Vifurushi vipya vya mitandao: TCRA yatoa tamko na maagizo kwa makampuni ya simu

nijothemaster

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
324
56
Mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA imetoa tamkokuhusiana na malalamiko kutoka kwa watumiaji wahuduma za simu nchini kufuatia kubadilika kwa vifurushivya mawasiliano. Malalamiko hayo yalikuja baada ya baadhi ya mitandaoya simu kupunguza ukubwa wa data anazopata mtumiajiwa simu anapojiunga na vifurushi vya muda wamaongezi, sms na data kwa pamoja.

Baadhi ya mitandao imekuwa ikitoa Mega Bytes 8 pekeyake ambazo kwa matumizi ya kawaida ni ndogo mno."TCRA imechambua mpangilio wa vifurushi – tozo za zamani na mpya na kugundua kwamba ingawaje baadhiya watoa huduma wamebadilisha bei, kwa ujumla bei za muda wa kuzungumza na idadi ya meseji hazikubadilika sana.

Hata hivyo, kuna upungufu mkubwa kwa idadi yauniti za data (MBs)," amesema Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Jumanne.

Kupitia kifungu cha 5 cha Kanuni za tozo (EPOCA Tariff Regulations) za mwaka 2011, TCRA imeyataka makampuni ya simu kuwasilisha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania gharama mpya wanazokusudia kutoza wateja wao kabla hazijaanza kutumika.

Pia imeyataka kupitia upya bei na tozo mpya kwa kuzingatia mapendekezo hayo na kuwasilisha kwa Mamlaka kama inavyotakiwa kwa mujibu wa Kanuni za EPOCA za 2011 kuhusu tozo.

"TCRA inawaagiza watoa huduma kuhakikisha kwambamabadiliko yoyote yanatekelezwa kidogo kidogo na sioya ghafla ili kuepuka sintofahamu katika soko'' imesema. "TCRA inawaagiza watoa huduma kuwapa wateja waonafasi ya kuchagua mpangilio wa vifurushi tofauti kwahuduma wanazohitaji: Kifurushi cha mazungumzo, Meseji na Intaneti cha siku, siku saba au mweziambacho kinampa mtumiaji uhuru wa kuchagua kiasiambacho wako tayari kulipia kwa mazungumzo, mesejina intaneti.

"TCRA inawashauri watumiaji wa huduma zamawasiliano kuchagua vifurushi na mpangilio wa tozoambao unafaa kwa matumizi yao. Watumiaji wanatakiwa kudai taarifa kamili kuhusu hudumawanazozilipia na waelewe taarifa za watoa hudumakuhusu bei na tozo, ikiwa ni pamoja na vigezo na masharti ya huduma.

Mtumiaji asiporidhishwa na huduma anayopata anatakiwa alalamike – kwanza kwa mtoa huduma wake, na asiporidhika na ufumbuzi awasilishe malalamiko yake TCRA," imesisitiza. "Watumiaji wanashauriwa kuchukua fursa ya soko huriala mawasiliano nchini kama nafasi ya kulinganisha huduma na bei za watoa huduma na vifurushiwanavyouza kabla ya kuamua kujiunga na kifurushichochote au huduma yoyote.

Watumiaji wa simu janjazinazowezesha matumizi ya huduma nyingi, maarufukama "smart phone", kuwa makini wakati wa kuzitumia.Wahakikishe kwamba wanazima maeneo ambayoyanaweza kutumia data hata kama wakati huohawatumii vifurushi vya data walivyonunua kwenyevifurushi."

Katika hatua nyingine taarifa hiyo imetoa takwimu yakuongezeka kwa matumizi ya simu na internet nchini katika kipindi cha miaka 10. Imesema hadi sasa kuna laini za simu za mkononi zipatazo 31,862,656 ukilinganisha na laini 2,963,737 mwaka 2005."

Idadi ya simu za mezani ni 151, ukilinganisha na 154,420 mwaka 2005. Watumiaji wa intaneti wameongezake hadi kufikia 11,000,000 Desemba 2014kutoka 3,563,732 mwaka 2008. Kwa sasa, kuna hamukubwa ya matumizi ya intaneti na mwelekeo huu utaendelea; hasa kutakapokuwa na ongezeko la mitandao inayowezesha kutoa huduma za intaneti; nakuongezeka kwa mitandao ya jamii," imesema.

"Wateja walionunua laini au ambao wanatumia huduma za simu kwa kuzungumza imeongezeka kwa asilimia 91 kutoka milioni tatu (3,000,000) mwaka 2005 hadimilioni 32 ( 32,000,000) mwaka 2014. Hii imewezeshahuduma za simu kufikia asilimia 97 ya Watanzania ilipofika Desemba 2014; kutoka asimilia 10 mwaka 2005.

Kwa upande mwingine, muda wa kuzungumza kwasimu, ukiwa umepimwa kwa dakika zinazotumika, umeongezeka sambamba na ongezeko la idadi ya watumiaji. Umefikia dakika bilioni 41 kutioka dakika milioni 506 mwaka 2005," imeongeza mamlaka hiyo.

"Matumizi kwa upande wa meseji, yaani SMS na datapia yameongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka SMS zipatazo milioni 5 mwaka 2005 hadi SMS bilioni 10 mwaka 2014. Watumiaji wa intaneti wanaotumia simu za mkononi sasa wanafikia milioni 10."

Source: Bongo 5

===================

TAARIFA KWA UMMA

KUHUSU TOZO KWENYE SEKTA YA TEHAMA

Katika wiki ya pili ya Februari 2015, baadhi ya watoa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi walianzisha vifurushi vya mawasiliano na bei na kusabababisha malalamiko kutoka kwa watumiaji na umma kwa ujumla. TCRA, kwa kuzingatia upeo wa shughuli zake, imechambua hali hiyo na inapenda kutoa maelezo na maagizo ambayo yatawezesha kuondoa sintofahamu iliyopo na kujenga mustakabali kwa siku zijazo.

Kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003, miongoni mwa kazi za TCRA ni kufuatilia utoaji wa huduma katika sekta inazozisimamia kwa kuzingatia kiwango cha upatikanaji wa huduma hizo, ubora na viwango vya huduma, bei ya huduma na kuhimiza ushindani na ufanisi wa kiuchumi. Katika kutelekeza majukumu yake, TCRA inawajibika kupitia na kuchambua, mara kwa mara, utoaji wa huduma katika sekta na kuchukua hatua dhidi ya chochote kinachotokea kwenye soko, kiwe chanya au hasi.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inaongozwa na Sera za Kisekta, Sheria ya Mamlaka ya Mawasilioano Tanzania ya 2003, Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta (EPOCA) ya 2010, na Kanuni zake za mwaka 2011 zilizotungwa kwa kuzingatia matakwa ya EPOCA. Kifungu 6(1) cha Sheria ya TCRA kinaitaka Mamlala kufuatilia utoaji wa huduma unaofanywa na sekta inazozisimamia ikiwa ni pamoja na upatikanaji, ubora na viwango vya huduma, gharama za huduma hizo na kufanikisha ufumbuzi na utatuaji wa malalamiko na migogoro. Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kuhusu tozo mpya zilizotangazwa na makampuni ya simu za mkononi.

Habari zaidi Soma kiambatanisho hapa chini
attachment.php
 
afadhali kama kutakuwa na punguzo la bei na ongezeko la ukubwa wa muda wa maongezi na sms. Maana Vodacom imevuruga saana wateja. kutoka sh 250 bei inapanda had 500 ghafla tu hata bila taarifa. Wateja tunapelekeshwa kama gari ambalo halijui dereva ataamua lielekee wapi. ni majanga sana
 
naomba kuuliza..
internet inanunuliwa wapi mpaka kufika kwenye mitandao ya simu...kama inawezekana watu waanzishe makampuni ya kuuza MB..

Wananunua TTCL, nadhani kuna mbunge alifichua ufisadi wa TTCL hasa kwenye mauzo ya data na kutumika kwa mitambo yao ya tramsmission kwa hizi kampuni za simu za mikononi! Hapo ndio mitandao ikapunguza data(MB) kwenye packages zao.

Serikali ingeiwezesha TTCL wawe na micro chip(sim card) ndogo kama za hii mitandao mingine kuendeleza ushindani sokoni. Nadhani ingewasaidia kuongeza mapato yao. Kama ilivyo ZANTEL Zanzibar.

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums
 
aise kumbe TTCL ndo wana MB...hivo kama nkitaka kwenda kununua na kufungua kampuni yangu ya kuuza MB tu si inawezekana?
 
Wananunua TTCL, nadhani kuna mbunge alifichua ufisadi wa TTCL hasa kwenye mauzo ya data na kutumika kwa mitambo yao ya tramsmission kwa hizi kampuni za simu za mikononi! Hapo ndio mitandao ikapunguza data(MB) kwenye packages zao.

Serikali ingeiwezesha TTCL wawe na micro chip(sim card) ndogo kama za hii mitandao mingine kuendeleza ushindani sokoni. Nadhani ingewasaidia kuongeza mapato yao. Kama ilivyo ZANTEL Zanzibar.

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums

wazo zuri
 
serikali ipi unayozungumzia wewe?

hao mafisadi wa TTCL ndo hao hao wenye hisa vodacom, aitel tigo usitegemee ushindani hapo kwanza wanatamani TTCL ife kabisa ili waneemeke zaidi.

solution ni kuipiga chini CCM.
 
hivi mkonga wa taifa unafanya kazi kweli? manake tuliambiwa gharama za internet nk zitapungua kwa kiasi kikubwa
 
TCRA walisimamie kidete jambo hili kwani watumiaji wa simu za mkononi tumegutushwa sana kwa jinsi MB( mega bytes ) zilivyo punguzwa kwa kasi, toka 50 hadi kufikia 8! Wengi tumekuwa wahangwa pa kukimbilia ni TCRA pekee.
 
Takwimu nyiiingi... Ujumbe hafifu!
TCRA wanamshauri nani kuhusu matumizi ya smart phone na bundles?

Ishu ilikua kupanga bei kwa makampuni yote ya simu. Mitandao yote yalipunguza data to 8MBs, ingekua imepungua kwa kampuni moja wateja wangehamia kampuni ingine. Ila ishu ilikua kama kampuni zote zimekaa na kupanga bei, hii ndio TCRA walitakiwa kuishughulikia
 
naomba kuuliza..
internet inanunuliwa wapi mpaka kufika kwenye mitandao ya simu...kama inawezekana watu waanzishe makampuni ya kuuza MB..
Kwa kifupi hakuna sehemu moja ambayo inaweza ikasema kwamba inauza huduma ya internet. Internet ni muunganiko wa vifaa lukuki vya mawasiliano, muunganiko huo unatumia lugha yake ya ili vifaa hivyo viweze kuelewana na kifaa kimoja kukitimizia kifaa kingine mahitaji yake. Sehemu ambazo taarifa zinapatikana kifaa hiki huitwa Server na ili uweze kupata taarifa unazozitaka lazima uifikie server husika na ili uifikie inabidi upitie vifaa vingine vingi.

Kila kifaa kilicho katika muunganiko huo kimepewa namba maalumu ili kiweze kutambulika katika muunganiko huo, namba zingine ni static (yaani haibadiliki badiliki) na zingine ni dynamic (zinabadilika badilika)
 
Makampuni ya simu yamefanya hujuma ya wazi kabisa. Haiwezekani kampun zote zishushe ukubwa wa bundle tena kwa MB zinazofanana. Huu sio soko huria bali ni mipango ya kihujuma imefanyika.
 
TCRA walisimamie kidete jambo hili kwani watumiaji wa simu za mkononi tumegutushwa sana kwa jinsi MB( mega bytes ) zilivyo punguzwa kwa kasi, toka 50 hadi kufikia 8! Wengi tumekuwa wahangwa pa kukimbilia ni TCRA pekee.

Acheni kufuatawmkumbo amia airtel. Hii OMG pack weekly.
 
Attachments

  • 1424784534434.jpg
    1424784534434.jpg
    22 KB · Views: 452
Kwa kifupi hakuna sehemu moja ambayo inaweza ikasema kwamba inauza huduma ya internet. Internet ni muunganiko wa vifaa lukuki vya mawasiliano, muunganiko huo unatumia lugha yake ya ili vifaa hivyo viweze kuelewana na kifaa kimoja kukitimizia kifaa kingine mahitaji yake. Sehemu ambazo taarifa zinapatikana kifaa hiki huitwa Server na ili uweze kupata taarifa unazozitaka lazima uifikie server husika na ili uifikie inabidi upitie vifaa vingine vingi.

Kila kifaa kilicho katika muunganiko huo kimepewa namba maalumu ili kiweze kutambulika katika muunganiko huo, namba zingine ni static (yaani haibadiliki badiliki) na zingine ni dynamic (zinabadilika badilika)

kwahiyo hapo inamaanisha,haiwezekani mtu kuuza MB..manake hapo nnachoana kupata mb,sms na dakika kwa pamoja ndo gharama.Hivo wange weka ushindani kwenye soko la MB kivyake na kwenye sms na dakika kivyake...
 
serikali ipi unayozungumzia wewe?

hao mafisadi wa TTCL ndo hao hao wenye hisa vodacom, aitel tigo usitegemee ushindani hapo kwanza wanatamani TTCL ife kabisa ili waneemeke zaidi.

solution ni kuipiga chini CCM.

Solution sio chama fulani kuwa madarakani au laa! Hapo tatizo kubwa ni watu(viongozi) wa hivyo vyama kuchanganya uongozi/siasa na biashara! Hapo ndio tunasema conflicts of interest! Hapo haijalishi ni chama gani kinaendesha serikali ila watu wachache kwenye serikali wanaangalia maslahi yao binafsi.

Hiyo mitandao mingine hawewezi kuiombea TTCL ife, bila TTCL hakuna hiyo mitandao mingine, mfano Airtel na Voda wanatumia minara ya TTCL kwenye transmission zao, Tigo pia huko remonte area wanatembelea signal za hao jamaa!

Kwenye data(internet)ndio kabisaa mitandao yote wanategemea server za TTCL manake ndio wana artitecture na infrastructure nzuri za ku supply hizo data so wanategemeana!

Tatizo ni ufisadi wa watu wachache waliokuwa wanakula hizo pesa na kushindwa kuiendeleza TTCL ndipo MH.Zitto kuwalipua ndio fasta wakaja na huo mpango wakupunguza packages zao! Na data ndio ili-affectika zaid manake hiyo mitandao bado haina mifumo mizuri ya ku supply huduma ya bundles so walipewa data kwa real price tofauti na wizi wa bundle wa awali ndio maana wakazipunguza.

Ndio maana ukifuatilia utaona kwenye packages sms na dakika za muda wa maongezi kuna badiliko ndogo sana, ila MB's ndio kwenye utata!

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums
 
Takwimu nyiiingi... Ujumbe hafifu!
TCRA wanamshauri nani kuhusu matumizi ya smart phone na bundles?

Ishu ilikua kupanga bei kwa makampuni yote ya simu. Mitandao yote yalipunguza data to 8MBs, ingekua imepungua kwa kampuni moja wateja wangehamia kampuni ingine. Ila ishu ilikua kama kampuni zote zimekaa na kupanga bei, hii ndio TCRA walitakiwa kuishughulikia

Mkuu umeongea vema hapo.. Kwa mujibu wa sheria zinazotawala soko huria haitakiwi makampuni hasimu kukaa pamoja na kupanga bei ya bidhaa zao.. Hapa ndipo TCRA watupe ufafanuzi wa hatua zipi watayachukulia haya makampuni kwa kula njama na kupanga bei za pamoja..

Hayo mengine yote ni blah blah..
 
Back
Top Bottom