Vifaranga Vya Kuchi...

Ni aina ya kuku ambao ukiweza kuwakuza na kuwatunza vizuri wanadeal mjini si wa kisasa ila ni wakienyeji.
Mi nawapenda ukiwa nao kuku wa jirani hawakusumbui kupiga piga kuku wako, jogoo kuchi ndo anakuwa mwenye kijiji. Hapigwi, nq watetea hivyo hivyo, kazi kazi, wanatoa vichapo vya hatari kwa kuku wengine.
Sipendagi ujinga nimefungulia kuku wangu alafu anakuja jogoo wa jirani anampa kichapo jogoo wangu kisha anawapanda watetea wangu mbele ya jogoo wangu, dawa kuchi.

image.jpeg



image.jpeg
 
Mkuu nipo mkoa jirani hapa..vp unaweza changanya na kuku Wa kawaida? tukikubaliana naitaji jike na dume yan wawili tu
Ndio unaweza kuchanganya..lakini majogoo wa Kuchi ni wakorofi sana kukaa na majogoo ya kawaida ni tatizo
 
Haiwezekani kwa hiyo bei. Afadhali nikanunue mbuzi wawili nifuge kulliko hao kuchi
 
Hiyo bei ni kawaida sana kwa hao kuku haijalishi ni vifaranga maana hao wameshakuwa. Msibishe tu kwa minajili ya kubisha hao ni wenyewe kwa anaewajua na Mara zote sio kila mtu atanunua kuchi. Wazanzibari huwa wanauziwa paka Laki 3 na hawaliilii.
 
....Duuh kwa huku nilipo hiyo bei wapata mbuzi wawili saafiii

Haha kilashetani na mbuyu wake...

Mkuu.. Wewe naona ni mheni katika hii tasnia

Hao ni vifaranga tuu hujakutana na mkubwa wanauzwa hadi laki 2 na hao jamii ya kuku tu wanajulikana kama kuchi...
 
Duu! Nilikuwa sifahamu kabisa hawa kuku ila leo nimejifunza kitu kipya.

Nimeona watu wengi wamecomment maneno ya dhihaka nahisi kwa sababu ya kutokufahamu. Mleta mada umekosea jambo moja umetoa tangazo kama vile kila mtu anafahamu KUCHI , ungetakiwa utoe ufanunuzi KUCHI ni nini na wanasifa gani hapo ungepiga bingo.

Mimi nimeelewa wanatumika kubebea ngada, kubetia kwwnye mahoteli makubwa, soko lao lipo zaidi zanzibar, minofu mingi, wababe n.k
 
Hao kuku hawana uspecial wowote. Ilikuwa ni aina ya utapeli iliyovuma miaka ya tisini kwamba wanahitajika sana na wazungu na warabu.

Hivyo watu wakajikuta wanauziwa ifaranga kwa bei ya ajabu. Baada ya kuwakuza, soko likawa halipatikani. Wakajikuta nao wanaanza kuwatapeli watu kuwa wanawauzia kuku wa thamani ya juu.

Ki uhalisia hakuna soko hilo. Na kuku hao hawana thamani hiyo.

Ukifanikiwa kumpumbaza mtu unamnyoosha kwa bei hizo.

Mafia wapo wanauzwa elfu20. Tabora na geita ndio kuku wafugwao
 
Back
Top Bottom