Vifaru chapa leopard vina kitu gani hasa special?

Nadhani ndio mana hata Israel akinunua ndege toka Marekani, anaweka vifaa vyake vilivyotengenezwa nchini mwake. (Customization)
Israel huwa haina imani na silaha zinazotumika na watu wengi hata F-35 imefanya upgrade zake inaitwa F-35 Adir. Hakuna nchi nyingine inaruhusiwa kufanya upgrade. Israel ilikataa kuipa Marekani keys za Iron Dome na Marekani ikaachana na programu ile iliyokuwa iilipe Israel $1 billion. Bila kutoa keys ule mfumo usingeweza kuwa coordinated na mifumo ya Marekani kutengeneza umbrella of air defence. Israel haitaki kutoa critical technology inaamini chances za kuwa compromised ni kubwa
 
Ukiwa mweupe kichwani unasingizia mwenzako mjuaji.

Kwenye vifaru tunalinganisha tank battle, sio vita nzima. Tank battle haina habari za nani anamiliki ndege nyingi na nani ana meli za kivita. Vifaru vimekutana bila support ya attack helicopters, ground attack jets wala melivita. Hapo ndio kipimo sahihi provided everything remain constant na tunalinganisha numbers between opponents, years of production, training na vitu vingine. Kwahiyo Waarabu ni matahahira walioenda kupambana na Israel wakijua ana supporters wenye nguvu, mbona USSR iliwapa support nao au unakubali yenyewe ni inferior?

Israel iliwapiga single handed hakuna mwanajeshi wa Marekani, UK wala Ufaransa alikanyaga frontline. Silaha Waarabu walinunua na wakakopa kama ambavyo Israel ilinunua na kukopa na kupewa. Hakuna kisingizio.

Walivyoenda kwenye tank battles Israel ilikuwa na Centurion za Uingereza na M48 Patton za Marekani, Waarabu walikuwa na T-55. M48 imeanza kutumika 1952, Centurion imeanza 1948, T-55 imeanza production mwaka 1954 na service jeshini USSR ikaanza 1955. Hivyo vifaru si unaona years of production zinakaribiana, sasa mikwara ya sijui nani ana uchumi inakusaidia nini, GDP ndio inafyatua cannon ya kifaru?

Tukiachana na Six Days war tuje Ukraine. Mwanzo wakati Russia inavamia kabla silaha yoyote ya West ya misada haijafika Russia ilifanya bombardment kwa 1st Tank Brigade. Hapo ni 24 February 2022, vifaru vya Urusi vikaingia ndani ya Ukraine. 1st Tank Brigade ya Ukraine ikajipanga kwenye Battle of Chernihiv na kukutana na 41st Combined Army ya Russia, hapo Russia inawa-outnumber many times. Ukraine ikiwa na T-64BM imefanya modification yenyewe kutoka Soviet T-64, kuna vifaru vilikuwa ordered na DRC vikazuiwa kwenda wakavitumia. Russia vifaru vyao unavijua, modified T-64s, T-72, T-90 na kipindi hicho T-90M the most latest Russian tank haijaletwa vitani. Warusi wakapigwa na hapo wana latest tanks.

Warusi walikuwa 60km from taking Kyiv, msingekuwa hapa mnalialia misaada ya West imesaidia Ukraine. Kabla ya misaada mlifeli wenyewe visingizio havina tija.

Na kuhusu Libya, hakukuwa na tank battles. No tank can survive air attack or artillery strike, hakuna haja ya kuitaja Libya wala Syria hapa.

hivi vitu ndio napendaga kuvisikia. [emoji991]
 
Mzuka wanajamvi.

Naomba mwenye ufahamu,

Hivi vifaru vya leopard vina sifa gani special tofauti na vifaru vingine? Uwezo wake wa kushambulia bila shaka utakua mkubwa, lakini uwezo wake wa kujikinga na mashambulizi upoje?

Je, uwezo wa kua sported kwenye uwanja wa vita na kua target ya kuviangamiza hauhofiwi?

Nimeona Serikali ya Kyiv inavipambania kuvipata na inauhakikishia ulimwengu kua itakomboa maeneo yote ilio pokonywa na russians. Nimeona hadi Poland inatishia kuvipeleka hata kama German watakataa kuidhinisha.

Najiuliza inauspecial gani hasa? Inabeba makombora gani?

Ninachokijua mimi ni kuwa. Vinatengenezwa German na uzalishaji wake ni kwaajili ya ujerumani na inaviuza kwa nchi maalumu tu. Na german haitaki visambae kwenye mataifa ambayo haijachagua kusambazwa huko.

Pia najua mataifa mengi wanavililia. Hicho tu ndicho nacho kijua. So mwenye maelezo ya ziada atujuze tupate elimu.

Sijaandika kishabiki.

Wasalaam.
Havina chochote special. Ila ipo hivi Russia na West wana tabia ya ku-exaggirate uwezo wa silaha zao. Kutokana na hilo kila mtu anaogopa kuwa wa kwanza kupeleka silaha/zana yake anayosema kuwa ni special mfano hii leopard tank au Abraham tank front line huko Ukraine

Hizi leopard zikipelekwa front line halafu mrusi akavipopoa itakuwa ni aibu kwa mjerumani na atakosa pa kuviuza maana madhaifu yake yatakuwa yamedhihirika.

Sasa USA naye ana vifaru vyake vinaitwa Abraham anavyosema ni vya kisasa sana. Lakini havijawahi kukutana na real army kama Russia; vimekutana na mujahedeen tu huko jangwani. Anaogopa naye kuvipeleka Ukrain front line.

Ndiyo maana Mjerumani kaweka condition atapeleka Leopard tanks endapo tu Abraham tanks nazo zitapelekwa ili kama kupopolewa wapopolewe wote. Isije ikawa yeye anapeleka Leopards zishindwe halafu marekani apete na kuendelea kuuza Abraham tanks kwa wateja wa waliokuwa leopards.

Ila cha muhimu tu uelewe hii vita ni sehemu ya kutest ubora wa silaha baina ya Russia vs West. Mambo ya kumsaidia Ukraine ni baadae
 
Israel huwa haina imani na silaha zinazotumika na watu wengi hata F-35 imefanya upgrade zake inaitwa F-35 Adir. Hakuna nchi nyingine inaruhusiwa kufanya upgrade. Israel ilikataa kuipa Marekani keys za Iron Dome na Marekani ikaachana na programu ile iliyokuwa iilipe Israel $1 billion. Bila kutoa keys ule mfumo usingeweza kuwa coordinated na mifumo ya Marekani kutengeneza umbrella of air defence. Israel haitaki kutoa critical technology inaamini chances za kuwa compromised ni kubwa
Sema kwa tech ya iron dome. Israel walicheza sana.

Saa nyingine bila kuwa na usiri katika tech zako especially kwa nchi iliyo na maadui kama israel ni risk sana
 
Pich
Mzuka wanajamvi.

Naomba mwenye ufahamu,

Hivi vifaru vya leopard vina sifa gani special tofauti na vifaru vingine? Uwezo wake wa kushambulia bila shaka utakua mkubwa, lakini uwezo wake wa kujikinga na mashambulizi upoje?

Je, uwezo wa kua sported kwenye uwanja wa vita na kua target ya kuviangamiza hauhofiwi?

Nimeona Serikali ya Kyiv inavipambania kuvipata na inauhakikishia ulimwengu kua itakomboa maeneo yote ilio pokonywa na russians. Nimeona hadi Poland inatishia kuvipeleka hata kama German watakataa kuidhinisha.

Najiuliza inauspecial gani hasa? Inabeba makombora gani?

Ninachokijua mimi ni kuwa. Vinatengenezwa German na uzalishaji wake ni kwaajili ya ujerumani na inaviuza kwa nchi maalumu tu. Na german haitaki visambae kwenye mataifa ambayo haijachagua kusambazwa huko.

Pia najua mataifa mengi wanavililia. Hicho tu ndicho nacho kijua. So mwenye maelezo ya ziada atujuze tupate elimu.

Sijaandika kishabiki.

Wasalaam.
Picha
 
Havina chochote special. Ila ipo hivi Russia na West wana tabia ya exaggirate uwezo wa silaha zao. Kutokana na hilo kila mtu anaogopa kuwa wa kwanza kupeleka silaha/zana yake anayosema kuwa ni special mfano hii leopard tank au Abraham tank front line huko Ukraine

Hizi leopard zikipelekwa front line halafu mrusi akavipopoa itakuwa ni aibu kwa mjerumani na atakosa pa kuviuza maana madhaifu yake yatakuwa yamedhihirika.

Sasa USA naye ana vifaru vyake vinaitwa Abraham anavyosema ni vya kisasa sana. Lakini havijawahi kukutana na real army kama Russia; vimekutana na mujahedeen tu huko jangwani. Anaogopa naye kuvipeleka Ukrain front line.

Ndiyo maana Mjerumani kaweka condition atapeleka Leopard tanks endapo tu Abraham tanks nazo zitapelekwa ili kama kupopolewa wapopolewe wote. Isije ikawa yeye anapeleka Leopards zishindwe halafu marekani apete na kuendelea kuuza Abraham tanks kwa wateja wa waliokuwa leopards.

Ila cha muhimu tu uelewe hii vita ni sehemu ya kutest ubora wa silaha baina ya Russia vs West. Mambo ya kumsaidia Ukraine ni baadae
Ila Leopard si zisha teketezwa kule Syria?
 
Sema kwa tech ya iron dome. Israel walicheza sana.

Saa nyingine bila kuwa na usiri katika tech zako especially kwa nchi iliyo na maadui kama israel ni risk sana

Lakini hizo Iron Dome bado zilipopolewa na Hezbollah. Kama wachangiaji walivyosema, hakuna real battle ambayo silaha zitakosa kupopolewa kama ambavyo hakuna vita itakosa madhara kwa kila upande haijalishi una nguvu kiasi gani
 
Ila Leopard si zisha teketezwa kule Syria?
Leopard tanks zimekuwa Syria na jeshi la Turkey, pia zimewahi kuwa kwenye action Iraq, Kosovo na Afghanistan tu. Lakini kote huko walikuwa wanapambana na majeshi dhaifu (mostly ni mujahedeen/rebels) yasiyo na ant tank misile yenye uwezo wa kufanya damage kwa morden tanks kama leopards au Abraham. Russia wanazo misile za kuzipopoa hizi tanks kama leopards. (Hata West wana system ya kuharibu vifaru vya Russia. Ndiyo maana ule mrafara wa 60km wa vifaru vya Russia mwaka jana vilipopolewa karibu vyote).

Ni kama vile mfumo wa kujilinda na makombora wa Israel wa Iron Dome unavyotungua makombora ya Wapalestina yanayotengezwa kienyeji uwani na kwenye gereji. Huo mfumo ukiwambia Israel waupeleke Ukraine watakataa maana wanajua kule watakutana na makombora haswa na siyo toys zilizotengenezwa uwani au garage

NB. Kule Syria madhaifu ya Leopards hayakuonekana sana. Subiria zipelekwe Ukraine halafu Russia aziharibu na labda acopy some hidden technology yake ndipo utaona majigambo ya Russia na kebehi zake dhidi ya hivyo vifaru
 
Kwa nini Ujerumani anasita kupeleka leopard 2 Ukraine

1.Anaogopa kukiuka mikataba aliyo isaini ya vita vya pili ya dunia ya kutojihusisha direct na vita ambavyo inakua na viashiria vya kutokea kwa vita 3 ya dunia.

Ikumbukwe kua Ujerumani katika vita ya 2 ya dunia chini ya Hitler ilitengeneza leopard 2 nyingi sana na kuzisambaza kwa washirika wake ili aweze kushinda vita.Hii ilipelekea Ujerumani kuzalisha kwa wingi leopard 2 na vifaru hivi vilisambaa sana kwa washirika wake wa nchi za ulaya.

Kama Ujerumani itabariki usambazaji wa leopard 2 Ukraine basi itakua imevunja mkataba iliousaini na rasmi Ujerumani itakua imejingiza direct kwenye vita.

2.Utegemezi mkubwa wa nishati wa Ujerumani kwa Russia

Kipindi NATO inaweka vikwazo kwa Russia kutokana na uvamizi wake kule Ukraine, Ujerumani ni moja ya nchi ambayo ilikua inasita kuiwekea vikwazo Russia kutokana na kuwa walikua hawana mbadala wa haraka ili kuweza kuacha na na nishati ya Russia. Marekani kama key member wa NATO bado hana uwezo wa kuziba pengo kama Russia akijitoa katika kusambaza nishaji ujerumani

Kama Russia akijitoa katika kusambaza nishaji kwa Ujerumani hii inaweza kupelekea athari kubwa kiuchumi kama kupanda kwa gharama za maisha kama inavyoshuhudiwa kwa baadhi ya nchi za ulaya (france, Netherlands na Spain) watu wanaandaman kutokana na gharama za maisha kupanda.

Kusita sita kwa Ujerumani kupeleka leopard 2 Ukraine ni ili kumfanya Russia asije akasitisha kupeleka nishati Ujerumani au kupandisha bei ya hiyo nishati kwani ni muhimu sana kwa uchumi wa Ujerumani.

Note. Ujerumani kwa sasa amelegeza vikwazo zidi ya Russia ili iweze kupata nishati kutoka Russia

Kwa nini NATO wanapendekeza matumizi ya leopard 2 Ukraine

1. Leopard 2 ni vifaru vinavyopatikana kwa wingi katika nchi na ulaya. Kwenye vita ya 2 ya dunia Ujerumani alitengeneza kwa wingi leopard 2 na kuzisambaza kwa washirika wake.kutokana na kupatikana kwa wingi basi itakua ni msaada sahihi na wa haraka kwa Ukraine.

2. Leopard ni vifaru vinavyotumia tekinologia ya kisasa katika kushambulia na kujilinda. Leopard 2 ina speed ya 70km per hour. Hii ni speed nzuri sana kwa kifaru kuweza kumshambulia adui. Hili litasaidia Ukraine kuweza kurudisha vikosi vya Russia nyuma na kuweza kukombo miji yao iliyotekwa. Ikumbukwe kua ni vifaru vichache sana vyenye speed ya leopard 2.

Leopard 2 pia inatumia mafuta kidogo ukilinganisha na vifaru vya marekani vya Abram hii inakua na unafuu wa gharama za uendeshaji hasa kwa serikali ya Ukraine ambayo teyari ipo katika changamoto kubwa ya kiuchumi.

NOTE. Upelekaji kwa wingi wa leopard 2 Ukraine pamoja na silaha nyingine za kisasa itakua inachochea kutokea kwa vita ya 3 ya dunia kwa kua Russia na yeye atachukua hatua kubwa zaidi maana silaha hizo zinaweza kumika kushambua ndani ya Russia hususani Kremlin.

NAWASILISHA.
 
Hakuna kitu pale make vilipelekwa Syria na viliharibiwa vibaya sana, Wazungu utawaweza? na hofu ya Ujerumani ni kwamba endapo vitaharibiwa na Urusi basi watakosa soko kabisa.
Hivi bajeti za dola million 600 na zaidi zinashindwa kuamua na kupeleka machuma Ukrain? Kuna maana gani ya kuwa na bajeti kubwa hadi chuma linapigiwa kura? Na leopard hataki kua chambo na M1 Abrams naye hataki kua chambo pia.
Kama mim ndio Zelensky nainua miguu juu, siyo mikono peke yake
 
Pamoja na sifa zote, yaani one gets an impression kana kwamba labda zimenukiliwa kutoka kwenye make believe movie script za Hollywood script writer - utani tu huo mkuu.

For a starter: mbona tuliona hizo tankers za Kijerumani mnazo zisifia hapa zilikuwa zinatiwa kiberiti na Russian no nonsense Kornet ATGM huko Syria - vifaru hivyo Wajerumani waliwauzia Waturuki - waturuki wakafanya makosa ya kutaka kutumia vifaru hivyo vya Kijerumani kuivamia Syria - sijui kama hata kifaru kimoja kilifanikiwa kurudi Uturuki, vilitiwa viberiti, Waturuki hawajarudia tena makosa hayo.

Sasa hawa viongozi wa Poland wanao kuwa driven na chuki zao za asili dhidi ya Taifa la Urusi ndio wanajitia kulazimisha mambo wanafikiri wakipeleka vifaru vya Kijerumani huko Ukraine vitafanya miujiza gani??

Zelensky akubali kushindwa tu ili yaishe - hasikubali taifa lake na raia wake watumike kijinga na mataifa ya magharibi wakiwa na lengo la kutaka kuikomoa Russia - mbinu za magharibi zimekwisha gonga mwamba unless wako tayari kuanzisha WW3 na wanajua vizuri hawawezi kushinda vita hii come rain or shine.
kwa watu wanaojua technology lazima utakubali kuwa wajeruman ni miongoni mwa engineer bora ktk dunia hatuna mashaka na uwezo wa hizo tank lkn kwa nn kumekuwa na ukakasi wa kutoa huo msaada.Ikumbukwe ya kwamba ni ujeruman pekee ndio anajua kwa nn Russia ni hatar na wanaelewa combat force ya Russia ukirejerea ktk historia Germany wako vizur kwenye battle field lakn ktk WW2 ni Russia pekee ndio walioweza kuwazuia Germany.ukisema sababu ya soko yaan market ya hizo tank hapan koz wanaziuza kwa kuchagua mnunuzi, ukisema technology tayari tank hiz zishauzwa kuna kitu nyuma ya pazia ni kipi?
 
Kwa nini Ujerumani anasita kupeleka leopard 2 Ukraine

1.Anaogopa kukiuka mikataba aliyo isaini ya vita vya pili ya dunia ya kutojihusisha direct na vita ambavyo inakua na viashiria vya kutokea kwa vita 3 ya dunia.

Ikumbukwe kua Ujerumani katika vita ya 2 ya dunia chini ya Hitler ilitengeneza leopard 2 nyingi sana na kuzisambaza kwa washirika wake ili aweze kushinda vita.Hii ilipelekea Ujerumani kuzalisha kwa wingi leopard 2 na vifaru hivi vilisambaa sana kwa washirika wake wa nchi za ulaya.

Kama Ujerumani itabariki usambazaji wa leopard 2 Ukraine basi itakua imevunja mkataba iliousaini na rasmi Ujerumani itakua imejingiza direct kwenye vita.

2.Utegemezi mkubwa wa nishati wa Ujerumani kwa Russia

Kipindi NATO inaweka vikwazo kwa Russia kutokana na uvamizi wake kule Ukraine, Ujerumani ni moja ya nchi ambayo ilikua inasita kuiwekea vikwazo Russia kutokana na kuwa walikua hawana mbadala wa haraka ili kuweza kuacha na na nishati ya Russia. Marekani kama key member wa NATO bado hana uwezo wa kuziba pengo kama Russia akijitoa katika kusambaza nishaji ujerumani

Kama Russia akijitoa katika kusambaza nishaji kwa Ujerumani hii inaweza kupelekea athari kubwa kiuchumi kama kupanda kwa gharama za maisha kama inavyoshuhudiwa kwa baadhi ya nchi za ulaya (france, Netherlands na Spain) watu wanaandaman kutokana na gharama za maisha kupanda.

Kusita sita kwa Ujerumani kupeleka leopard 2 Ukraine ni ili kumfanya Russia asije akasitisha kupeleka nishati Ujerumani au kupandisha bei ya hiyo nishati kwani ni muhimu sana kwa uchumi wa Ujerumani.

Note. Ujerumani kwa sasa amelegeza vikwazo zidi ya Russia ili iweze kupata nishati kutoka Russia

Kwa nini NATO wanapendekeza matumizi ya leopard 2 Ukraine

1. Leopard 2 ni vifaru vinavyopatikana kwa wingi katika nchi na ulaya. Kwenye vita ya 2 ya dunia Ujerumani alitengeneza kwa wingi leopard 2 na kuzisambaza kwa washirika wake.kutokana na kupatikana kwa wingi basi itakua ni msaada sahihi na wa haraka kwa Ukraine.

2. Leopard ni vifaru vinavyotumia tekinologia ya kisasa katika kushambulia na kujilinda. Leopard 2 ina speed ya 70km per hour. Hii ni speed nzuri sana kwa kifaru kuweza kumshambulia adui. Hili litasaidia Ukraine kuweza kurudisha vikosi vya Russia nyuma na kuweza kukombo miji yao iliyotekwa. Ikumbukwe kua ni vifaru vichache sana vyenye speed ya leopard 2.

Leopard 2 pia inatumia mafuta kidogo ukilinganisha na vifaru vya marekani vya Abram hii inakua na unafuu wa gharama za uendeshaji hasa kwa serikali ya Ukraine ambayo teyari ipo katika changamoto kubwa ya kiuchumi.

NOTE. Upelekaji kwa wingi wa leopard 2 Ukraine pamoja na silaha nyingine za kisasa itakua inachochea kutokea kwa vita ya 3 ya dunia kwa kua Russia na yeye atachukua hatua kubwa zaidi maana silaha hizo zinaweza kumika kushambua ndani ya Russia hususani Kremlin.

NAWASILISHA.

asant boss
 
kwa watu wanaojua technology lazima utakubali kuwa wajeruman ni miongoni mwa engineer bora ktk dunia hatuna mashaka na uwezo wa hizo tank lkn kwa nn kumekuwa na ukakasi wa kutoa huo msaada.Ikumbukwe ya kwamba ni ujeruman pekee ndio anajua kwa nn Russia ni hatar na wanaelewa combat force ya Russia ukirejerea ktk historia Germany wako vizur kwenye battle field lakn ktk WW2 ni Russia pekee ndio walioweza kuwazuia Germany.ukisema sababu ya soko yaan market ya hizo tank hapan koz wanaziuza kwa kuchagua mnunuzi, ukisema technology tayari tank hiz zishauzwa kuna kitu nyuma ya pazia ni kipi?

umetumia logic zaid naona.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom