Dah kweli ujuaji ukizidi unakuwa ujinga ivi unaweza kucompare vifaru vya Russia kwenye vita kama six day war na ile vita ya ukrein vita ambazo zilielemea upande mmoja vita ambazo mataifa makubwa kiuchumi, kivita na kisalaha yaliungana kuwachapa nchi zisizokuwa na mbinu kubwa za kivita ni kama Leo hii uanzee kusema Libya silaha zake siyo nzuri kuzidi za marekani au Ufaransa kweli kwa ugumu gani wa vita walioupata battle gani ngumu walikutana nayo kwenye vita izo challenge na Abraham na leopard ngoja ziendee ukrein maana pale ndyo uwanja wa vita sahihi siyo vita vya waarabu. Marekani hawezi kusahau vita ya Vietnam, au vita ya Korea maana baada ya vita ya pili ya dunia izo ndyo vita vilimtoa jashoo na askari na vifaa vingi viliaribika alafu vifaa vitani vifaa vinatengenezwa ili kuaribika kwenye vita ngumu si rahisi kuzuia vifaa kuaribika au kulipuliwa huwezi kuzuia iloo ni mjinga pekee atakayedhani vifaa vitarudi vyote
Ukiwa mweupe kichwani unasingizia mwenzako mjuaji.
Kwenye vifaru tunalinganisha tank battle, sio vita nzima. Tank battle haina habari za nani anamiliki ndege nyingi na nani ana meli za kivita. Vifaru vimekutana bila support ya attack helicopters, ground attack jets wala melivita. Hapo ndio kipimo sahihi provided everything remain constant na tunalinganisha numbers between opponents, years of production, training na vitu vingine. Kwahiyo Waarabu ni matahahira walioenda kupambana na Israel wakijua ana supporters wenye nguvu, mbona USSR iliwapa support nao au unakubali yenyewe ni inferior?
Israel iliwapiga single handed hakuna mwanajeshi wa Marekani, UK wala Ufaransa alikanyaga frontline. Silaha Waarabu walinunua na wakakopa kama ambavyo Israel ilinunua na kukopa na kupewa. Hakuna kisingizio.
Walivyoenda kwenye tank battles Israel ilikuwa na Centurion za Uingereza na M48 Patton za Marekani, Waarabu walikuwa na T-55. M48 imeanza kutumika 1952, Centurion imeanza 1948, T-55 imeanza production mwaka 1954 na service jeshini USSR ikaanza 1955. Hivyo vifaru si unaona years of production zinakaribiana, sasa mikwara ya sijui nani ana uchumi inakusaidia nini, GDP ndio inafyatua cannon ya kifaru?
Tukiachana na Six Days war tuje Ukraine. Mwanzo wakati Russia inavamia kabla silaha yoyote ya West ya misada haijafika Russia ilifanya bombardment kwa 1st Tank Brigade. Hapo ni 24 February 2022, vifaru vya Urusi vikaingia ndani ya Ukraine. 1st Tank Brigade ya Ukraine ikajipanga kwenye Battle of Chernihiv na kukutana na 41st Combined Army ya Russia, hapo Russia inawa-outnumber many times. Ukraine ikiwa na T-64BM imefanya modification yenyewe kutoka Soviet T-64, kuna vifaru vilikuwa ordered na DRC vikazuiwa kwenda wakavitumia. Russia vifaru vyao unavijua, modified T-64s, T-72, T-90 na kipindi hicho T-90M the most latest Russian tank haijaletwa vitani. Warusi wakapigwa na hapo wana latest tanks.
Warusi walikuwa 60km from taking Kyiv, msingekuwa hapa mnalialia misaada ya West imesaidia Ukraine. Kabla ya misaada mlifeli wenyewe visingizio havina tija.
Na kuhusu Libya, hakukuwa na tank battles. No tank can survive air attack or artillery strike, hakuna haja ya kuitaja Libya wala Syria hapa.