Vifaa vipi vya ujenzi vimeshuka bei? ahadi ya CCM

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,945
3,237
Katika Ahadi za Rais Wetu mpendwa JPM, ahadi zipi zimetekelezwa..

Ahadi ambayo ilipewa msukumo mkubwa kuwa ingetekelezwa ni punguzo la Vifaa vya ujenzi

Mikoa ya Morogoro, Dodoma na Shinyanga ni Ngome za CCM, ila ndo mikoa inayoongoza kwa nyumba za Tope (Tembe). Sasa asante kwa hawa wapiga kura ni nini?

Wakati Dangote Anakuja na wakati gesi inatolewa Mtwara....CCM walisema kwa sauti kubwa kuwa Cementi itakuwa 8000 Tshs kwa mfuko...

Sasa mbona hii ahadi imepotea? Au Hapa Kodi tu?

Raw material (Mali ghafi) kubwa inapatikana Hapa Tanzania......Nini sababu cementi inakuwa Ghali? Serikali inatoza kodi kubwa au Umeme ghali

Watanzania wanalipa Kodi PAYE, VAT on everything you buy, Na sasa VAT on Banking and Mobile Money

HAPA KODI TU....

Serikali itengeneze ajira mpya kwa vijana..

Nguvu kazi ya Taifa inapotea chini........

Ajira mpya zitaongeza kodi kwenye serikali na uchumi wa nchi utakuwa

Ni Hayo tu.....
 
Ngoja tuone mwisho wake mkuu.Muda utazungumza.Tuishi tu 'kwa matumaini' maana mpangaji wa sasa wa Magogoni ana miezi saba tu.Na tunalazimika kuishi kwa matumaini kwa sababu ya wengi wetu Tz ambao maono yao ni kama mwanga wa tochi kwenye giza totoro.
 
huko kwenye ngome ya ccm ambako kuna nyumba za tembe waachwe tu waisome namba maana wameipenda wenyewe.
 
Nipe mfano wa ahadi ambazo Ccm imewahi kutoa kwa Watanzania wakati wa kampeni halafu zikatekelezwa. Nyie wapeni kura halafu piteni hivi elimu bure sasa mnaambiwa changieni madawati, dawa bure kwa wazee na watoto. Nenda uone kama utapewa dawa. Maisha bora je mliyapata, ?? Niwatumikia maskini, sasa hata chip yako ya simu unailipia kila mwezi. Nashangaa sana kuona mtu anaishabikia Ccm.
 
Hivi mnapata wapi ujasiri wa kuwaamini ccm , chama kilichoshindwa kwa miaka 60 kitaweza miezi 6 ?
 
Kampuni ambayo watanzania walidhani itauza saruji kwa bei ya kutupa/chini kabisa ni Dangote, lakini matumaini yametoweka baada ya kuona kampuni hiyo ikiuza mfuko mmoja wa saruji kwa bei ya sh. 12,000. CCM ni waongo kupindukia. Kamwe hawaaminiki.
 
Back
Top Bottom