Vifurushi vipya vya mitandao: TCRA yatoa tamko na maagizo kwa makampuni ya simu

Solution sio chama fulani kuwa madarakani au laa! Hapo tatizo kubwa ni watu(viongozi) wa hivyo vyama kuchanganya uongozi/siasa na biashara! Hapo ndio tunasema conflicts of interest! Hapo haijalishi ni chama gani kinaendesha serikali ila watu wachache kwenye serikali wanaangalia maslahi yao binafsi.

Hiyo mitandao mingine hawewezi kuiombea TTCL ife, bila TTCL hakuna hiyo mitandao mingine, mfano Airtel na Voda wanatumia minara ya TTCL kwenye transmission zao, Tigo pia huko remonte area wanatembelea signal za hao jamaa!

Kwenye data(internet)ndio kabisaa mitandao yote wanategemea server za TTCL manake ndio wana artitecture na infrastructure nzuri za ku supply hizo data so wanategemeana!

Tatizo ni ufisadi wa watu wachache waliokuwa wanakula hizo pesa na kushindwa kuiendeleza TTCL ndipo MH.Zitto kuwalipua ndio fasta wakaja na huo mpango wakupunguza packages zao! Na data ndio ili-affectika zaid manake hiyo mitandao bado haina mifumo mizuri ya ku supply huduma ya bundles so walipewa data kwa real price tofauti na wizi wa bundle wa awali ndio maana wakazipunguza.

Ndio maana ukifuatilia utaona kwenye packages sms na dakika za muda wa maongezi kuna badiliko ndogo sana, ila MB's ndio kwenye utata!

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums

kama ni hivo basi namuona TTCL anajiandaa kuwa muuza MB itakua poa tu
 
Mkuu hambacho hujaelewa ni nini haswa..

Yaani silielewi tamko lenyewe, naona kama wanakubaliana na mwizi kutuibia, na wanamuomba mwizi next time atoe taarifa in advance. Ndio maana naomba upost tena pengine kuna mstari hukuukopi vizuri ili this time around ukopi.

Samahani kama itakuwia usumbufu.
 
kama ni hivo basi namuona TTCL anajiandaa kuwa muuza MB itakua poa tu

TTCL wana broadband zao nzuri tu, na gharama yao ni nafuu! Nadhani ni 50k kwa mwezi na ni unlimited data, na wana speed nzuri tu!

Safi kwa matumizi ya nyumbani, hata ofisi ndogo isiyozidi computer tano! Uta enjoy huduma zao za net vizuri! Pia kuna package mbali mbali za usiku ambazo unapata GB's nyingi sana kwa bei chee na kasi ya ajabu!

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums
 
naomba kuuliza..
internet inanunuliwa wapi mpaka kufika kwenye mitandao ya simu...kama inawezekana watu waanzishe makampuni ya kuuza MB..

Ukweli ni kwamba internet haiuzwi, huduma yake ni ya bure duniani kote. Isipokuwa ili utumie hiyo huduma ni lazima uunganishwe. Kwa hiyo tunacholipia ni gharama ya kuunganishwa kwenye internet ili uweze kitumia huduma iliyoko huko. Waunganishaji wanatumia mfumo fulani unaowawezesha kupima gharama za kuunganishwa wateja wao kama vile muda wa kutumia internet, muda wa kuperuzi na kiasi cha Data ulizopakua. Kwa hiyo wanachofanya mitandao ya simu ni kituwezesha kuifikia hiyo internet ili tuzitumie huduma mbali mbali zilizoko kwenye internet.
 
Haya Vodacom tumewasemea kwa mkubwa wetu TCRA .. Amewaagiza mtuulize tunataka nini na kwa bei gani . Sio kutupangia tu.

Mimi nata 1GB kwa shilingi za Kitanzania 500 tu.. Sitaki mniulize tena chukueni hiyo mkalifanyie kazi.

Anyway!

TCRA wanapaswa kujua kuwa wananchi hatuna haja ya kujua hizo data alizotuletea, tunahitaji unafuu ktk hizi huduma.

Hili ni tamko dhaifu na linaonyesha Unyonge tulionao.
 
Ukweli ni kwamba internet haiuzwi, huduma yake ni ya bure duniani kote. Isipokuwa ili utumie hiyo huduma ni lazima uunganishwe. Kwa hiyo tunacholipia ni gharama ya kuunganishwa kwenye internet ili uweze kitumia huduma iliyoko huko. Waunganishaji wanatumia mfumo fulani unaowawezesha kupima gharama za kuunganishwa wateja wao kama vile muda wa kutumia internet, muda wa kuperuzi na kiasi cha Data ulizopakua. Kwa hiyo wanachofanya mitandao ya simu ni kituwezesha kuifikia hiyo internet ili tuzitumie huduma mbali mbali zilizoko kwenye internet.

hapa unazidi kunielimisha kumbe tatizo ni mitambo yao tu yakutugawia MB..kwahyo MB zilivokua nyingi ilikua inafanya kazi vizuri tofauti na sasa MB zilivo pungua, au ukanjanja
 
Utaelewa wapi? wakati mimi nakuja hadi kwenu na shule ulifeli form two.
wewe uliyefaulu Form two umeelewa wapi ambako pameandikwa au Tamko hilo la TCRA?
Bundle zimepanda Je TCRA
  • WAMEPUNGUZA
  • WAMEKEMEA?
  • WAMEREKEBISHA? WAMEFURAHIA BEI IMEONGEZEKA
"TCRA inawashauri watumiaji wa huduma za
mawasiliano kuchagua vifurushi na mpangilio wa tozo
ambao unafaa kwa matumizi yao. Watumiaji
wanatakiwa kudai taarifa kamili kuhusu huduma
wanazozilipia na waelewe taarifa za watoa huduma
kuhusu bei na tozo, ikiwa ni pamoja na vigezo na
masharti ya huduma. Mtumiaji asiporidhishwa na huduma
anayopata anatakiwa alalamike – kwanza kwa mtoa
huduma wake, na asiporidhika na ufumbuzi awasilishe
malalamiko yake TCRA," imesisitiza
.
mbona post nzima ni blahblah haieleweki?
 
Wapi ahadi ya viongozi wakuu wa serikali kua kufikia mwaka 2015 gharama za mawasiliano zikiwamo internet zitapungua maradufu,matokeo yake ndio zimeongezeka kwa 150%. Au ni agizo toka serikalini kujaribu kuminya uhuru wa watu kupeana habari??kama ni hivyo haitasaidia,imeshakua too late,sana sana ndio mnazidi kuwapandisha wananchi hasira,na watawaadhibu vibaya sana kwenye sanduku la kura!ni serikali gani isiyo na uwezo wa kutetea wananchi yake dhidi ya wafanyabiashara wenye uchu??nini msaada wa serikali kwa wananchi wake?yaani makampuni ya simu yawe na nguvu na sauti kwa kujiamulia yatakavyo kuliko serikali?hiki ni kichekesho sana,na nahisi kuna kitu nyuma ya panzia
 
hivi mkonga wa taifa unafanya kazi kweli? manake tuliambiwa gharama za internet nk zitapungua kwa kiasi kikubwa

NAUNGANA NAWE . TCRA vibaraka tu, au mkongo wa taifa bado haujakamilika?
 
Hata voda wana internet bila kikomo kwa gharama ya sh.elfu moja tu Matola. Hapa tunajadili issue ya bundle lenye kujumuisha sms, dakika na internet.
 
mkuu umeongea vema hapo.. Kwa mujibu wa sheria zinazotawala soko huria haitakiwi makampuni hasimu kukaa pamoja na kupanga bei ya bidhaa zao.. Hapa ndipo tcra watupe ufafanuzi wa hatua zipi watayachukulia haya makampuni kwa kula njama na kupanga bei za pamoja..

Hayo mengine yote ni blah blah..

100% agree!
 
Tuliambiwa Mkonga wa mawasiliano utapunguza bei za internet na kuongeza kasi ya internet.

Naona imekuwa kinyume bei juu speed ile ile. Siku hizi kila kitu ni danganya toto
 
Porojo nyingi facts hewa, sasa hizi takwimu zinatuhusu nini sisi? Tamko gani limekaa kimama mama? Hivi January makamba bado tu anataka urais?
 
Bei za bundle zitashushwa baada ya kipindi cha chaguzi za mwaka huu kupita.
 
Mkuu carter umeelezea vizuri ila kuna sehemu umepwaya iyo conflict of interest ndo inayoleta matatizo sio!
ikiwa TTCL ina mitambo mizuri mpaka makampuni mengine ya simu yanategemea minara yake kwanini TTCL haipo kwenye ushindani?

TTCL ni shirika la serikali na serikali inaongozwa na CCM mafisadi wanaihujumu TTCL ili ife wapole mali waendeleze company zao.

Tunaitaji viongozi waadilifu CCM ikipigwa chini ndo tutapata mabadiliko vinginevyo ni maumivu tu kwenda mbele.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom