Vigogo chuo cha uhasibu Arusha mbaroni

Vigogo chuo cha uhasibu Arusha mbaroni

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,455
vigogo.jpg

Vigogo 11 akiwamo Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (AA), Profesa Johannes Monyo, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha jana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa kosa la uhujumu uchumi na kuisababishia hasara serikali. Katika shtaka la kwanza, Profesa Monyo na mwenzake Jerome Augustine ambaye ni Mkuu wa Idara ya Ununuzi chuoni hapo wanadaiwa kutumia vibaya madaraka yao kwa kuhamisha umiliki wa Solar Power Back-up Kit yenye thamani ya Sh6.2 milioni, mali ya chuo na kuifanya mali binafsi ya mkuu huyo wa chuo.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Wakili Kilongozi Adama aliyekuwa akisaidiana na Wakili Hamidu Simbano alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Mustapha Sayani kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo Septemba 30, 2011 kinyume cha kifungu cha 31 cha sheria namba 11 ya kuzuia na kupambana na rushwa ya mwaka 2007.

Shtaka la pili linawakabili wajumbe wa bodi ya zabuni wa chuo hicho, Jerome Augustine, Chacha Wambura, Mpoki Mwasaga, Papias Njaala, Mathew Melita, Mary Thomas, Elisaria Kisanga na Gerald Malisa ambao kwa pamoja wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya kwa kuruhusu ununuzi wa kifaa hicho cha Umeme Jua kinyume cha sheria.

Katika shtaka la tatu, Wakili Adam alidai kuwa kati ya Novemba Mosi na 30, mwaka 2011, washtakiwa Jerome Augustine, Faraji Mnyepe na Honory Mkelemi walitumia madaraka yao vibaya kwa kusaidia malipo ya Sh6.2 milioni kwa ajili ya kifaa hicho cha umeme jua kinyume cha sheria.

Shtaka la nne linawakabili washtakiwa Johannes Monyo na Jerome Augustine wanaodaiwa kuwa mnamo Julai 26 na Novemba 30, mwaka 2011, kwa pamoja wakiwa waajiriwa wa Chuo cha uhasibu, waliisababishia taasisi hiyo hasara ya Sh. 6.2 milioni kinyuma cha kifungu cha 31 ya sheria namba 11 ya makosa ya kupambana na kuzuia rushwa ya mwaka 2007.

Kabla ya kuwasomea watuhumiwa mashtaka yao, Wakili Adam aliiomba Mahakama kutoa hati ya kuwakamata washtakiwa namba tano Mpoki Mwasaga, namba Saba Mathew Melita na namba 10 Gerald Mkelemi ambao hawakuwepo mahakamani jana, ombi lililokubaliwa kwa Hakimi Siyani kutoa hati hiyo.

Upande wa mashtaka pia uliomba kubadilisha jina la mshtakiwa wa nne Chacha Wambura ambaye awali jina lake liliandikwa Chacha Makamba Augustine, Mahakama ilikubali ombi hilo.

Upelelezi wa shauri hilo lililovutia umati mkubwa wa wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo cha Uhasibu umekamilika na itatajwa Agosti Mosi, mwaka huu ambapo washtakiwa watasomewa maelezo ya awali ya kosa.

Awali kabla ya Mahakama kuanza, kulitokea mvutano kati ya kundi la waandishi wa habari, ndugu, jamaa, marafiki na wapambe wa watuhumiwa waliokuwa wakijaribu kuzuia upigaji wa picha kabla ya hakimu kuingia.

Chanzo: GAZETI LA MWANANCHI
 
Sh6.2 milioni inawatoa roho ma prof amakweli njaa mbaya
 
Hakuna kitu hapo,Tunataka wezi wa Escrow,Meremeta,EPA,richmond wakamatwe na si hizi drama za kukamata vidagaa.watu 10 pesa yenyewe mil 6 tu?????

Mkubwa umesahau kwamba Dr. Hosea (Dakika 45 ITV)alisema kukamata papa kwenye deep sea inahitaji vifaa na uwezo mkubwa watawndelea kukamata dagaa wadogo wadogo kwa7bu ni rahisi kukamatika.
 
Hakuna kitu hapo,Tunataka wezi wa Escrow,Meremeta,EPA,richmond wakamatwe na si hizi drama za kukamata vidagaa.watu 10 pesa yenyewe mil 6 tu?????

Inashangaza kwa kweli kwamba eti kifaa ambacho kilinunuliwa kweli na kipo wala sio hewa kinapewa publicity kubwa sana na ambacho eti thamani yake ni Millioni 6. Hapa nafikiri kuna agenda ya siri juu ya hii kesi, si bure. Natabiri hawa watu hawaendani na matakwa ya CCM ndio maana wametundikwa. Kama M4Cjb ulivyosema, mbona hatujaona wezi wakubwa waliokwapua mamilioni wakifikishwa mahakamani? Eti millioni 6 ni kesi ya uhujumu uchumi?

Kuna kitu hapa.

Tiba
 
6200000 / 10 = 620000 eti wahujumu uchumi, nchi hii bwana sinema zimezidi, hii takukuru inatumia tu kodi zetu bure kama hii ndio kazi yao... itabidi hii taasisi ivunjwe tu maana haina faida katika taifa hili masikini zaidi ya kuongeza hizo hasara.

6.2 mil skendo watu wanakamatwa na serikali inajifanya inafanya kazi kweli hapa, halafu 200bill watu wanvimba shingo bungeni kutetea,, poleni sana wezi wa huo mtambo wa 6.2 mill kwa kusumbuliwa maana nyie ndio kafara na sehemu za serikali yetu tukufu kuonyesha inafanya kazi na kuwajali wananchi wake..... next time na nyie muibe nyingi kuanzia 1bill na kuendelea hapa kwetu tanzania ni shambani...........
 
Hakuna kitu hapo,Tunataka wezi wa Escrow,Meremeta,EPA,richmond wakamatwe na si hizi drama za kukamata vidagaa.watu 10 pesa yenyewe mil 6 tu?????
ueona hawa jamaa wanataka kutuhamisha kwenye ishu za msingi
 
Huyu prof ndiye aliyesababisha wanachuo kufukuzwa na kukatisha masomo wakati wa sakata la RC vs Lema na wana IAA?
 
Yaan CCM inajenga nchi kwa kukomaa na 6.2M wakati billions za Escrow wanawakumbatia wezi.
Huu ni upuuzi kabisa
 
Je K.i.n.a.n.a watamkamata lini arudishe mashine za kufulia alizowaibia Mount Meru Hospital?
 
Nchi itayumba vipi mkuu kwani hao ndio nguzo kuu ya nchi yetu?fafanua kidogo

Hao wakikamatwa watamtaja waliyeshirikiana nae na yeye ana kinga ya kutoshitakiwa kikatiba kwa kutoshitakiwa huyo mkuu wao watasababisha malalamiko yatakayosababisha vurugu na nchi kutotawalika tena.
 
hiku ni kichekesho kingine...yale mapapa ya 6.2 trilioni mbona hayakamatwi?
 
Kupeleka wezi wa kuku mahakamani na kuwaacha mabilion yakiibwa na DOWANS, RADA....

Wanafunzi wa vyuo vikuu kukosa mikopo

-Pesa za walipa kodi wa Tanzania kuibwa mfano EPA, DOWANS, Escrow, RADA n.k

-Pesa kutoroshwa nje ya nchi - Mabillion ya Uswisi

-Tanzania kuwa kitovu cha biashara ya Madawa ya kulevya

-Twiga kutoroshwa nje ya nchi...

- Watu kutekwa na kuuawa

-Katiba ya nchi imevunjwa - Rasilimali za nchi zinaibwa na Raia hawapati usalama
 
Vigogo 11 akiwamo Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (AA), Profesa Johannes Monyo, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha jana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa kosa la uhujumu uchumi na kuisababishia hasara serikali. Katika shtaka la kwanza, Profesa Monyo na mwenzake Jerome Augustine ambaye ni Mkuu wa Idara ya Ununuzi chuoni hapo wanadaiwa kutumia vibaya madaraka yao kwa kuhamisha umiliki wa Solar Power Back-up Kit yenye thamani ya Sh6.2 milioni, mali ya chuo na kuifanya mali binafsi ya mkuu huyo wa chuo.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Wakili Kilongozi Adama aliyekuwa akisaidiana na Wakili Hamidu Simbano alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Mustapha Sayani kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo Septemba 30, 2011 kinyume cha kifungu cha 31 cha sheria namba 11 ya kuzuia na kupambana na rushwa ya mwaka 2007.

Shtaka la pili linawakabili wajumbe wa bodi ya zabuni wa chuo hicho, Jerome Augustine, Chacha Wambura, Mpoki Mwasaga, Papias Njaala, Mathew Melita, Mary Thomas, Elisaria Kisanga na Gerald Malisa ambao kwa pamoja wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya kwa kuruhusu ununuzi wa kifaa hicho cha Umeme Jua kinyume cha sheria.

Katika shtaka la tatu, Wakili Adam alidai kuwa kati ya Novemba Mosi na 30, mwaka 2011, washtakiwa Jerome Augustine, Faraji Mnyepe na Honory Mkelemi walitumia madaraka yao vibaya kwa kusaidia malipo ya Sh6.2 milioni kwa ajili ya kifaa hicho cha umeme jua kinyume cha sheria.

Shtaka la nne linawakabili washtakiwa Johannes Monyo na Jerome Augustine wanaodaiwa kuwa mnamo Julai 26 na Novemba 30, mwaka 2011, kwa pamoja wakiwa waajiriwa wa Chuo cha uhasibu, waliisababishia taasisi hiyo hasara ya Sh. 6.2 milioni kinyuma cha kifungu cha 31 ya sheria namba 11 ya makosa ya kupambana na kuzuia rushwa ya mwaka 2007.

Kabla ya kuwasomea watuhumiwa mashtaka yao, Wakili Adam aliiomba Mahakama kutoa hati ya kuwakamata washtakiwa namba tano Mpoki Mwasaga, namba Saba Mathew Melita na namba 10 Gerald Mkelemi ambao hawakuwepo mahakamani jana, ombi lililokubaliwa kwa Hakimi Siyani kutoa hati hiyo.

Upande wa mashtaka pia uliomba kubadilisha jina la mshtakiwa wa nne Chacha Wambura ambaye awali jina lake liliandikwa Chacha Makamba Augustine, Mahakama ilikubali ombi hilo.

Upelelezi wa shauri hilo lililovutia umati mkubwa wa wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo cha Uhasibu umekamilika na itatajwa Agosti Mosi, mwaka huu ambapo washtakiwa watasomewa maelezo ya awali ya kosa.

Awali kabla ya Mahakama kuanza, kulitokea mvutano kati ya kundi la waandishi wa habari, ndugu, jamaa, marafiki na wapambe wa watuhumiwa waliokuwa wakijaribu kuzuia upigaji wa picha kabla ya hakimu kuingia.

GAZETI LA MWANANCHI

Wa EPA 130 Bil waliombwa kwa kubembelezwa warudishe, wa AIA waliojihamishia solar backup kit ya shilingi Mil 6.2 wameshtakiwa. Tanzania nakupenda.
 
Inashangaza kwa kweli kwamba eti kifaa ambacho kilinunuliwa kweli na kipo wala sio hewa kinapewa publicity kubwa sana na ambacho eti thamani yake ni Millioni 6. Hapa nafikiri kuna agenda ya siri juu ya hii kesi, si bure. Natabiri hawa watu hawaendani na matakwa ya CCM ndio maana wametundikwa. Kama M4Cjb ulivyosema, mbona hatujaona wezi wakubwa waliokwapua mamilioni wakifikishwa mahakamani? Eti millioni 6 ni kesi ya uhujumu uchumi?

Kuna kitu hapa.

Tiba

There must be political motives behind this
 
Back
Top Bottom