Vigogo Ilala waburuzwa kortini bomoabomoa ya Tabata Dampo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo Ilala waburuzwa kortini bomoabomoa ya Tabata Dampo

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Jul 7, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,231
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Vigogo Ilala waburuzwa kortini bomoabomoa ya Tabata Dampo
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Tuesday, 05 July 2011 20:54 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Hadija Jumanne
  VIGOGO sita wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, akiwamo aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa manispaa hiyo, John Lubuva na Naibu Meya, Mohamed Yakub, wamepandishwa kizimbani kujibu shtaka la kula njama na kuisababishia Serikali hasara ya Sh1.76 bilioni.

  Vigogo hao wanakabiliwa na shtaka hilo pamoja na maofisa wengine wanne wa manispaa hiyo ambao ni Mhandisi Mkuu wa Idara ya Maji, Idd Kisisa, Mkuu wa Idara ya Sheria na Ulinzi, Anderson Msumba, Mwanasheria Andrew Kanonyele na Mkadiriaji wa Ardhi na Majengo, Romuald Lutinah.

  Walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jana kwa makosa hayo ambayo yametokana na kupanga na kuendesha bomoabomoa eneo la Tabata Dampo jijini Dar es Salaam, mwaka 2008 kinyume na sheria.

  Mbele ya Hakimu, Joyce Minde, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Isdory Kiando alidai kuwa Februari 29, mwaka 2008 kwa pamoja, washtakiwa hao walikula njama na kutenda kosa la uvunjaji wa nyumba za makazi ya watu katika kiwanja namba 52 kilichopo Barabara ya Mandela eneo la Tabata, jijini Dar es Salaam.

  Kiando ambaye alikuwa akisaidiwa na Allan Kasamala aliendelea kudai kuwa katika shtaka la pili washtakiwa hao kwa pamoja, walitumia vibaya ofisi walizopewa kuzisimamia, kinyume na kifungu namba 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

  Waendesha mashtaka hao waliendelea kudai mahakamani hapo kuwa kwa pamoja washtakiwa hao walikiuka mipaka iliyowekwa na mamlaka husika na kubomoa nyumba za wakazi wa eneo hilo katika kiwanja namba 52 Barabara ya Mandela eneo la Tabata kinyume cha sheria.

  Katika shtaka la tatu ilielezwa kuwa washtakiwa hao kwa pamoja, waliingizia Serikali hasara ya Sh1.760 bilioni kwa uamuzi huo, fedha ambayo Serikali iliitumia kuwalipa fidia wakazi hao wa Tabata.

  "Kupandishwa kizimbani kwa vigogo hao kunafuatia hasara waliyoisababishia Serikali kutokana na uamuzi wao mbovu wa kubomoa nyumba za wakazi 90 kinyume cha sheria katika eneo la Tabata Dampo jambo liloilazimu Serikali kuwalipa fidia wakazi hao," alidai mwendesha mashtaka huyo na kuendelea: "Tukio hilo lilotokea mwanzoni mwa mwaka 2008, liliilazimu Serikali kulipa zaidi ya Sh1.7 bilioni kama fidia kwa wakazi hao."

  Hata hivyo, washtakiwa wote baada ya kusomewa mashtaka hayo walikana kosa na kesi hiyo iliahirishwa hadi hadi Julai 19 mwaka huu. Washtakiwa wote wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwasilisha hati za mali zenye thamani ya Sh880 milioni ambazo ni nusu ya pesa walizoshtakiwa nazo. Mwanzoni mwa mwaka 2008, Serikali ililazimika kulipa fidia zaidi ya wakazi 90 waliokuwa wakiishi katika eneo la Tabata Dampo baada ya nyumba zao kubomolewa.

  Serikali ililazimika kuwalipwa fidia wakazi hao baada ya tume iliyoundwa kubaini kuwa hawakuvunjiwa nyumba zao kihalali. Tume hiyo iliundwa baada ya Manispaa hiyo kulaumiwa kwa kuendesha bomoa bomoa hiyo bila kufuata taratibu na sheria. Katika fidia hiyo kila mkazi aliyebomolewa nyumba alilipwa TSh 20 milioni pamoja na kiwanja katika eneo la Buyuni Chanika.

  Baada ya kutokea kwa sakata hilo, Serikali iliamua kumuadhibu Mkurugenzi huyo kwa kumuhamisha kituo cha kazi na kwenda mkoani Shinyanga. Hata hivyo, wananchi walikilalamikia kitendo hicho. ENDS
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,231
  Trophy Points: 280
  hivi sera za Nyerere kuhamisha hamisha watendaji wabovu serikalini kumbe ndiyo sera ya sirisiri ndani ya CCM....kwa nini watajwa hawa hawakuchukuliwa hatua za kinidhamu kwanza kabla ya kupewa uhamisho............................... I beg to question......................
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  duuu Msumba Anderson homeboy halafu tumeoa kwenye ukoo mmoja aisee wakati ule 2008 jamaa walimuhamishia mtwara baada ya lile sakata kufunikwa. sasa naona limeibuliwa upyaa duh mme mwenzangu atapona kweli hapo?
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,335
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  This is a soft reminder that uongozi ni dhamana...tusijisahau tukiwa madarakani wajameni
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Tuombe heri kuwe na ushahidi wa kutosha pasi na shaka hili hawa watu waingie hatiani. Isije ikawa kiini macho tu.
   
 6. mwanatanu

  mwanatanu JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45

  Jamani kesi iliishia wapi?
   
Loading...