg
08721bcf1d24cd8876fa45b76b4edb66.jpg
a419c89e8d474123f24b68739e39b072.jpg
 
Back
Top Bottom