Bei ya kuku yapanda mara dufu baada ya serikali kuzuia uigizaji kutoka nje

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Bei ya vifaranga vya kuku wa nyama mayai imepanda kutoka Tsh 1,300 hadi Tsh 2,200 baada ya Serikali kuzuia uagizaji kutoka nje


Kama unapenda kula nyama ya kuku au mayai, anza kujiandaa kukabiliana na upungufu ambao unaweza kukufanya ujipige mifuko zaidi kupata kitoweo hicho.

Kutokana na uamuzi wa Serikali kupiga marufuku uagizaji wa kuku wa nyama na mayai kutoka nje ya nchi, uhaba wa kitoweo hicho umeanza kutikisa.

Na huenda uhaba ukaongezeka zaidi miezi michache ijayo kama Serikali haitaghairi na kuruhusu vifaranga kutoka nje kuingia nchini, kwa mujibu wa uchunguzi wa The Citizen, gazeti dada la Mwananchi.

Gazeti hilo limebaini kuwa wazalishaji wa vifaranga wa kuku wa nyama na mayai wanahangaika kupata vifaranga, na kulazimika kununua kwa bei ya juu tofauti na awali.

Vifaransa, ambavyo vilikuwa vikiuzwa kwa Sh1,300 hadi siku za karibuni, sasa vinauzwa hadi Sh2,000 kwa kifaranga kimoja baada ya Serikali kupiga marufuku uagizaji vifaranga kutoka nje mwezi Juni.

Wizara ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi ilisema imechukua uamuzi huo kwa lengo la kulinda kampuni za hapa nchini zinazojihusisha na uzalishaji vifaranga pamoja na kutaka kujua mahitaji halisi na ugavi wa kitoweo hicho katika sekta hiyo ndogo nchini.

Wakati wafugaji na wafanyabiashara wakitaka kuondolewa kwa marufuku hiyo, Serikali inasisitiza kuwa uamuzi huo hautabadilika.

Lakini, wazalishaji vifaranga wa ndani wanasema wana uhakika kuwa upungufu huo wa vifaranga wa mayai na nyama utakuwa wa muda mfupi na kwamba ifikapo Januari mwakani watakuwa na uwezo wa kuhudumia soko la ndani kulingana na mahitaji.

Katibu mkuu wa wizara hiyo anayehusika na ufugaji, Dk Mary Mashingo alisema hivi karibuni kuwa hakuna uwezekano wa kuondoa marufuku hiyo kwa sababu uamuzi wa kuzuia uagizaji wa vifaranga nje umelenga kuokoa kampuni za ndani dhidi ya vifaranga wa bei rahisi wanaoagizwa kutoka nje.

“Tunahubiri maendeleo ya viwanda nchini, lakini wazalishaji vifaranga wa ndani wamekuwa wakilia kuwa soko si zuri kutokana na ushindani usio sawa dhidi ya vifaranga wanaoagizwa kutoka nje,” alisema.

Katibu huyo pia alisema Serikali inajua kuhusu upungufu uliopo wa vifaranga, lakini akasisitiza kuwa uwezekano wa kuondoa marufuku hiyo katika siku chache zijazo haupo hadi hapo wizara itakapojua ni kiasi gani cha vifaranga kinahitajika.

Kwa mujibu wa katibu huyo, kwa sasa wizara inafanya utafiti kujua idadi ya kampuni zinazojihusisha na uzalishaji vifaranga na uwezo wao kwa kuangalia mahitaji.

“Naibu Waziri (William Ole Nasha) amekutana na viongozi wa Chama cha Wazalishaji Vifaranga (TPBA) na kuunda timu ambayo inategemewa kutoa takwimu za sasa zinazoonyesha uwezo wa wazalishaji wa ndani na kuangalia suluhisho linaloweza kumaliza tatizo la upungufu wa vifaranga,” alisema.

Katibu mkuu wa TPBA, Thabit Batenga anaamini kuwa ni suala la miezi michache kabla ya wazalishaji wa ndani kuweza kutosheleza mahitaji.

“Wazalishaji wa ndani walikuwa wakiogopa kuzalisha kwa wingi kutokana na tishio la vifaranga kutoka nje ambao ni bei rahisi na ambao ndio waliojaa sokoni. Sasa kwa sababu soko limebaki kwetu, tuna uhakika kuwa hali itakuwa nzuri muda mfupi ujao,” alisema.

Aliongeza kuwa muda mfupi baada ya Serikali kupiga marufuku uagizaji vifaranga kutoka nje, wazalishaji wa ndani wameanzisha programu ya kuzalisha kuku kwa matarajio kuwa upungufu huo utakuwa historia ifikapo Januari mwakani.

Pia wameanza kukuza soko lao kwa sababu biashara sasa ina matumaini.

Akizungumza na The Citizen, Arson Taylor, mkurugenzi wa kampuni ya Interchick ambayo ni moja ya makampuni makubwa ya ndani katika biashara hiyo, alisema wameshaanza programu kubwa ya kupanua biashara hiyo kama walivyokubaliana na TPBA.

Kampuni hiyo imepata shamba la hekari 300 mkoani Arusha lenya uwezo wa kuzalisha vifaranga 3,000.

“Upungufu wa vifaranga sokoni unamaanisha kuna mwanga katika biashara, na sisi Interchick tumeshaanza kupanua eneo letu la biashara ili kuzalisha vifaranga wengi kuweza kuziba upungufu huo,” alisema.

Wakati Serikali na wazalishaji wa ndani wakionyesha matumaini, wafanyabiashara na wateja wanapata machungu.

Bei ya kilo moja ya nyama ya kuku imepanda kutoka Sh4,00 hadi Sh6,500, kwa mujibu wa Zuberi Ligongo, muuza kuku wa Temeke jijini Dar es Salaam.

“Angali (anaonyesha banda la kuku); hili ni eneo la kukuzia vifaransa ambakoi wafugaji wengi, hasa wanawake hufugia. Lakini mabanda mengi ya vifaranga yako wazi pamoja na la kwangu,” alisema Angel Peter, mfugaji mwingine anayeishi Veterinary, Temeke. Wafugaji wengi wa eneo hilo wamefunga shughuli zao kwa muda wa angalau wiki mbili sasa, wakisubiri vifaranga wapya ambao ni vigumu kuwapata.

“Uwezo wangu wa kufuga kuku wa nyama pia umepungua kutoka vifaranga 3,000 hadi 2,200 kwa wiki tatu kutokana na upungufu huo sokoni na ambao umesababisha kupanda kwa gharama za ufugaji,” alisema.

Pia alisema kwamba mazingira ya biashara si mazuri kwake kuwekeza kwa sababu kila mara anashindwa kutosheleza mahitaji ya wateja wake.

Kwa upande mwingine, hali ya biashara ya vifaranga wa nyama si nzuri hata kwa kampuni ya Interchik Ltd ambayo ina uwezo wa kuzalisha vifaranga hadi 200,000 ndani ya wiki mbili huku ikiagiza mayai 150,000 kwa ajili ya kutotoa katika kipindi kama hicho, alisema ofisa mauzo, Adela Wilson.

“Uwezo wetu wa kutoto ni mdogo kuilingana na mahitaji ya sasa ya kuku wa nyama. Hata kuagiza mayai 150,000 kutoka Malawi na Kenya hakutoshi kutosheleza mahitaji ya soko,” alisema.

Alisema mahitaji ni vifaranga 400,000 katioka muda wa wiki mbili, lakini uwezo ni vifaranga 200,000.


Chanzo: Mwananchi














Mwananchi
 
walaji ndio watakaoteseka, hili zuio ni la kukurupuka, ikizingatiwa uzalishaji wa hivyo vifaranga kwa hapa nchini bado ni wa kiwango cha chini. wahitaji wa vifaranga ni wengi kuliko uwezo wa watotoleshaji wa vifaranga.
 
Nafikiri hapa serikali inapaswa kupongeza. Soko la kuku Na mayai lilikuwa linaathiriwa sana na mafuriko ya bidhaa hizo kutoka nje huku, wafugaji wa ndani wakikabiliana na gharama kubwa ya kuhudumia mifugo yao.
Bei kwenda juu ni neema Kwa upande mmoja lakini ni fursa ya kuwekeza zaidi ktk sekta hiyo.
Hata bei hiyo, iliyoongezeka bado haijafikia bei ya samaki lakini mfugaji anaingia gharama kubwa huku soko liko chini.
Kwa hatua hii, wafugaji waliokuwa wameacha Kwa kuanguka Kwa bei ya mayai na kuku huku gharama ya uzalishaji ikiwa kubwa, bila Shaka watarejea
 
Hapa ndo pale watu wanachanganyikiwa kila mtu atawaza kufunga kuku wisho wa siku kuku mtaan wa mejaa soko limepungua tunaanza kulialia mtaja umepotea. Ukiona wengi wanafunga kuku angalia frusa hapo kuku lazima wale nenda huko kusikojulikana katafute chakula cha kuku
 
Kauli za kutumia vya ndani tulizoea kuziona katika maandishi sasa ni kwa vitendo, safi sana serikali nchi yetu asilimia kubwa ya wananchi ni wakulima na wafugaji. Ni wakati sasa wa jasho la watanzania liwe na neema katika nchi yao. Mali itapatikana shambani na utajiri alioubariki Mungu enzi na enzi upo katika mazao na mifugo. Tuache kulialia tutumie fursa hiii
 
mi silagi kuku wa kizungu.labda niwe sina namna.

bunge la tanzania ni "rubber stamp" ya serikali ya magufuli
 
Kw
Hii ni fursa, hata unapopeleka kitambaa kwa fundi ili nguo iweze kutengenezwa ni lazima ikatwe kwanza. Tukubaliane na kipindi cha mpito ili baadae tuneemeke. Tusiwe watu wa kulalamika tuu kwa kila jambo.
Kwa hiyo ushaona mtu anapeleka nguo kwa fundi alafu atembee uchi au anavaa nyingine kwanza?
 
Kw
Kwa hiyo ushaona mtu anapeleka nguo kwa fundi alafu atembee uchi au anavaa nyingine kwanza?
Unakuwa unayo nyingine of which tayari wazalishaji wa vifaranga wapo nchini, its just a mater of time waendane na soko husika.
Muwe na subra watanzinia jamani, kila jambo lina mwanzo na mwanzo huwa mgumu.
 
Mie naipongeza serikali kwa hili kwa asilimia 100% uhaba huo utakuwa wa muda kwa sababu wawekezaji wa ndani watajenga tu mashamba ya kuku. Uagizaji ndio uliokuwa unasababisha kutoanzishwa mashamba haya. Sera hii ikifuatwa kwa budhaa zote tz ya viwanda itafanikiwa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom