Vifaa vya kuunganisha umeme (mfano. Nguzo) vinavyonunuliwa na mteja ni mali ya TANESCO au Mteja?

LUS0MYA

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
862
1,097
Hivi karibuni shirika la umeme nchini na kwa tamko la serikali limerudisha viwango vya kuunganisha umeme vya zamani na kuondoa kile kiwango cha 27 000/= kwa kigezo kuwa kiwango hakiakisi gharama halisi.

Maswali kwa Tanesco na Waziri Makamba,

1. Vifaa vinavyonunuliwa kwa fedha ya mteja ni mali ya mteja au Tanesco? Jibu ni mali ya Tanesco ndiyo ukishalipia nguzo huna ruhusa ya kuitoa au kuzuia mteja mwingine kuitumia. Hivyo basi mita, waya, nguzo nk ni asset za Tanesco na zinaonekana katika mizania ya tanesco ingawa kimsingi mtaji ni wa mteja!! Kifupi Tanesco inachukua mtaji kutoka kwa mteja kinyemela.

TANESCO inatakiwa kurudisha gharama ya awali ya 27,000/= na serikali iwajibike kuipa mtaji maana ni mali yake kwa 100%.

Kama serikali haina mtaji basi haya malipo anayofanya mteja kwa gharama mpya arudishiwe hata kama kwa njia za units za umeme.
 
Una hoja ya msingi bwashee. Ni wizi wa wazi wazi wateja kununua nguzo halafu tanesco wanazichukua bure bila kulipa fidia. Hili suala linapaswa kupelekwa mahakamani ili likaamuliwe kisheria. Ukichukua mali ya mtu bila kulipa fidia huo ni uzulumati na wizi.
 
Una hoja hapa

Mawakili wetu wamelala.Waiburuze Tanesco mahakamani
 
Wanasema mteja haulipii nguzo Wala mita ila unalipa huduma ya kuunganishiwa umeme kutokana na umbali wa nguzo ilipo mpaka kwenye nyumba yako. Kwa hiyo umbali ndo unatengeneza gharama .
 
Hii Ni kuopeleka mahakamani kupata ufafanuzi wa haki juu ya huu utaratibu wa wizi wa Tanesco. Hii ipingwe mahakamani
 
Kwenda mahakamani ni bora ulipe ili upate huduma kwani CCM inaagiza hadi mahakama icheleweshe shauri linalowaumbua.
 
Hakuna kitu kibaya kama nchi kuingilia maamuzi ya mahakama. Hapo ndo haki inakuwa imesiginwa. Kinachoendelea kwenye mahakma zetu kwa sasa kinatugharimu sana. Majaji wmejikabidhi wenyewe serikalini na wamejisahau kuwa mahakama ni muhimili unaojitegemea. KATIBA MPYA NI MUHIMU
 
Katiba mpya itasimamiwa na chama dume.Mungu atusaidie jeshi lishike nchi kwa mda ili ipatikane katiba bora na siyo bora katiba.
 
Hivi karibuni shirika la umeme nchini na kwa tamko la serikali limerudisha viwango vya kuunganisha umeme vya zamani na kuondoa kile kiwango cha 27 000/= kwa kigezo kuwa kiwango hakiakisi gharama halisi.

Maswali kwa Tanesco na Waziri Makamba,

1. Vifaa vinavyonunuliwa kwa fedha ya mteja ni mali ya mteja au Tanesco? Jibu ni mali ya Tanesco ndiyo ukishalipia nguzo huna ruhusa ya kuitoa au kuzuia mteja mwingine kuitumia. Hivyo basi mita, waya, nguzo nk ni asset za Tanesco na zinaonekana katika mizania ya tanesco ingawa kimsingi mtaji ni wa mteja!! Kifupi Tanesco inachukua mtaji kutoka kwa mteja kinyemela.

TANESCO inatakiwa kurudisha gharama ya awali ya 27,000/= na serikali iwajibike kuipa mtaji maana ni mali yake kwa 100%.

Kama serikali haina mtaji basi haya malipo anayofanya mteja kwa gharama mpya arudishiwe hata kama kwa njia za units za umeme.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili jambo lina mambo mengi sana, kabla hujalipa umeme Kuna form unatakiwa kujaza ya vigezo na mashart, wengi huwa hawazingatii hili jambo, unapolipia huduma za kuunganishiwa umeme haimaanishi kuwa vile vifaa vinavyofungwa kwako na TANESCO ni mali yako!! NI MALI YA TANESCO ndo maana vinakuwa na NEMBO ya TANESCO na vinakuwa vimefungwa nakiri (Sealed) hasa mita zinasoma matumizi yako.

Pili kumbuka hata wewe unapolipia nguzo utatumia kuunganishiwa umeme wako kupitia nguzo ambazo zilishalipiwa na watu wengine! Ingewezekana kuwa umezitoa moja kwa moja toka umeme ulikoanzia yaani SUB STATION mpaka kwako hapo huenda ungekuwa na hoja!

Tatu nguzo, waya na mita zinabaki kuwa mali ya TANESCO kwakuwa hata zikipata shida kuungua au kuharibika ni jukumu lao kukupatia mpya na hulipii tena.

TANESCO wana mamlaka ya kukuondolea huduma zao wakati wowote ule kama utakuwa umekiuka taratibu zao kama kuiba umeme au kugawa umeme kwa jirani nk.. ndo maana miundomibinu inabaki kwa chini yao yaani ni mali ya umma.

Nimejibu kwa uzoefu wangu tu kama mteja wao kama kuna mahali nimekosea basi sio kwa nia mbaya.
 
Hiyo nguzo ikioza ni wewe unaibadilisha?
Inaoza baada ya miaka mingapi? Hata ikiwa hivyo, issue on the table Ni kuwa is it just/fair for a customer to buy posts which then becomes Tanesco property, so as to be provided with power service line
 
Back
Top Bottom