Vifaranga vya broiler vimekuwa taabu sana kupatikana, nifanye nini?

Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,326
5,266
Wakuu salaam Sana,

Baada ya kuchoshwa na ajira nikaamua nirekebishe maBanda nianze kufuga Hawa kuku wa week nne (broilers) ila Sasa nimekuja kukwama baada ya kusaka vigaranga bila mafanikio na kuna makampuni ukiwapigia wanakuambia hawana vifaranga ila utasikia siku flani wameuza Sasa siajua wanatumia upendeleo gani?

Na baadhi ya wafugaji wanasema wananunua kwa bei ya juu tofauti na bei ya kampuni wanavyouza.

Kingine Cha kushangaza Bei nayo ya chakula imepanda sana, sasa najiuliza serekali inavyotuambia tujiajiri inakuwa na maana gani ? Kila siku wanaongeza tozo tu bila kuangalia athari.

1624957116630.png

Kama Kuna mtu anajua nawezaje kupata vifaranga kwa 1800 au 2000 anisaidie nisuru mtaji wangu maana gharama za maisha hazisubiri hata kidogo

Asante Sana
Mkuu habari yako, mkuu broiler wa 1800 kwa wakala sahau, sasa hivi ni 2000 mpaka 2300, hiyo 2000 unakaa foleni kwa wakala hata mwezi au miwili inategemeana na wakala wako, hiyo 2300 ndiyo fasta nenda kwa wakala aliye karibu nawe unayemuamini weka oda yako, ila jihadhari na matapeli mkuu wako wanaotumia mwanya huu kutupiga au kutupatia vifaranga vibovu.
Kila la kheri mkuu.
 
Nachoona Ni kuacha tu kufuga broiler ,niongezee ngombe wa maziwa maana , vifaranga ununue 2300 chakula wastani mfuko Ni 64,500 haya uje uuze 5500/5800
Tungekuwa na umoja tungepandisha Bei walau 6000 /6100

Najiuliza kwanini tulanguliwe na wakala kiasi hicho yaani yeye apate sh 500 kwa kila kifaranga ?? Kwa mtaji wa mteja ?

Maana pesa unampa cash anakataka zake zingene analipa kwa kampuni alafu anakuambia subiria siku ya kuchukua
 
Bora vitoke nje Kama zamani

Hapa dar Kuna kampuni tatu kubwa
Interchiki, animals care ubungo,na sliverland wanashirikiana na mkuza wote wamechemka
 
Me nafkilia kutengeneza chakula mwenyewe kwa ajili ya kuku wangu mwenyewe tu.
Mimi pia nina plan hii, ila ninakwama kwenye pellets mach, broiler wanakula pellets sasa ili kutengeneza chakula chao ni lazima uwe na hiyo machine.
 
Chakula chako mwenyewe sio lazima utengeneze pellets,kuna mama jirani yangu anatengeneza mwenyewe,na kuku wanakuwa fresh kabisa.
Kichwani mwangu na pia jinsi nilivyo aminishwa ni kuwa broiler ni lazima chakula chao kiwe katika mfumo ws pellets, kumbe hata mash inafaa?
 
Mimi pia nina plan hii, ila ninakwama kwenye pellets mach, broiler wanakula pellets sasa ili kutengeneza chakula chao ni lazima uwe na hiyo machine.
Hizo mashine sinzimeingia hapa tz hata miaka 6 haifiki mwanzo tulikuwa tunawalisha Cha Cha kawaida unakutana na dagaa humo humo na paraza ya mahindi haswa kwenye finishier kwa hiyo ukipita fomula unatengeneza tu mwenyewe ila Raha Yake uwe na kuku wengi au muungane.
 
Back
Top Bottom