Vietnam War katika kumbukumbu.

Vietnam War katika kumbukumbu.

Vietnam war katika kumbukumbu
Sehemu ya pili (2)

Huu ni mwendelezo wa makala hii fupi kuhusu historia ya vita vya Vietnam.
Kwanza kabisa napenda kuwaomba radhi ndugu wasomaji na wapenzi wote wa jukwaa letu pendwa pamoja na Wana JF wote maana wengi wenu mmeonesha kutopendezwa kabisa na utaratibu wa kuletewa habari fupi fupi na ahadi za miendelezo ya masimulizi.
Lakini kwa ufupi hii hutokana na mtindo wa maisha yetu na hatuwezi kukwepa jambo hili kutokana na ufinyu wa muda wa ziada wa ku-share mambo kwa pamoja hapa JF kuwa ni mdogo mno. (Tusamehane wakuu)

Katika sehemu hii ya pili ya masimulizi haya tutayaangazia masuala mbali mbali yaliyojitojeza katika vita vya Vietnam. Vita iliyobeba historia kubwa sana huku ikihusisha mataifa kadhaa tokea Asia, na Marekani ambapo nje ya Marekani kuonekana kama mshiriki mkuu katika vita hivyo lakini ndani yake kulikuwapo na mataifa mengine kama vile Laos, Cambodia, uchina na nchi nyingine za ulaya wakiwa washirika wakuu wa Marekani.
Twende pamoja. Mnamo mwezi January 1973, umoja wa mataifa ukishirikiana na Amerika ya kaskazini walihitimisha makubaliano ya mwisho ya amani na kukomesha vita vya wazi kati ya mataifa mawili.
Vita kati ya Vietnam ya kusini na Vietnam ya kaskazini (tunakumbuka Marekani ni kama aliununua ugomvi katika vita hivi, na kumuunga mkono aliekuwa mtawala wa Vietnam ya kusini na huu ni utaratibu wa Marekani kukuza mambo na vita kama ilivyokuwa kwa mataifa mengine kama vile Iraq,Syria,na kwingineko) na katika vita hivi vya Vietnam waliopaswa kuwa wenyeji wa vita ni wa-vietnam wenyewe, ila kwasababu ya Marekani kuitaji kupambana dhidi ya kuangamiza nguvu za usoviet, na itikadi za kikomunisti ndipo ikiingia vitani na kuiunga mkono Vietnam ya kusini dhidi ya iliyokuwa Jamuhuri ya Vietnam ya kaskazini iliyokuwa na makazi yake makuu huko Hanoi
5230609512_5c08640663_b.jpg
"Wanajeshi wa Marekani wakisaidia majerui wao katika uwanja wa vita"


Tukirudi nyumba kidogo tunaona ijapokuwa kulifanyika makubaliano ya kumalizia vita yaliofanywa mwaka 1973 lakini vita viliendelea mpaka mwezi April 30, 1975 huku majeshi ya (DRV) yalipoitwaa Saigon iliyokuwa ngome ya Vietnam ya kusini yenye kuungwa mkono na Marekani na washirika wake na kisha kuibadilisha jina na kutoka Saigon na kuita Ho Chi Minh city, jina la kiongozi wao ambaye wakati huo alikwisha kufa kutokana na maradhi ya kawaida tu na sio kuuwawa na Wamarekani.
220px-Ho_Chi_Minh_1946.jpg

Bwana Ho Chi Minh
Tunaendelea. Kumbuka pia makala hii imeandikwa kwa mtindo wa mbele nyumba, nyuma rudi mbele hivyo basi tuzingatie katika usomaji wetu.
Wakati vita baridi (cold war) vikiimarika duniani kote , Marekani ilijipanga vyema kukabiliana na washirika wowote wale watakao jitokeza na kuungana na umoja wa kisoviet na hapo ndipo aliekuwa Rais wa Marekani wakati huo bwana Dwingh Eisenhower aliahidi msaada wa hali na mali kwa bwana Dien na Vietnam ya kusini ili kupambana na kuuangusha utawala wa Vietnam ya kaskazini ya kina Ho Chi Minh.
Marekani kama ilivyo kawaida yake ilitoa mafunzo na vifaa vya vita kwa wapiganaji wa Vietnam ya kusini pamoja na kuongezewa maajenti wa CIA ili kutoa mafunzo na kuweka mikakati sawa.
Baada ya kupata msaada na nguvu ya kutosha, jeshi la Dien lilivamia huko Viet Minh, upande wa kaskazini na kuwakamata waviet Cong au unaweza kuwaita Vietnamese Communist ambapo waliwakamata mateka watu laki moja (100,000) kisha kuwatesa na kuwaua kikatili ikiwa ni pamoja na kuwanyonga.
Baada ya hapo kibao kiligeuka, pale ambapo ndani ya mwaka 1957 waviet-cong na wapinzani wengine wa Dien walipoungana na kuanzisha mashambuluzi dhidi ya viongozi wa serikali na hadi ilipifikia mwaka 1959 wa Viet Cong wameanza kuwa na jeshi kubwa sana, kama ulishawahi kufuatilia movie za kivietnam kama vile ile ya PLATOON, utakuwa unajua mziki wa waviet-cong huwa hawaishi wanakuja kama nyuki na kauli mbiu yao ni kusonga mbele tu pia katika movie ya FULL METAL JACKET ya mwaka 1987 kuna mziki mkubwa ndani yake, hivyo kutokana na vita hivi Wamarekani wametoa makumi ya ma movie kuhusu vita vya Vietnam, kaitafute movie nyingine iitwayo GOOD MORNING VIETNAM hii ni ya mwaka 1987 pia, kuna nyingine inaitwa AIR AMERICA ya 1990 na nyingine nyingi sana, wazee wa WAR BUS nadhani mtakuwa mnanielewa hapa.

Tukirudi katika mwendelezo wetu tunaona kuwa baada ya kuungana kwa wapinzani wa bwana Dien na mwaka 1960 huku muungano huo ukiwaleta pamoja waviet-cong wenye misimamo ya kikomunisti na wale wasio upande wowote, hao wote waliungana na kuwa kitu kimoja na hapo ndipo maneno ya muasisi wao mzee Ho chi Minh yalipotimia pale aliposema "wa-vietnam watafufuka, wataungana na kuwa mtu mmoja" note (hapa usije ukafananisha muungano huu na muungano wa vyema upinzani(ukawa) vya Tanzania, bali huu ulikuwa muungano wa vita na damu) dhidi ya Dien na Marekani.
Vita viliendelea zaidi na zaidi huku askari wa Marekani wakiongeza bidii katika mapigano bila kufumba macho, maana waviet-cong waliokuwa hawatabiriki hata kidogo.
16.png

"Askari wa Marekani ndani ya Vietnam"
Tujikumbushe kidogo jambo moja muhimu kabla hatujasonga mbele zaidi. Unajua baada ya kufa kwa kiongozi wa mwanzo kabisa wa Vietnam ya kaskazini, Bwana Ho Chi Minh, ambaye alifikwa na umauti kwa maradhi ya kawaida tu, lakini hiyo haikufanya mapambano yapoe ama kuisha bali vita viliendelea kupamba moto na hadi kufika idadi ya maraisi Watano (5) wa Marekani waliohudumu kipindi vita vikiendelea.
83621456456386TunnelRats.jpg
ambapo mwanzilishi akiwa ni Rais Dwight Eisenhower alieanza kuongoza Marekani tangu mwaka 1853 na mwaka 1955 akavipokea rasmi vita vya Vietnam hadi pale alipomaliza muhula wake mwaka 1961 na kukabidhiwa bwana John F Kennedy kuwa Rais. John Kennedy ambaye alijitahidi kuongeza nguvu zaidi katika vita huku akituma zaidi vikosi 400 vya special force na maajenti wengi zaidi wa CIA , lakini safari yake haikuwa ndefu sana baada ya kufanyiwa mauaji ya kutisha ndani ya nchi yake mwenyewe, ambapo alipigwa risasi huko Dallas akiwa katika gari la wazi
8bd2e3ea-70fd-443f-ac01-6ef5d6a49981_HTRA211_VV178_H-1900x1252_c.jpg
Pichani juu, ikionyesha gari la bwana Kennedy na mwili wake ukiwa chini kwenye seat ya nyuma.
jfk-assassination-weapon-gty-jt-171021_4x3_992.jpg

pichani juu ni bunduki iliyotumika katika kuutoa uhai wa Rais John F Kennedy.
Ndani ya mwaka 1963 baada ya Kennedy kufa aliingia madalakani bwana Lyndon .B. Johnson alipokea madalaka na kuendelea na vita hivyo hadi pale mwaka 1969 alipomwachia Rais Richard Nixon ambaye pia aliongoza kwa kipindi cha miaka mitano huku vita vikiendelea na kisha mwaka 1974 akamkabidhi madalaka Rais mpya Bwana Gerald Ford ambaye alimaliza muda wake mwaka 1977 ambapo Rais Ford alimaliza muda wake huku vita vikiwa vimeisha miaka miwili iliopita.
bong-son-south-vietnam-two-soldiers-of-the-u-s-first-cavalry-division-picture-id544040150.jpg
ambapo kwa ujumla vita hivyo vilichukua miaka 19 na miezi mitano (5) wiki nne (4) na siku moja (1).


Kwa kumalizia, maana bado mambo ni mengi sana kama vita yenyewe ilivyochukua muda mwingi kuisha.
Katika vita vya Vietnam Marekani na washirika wake walitumia ndege nyingi pamoja na maelfu ya helicopter, na siraha nyingine nyingi za kielectroniki.

bell-uh-1-906516_960_720.jpg


(katika sehemu ya tatu na ya mwisho, tutaona ni aina gani ya siraha zilizotumika katika vita, sehemu za kumbukumbu, siku ya maadhimisho na ni nani alieshinda vita)
Asanteni.
La Nuit.
 
View attachment 840808
Kutokana na rangi ya ngozi zao waweza fikilia ni moja wapo wa askari wetu wa JWTZ, lakini sivyo hivyo bali ni askari wa kimarekani wakiwa katika uwanja wa vita huko Vietnam.
Leo ikiwa ni siku nyingine tena, siku tulivu kabisa, napenda kuutambua uwepo wenu hapa JF maana nadhani tupo zaidi ya member 449,730 na zaidi hivi kama sikosei, pia tukiwa na wageni zaidi ya 5,054 hivi ijapokuwa idadi hubadilika badilika, nawashukuru sana kwa uwepo wenu Wakuu.
Leo ningependa nizungumzie kidogo kuhusu historia ya taifa la Vietnam na vita vilivyopiganwa na wa-vietnam na Wamarekani katika miaka ya 1955 na kuendelea kwa miaka kadhaa mbele.
Habari hii itakuwa na muendelezo kutokana na upana wake katika maelezo na mafafanuzi katika historia kuhusu Vietnam.
Wakati Vietnam ya kaskazini ikiingia ulingoni kupambana na Marekani, Marekani wakati huo ilishapigana vita dhaidi ya tisa, ambapo tunakumbuka Revolution war ambapo walikufa askari 4,435
war of 1813-waliokufa 2,260
Mexican war- 13,283
civil war -498,332
spanish American war- 2,446
World war (i)- 116,516
World war (ii)- 405,399
Korean war -54,246

Ndipo ikafuatia Vietnam war, na mission nyingine nyingi zilizofanywa na Wamarekani.


Vietnam likiwa ni taifa lililopo kusini mashariki mwa bara la Asia, wakati huo likiwa chini ya utawala wa kikoloni wa Kifalansa tangu karne ya 19.
Kwa wale wapenzi wa movie za kivietnam mnakumbuka jinsi hawa jamaa walivyokuwa noma sana katika medani ya mapambano vitani.
View attachment 840920Pichani juu ni"askari wa kivietnam wakiwa katika uwanja wa vita"
Tunakumbuka pia wakati vita vikuu vya Dunia (world war ii ) vikiwa vimepamba moto, vikosi vya japani vilitiananga Vietnam na kuivamia ili kupigana na utawala wa kikoloni wa Kifalansa, lakini kufuatia kwa kushindwa japani mwaka 1945 katika vita kuu ya pili, japani iliondoa vikosi vyake kutoka Vietnam na kuacha Mfalme aliyefundishwa na wafalansa waliokuwa watawala wa kikoloni dhidi ya wa-vietnam alieitwa Bai Dai. Unajua wakati ule kulikuwa na mapigano makali kati ya vikosi vya Marekani na wajapani, ambapo kuna makala nyingi, movie na documentaries kuhusu sehemu ya vita vikuu vya pili vya Dunia vilivyo ghalimu maisha ya watu wengi zaidi kuliko katika vita vikuu vya kwanza.
Hivyo kuifanya Japani kuonekana kama moja wapo ya taifa Sumbufu sana katika wakati huo.
Tukirudi kwa upande wa Vietnam, baada ya mfalme Bao kukabidhiwa nchi, kulitokea mgawanyiko ndani ya nchi ya Vietnam, baadhi ya viongozi wakiongozwa na bwana Ho, Ho Chi Minh, huyu jamaa kwa heshima yake jina lake limepewa mji mmoja wapo mkubwa wa Vietnam pale Ho Chi Minh city, mji mzuri kweli kweli kwa utalii na historia ya Vietnam.
Sasa baada ya mgawanyiko huo bwana Ho na wafuasi wake waliondoka mara moja huku wakichukua mji wa kaskazini mwa Vietnam, mji ulioitwa Hanoi na kisha kutangaza kuwa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Vietnam (DRV) na bwana Ho akiwa kama Rais.View attachment 840934"Huyu pichani ndie Ho Chi Minh mwenyewe,mtu ambaye watu wa Vietnam wanamkumbuka vyema kwa matendo yake na maneno mazito yenye sumu kali'
kuna baadhi ya misemo yake ambayo inakubalika sana kama vile

" Watu wa Vietnam kwa undani wanapenda uhuru, uhuru na amani. Lakini katika uso katili wa Marekani wamefufuka, wameungana kama mtu mmoja. Kumbuka dholuba ni fursa nzuri kwa pine (aina ya mti) na cypress (aina ya mti pia) kuonyesha nguvu zao na utulivu wao, ilikuwa ni patriotism, si ya kikomunisti ambayo imeniishia."
Bwana Ho aliamini sana katika falsafa za kikomunisti za uchina pamoja na Soviet ya wakati huo, ndio maana katika vita vya Vietnam tunaona baadhi ya askari wa kirusi wakisaidia upande mmoja wa Vietnam ya kaskazini. Pia Ho walianzisha Viet Minh au unaweza kuita ligi ya uhuru wa Vietnam.
Sasa wakati Vietnam ikigawanyika katika pande mbili yaani upande wa Mfalme Bao na upande wa kaskazini wa bwana Ho aliejitangazia Jamuhuri ya kidemokrasia ya Vietnam kwa upande wa kaskazini katika mji wa Hanoi, Hapo ndipo Ufalansa lililokuwa koloni la zamani kuamua kumuunga mkono Mfalme Bao ili kudhibiti tena mkoa huo wa Hanoi hivyo kuanzisha state ya Vietnam mnamo mwezi julai 1949 na mji mkuu ukawa Saigon.
Wakati huo pande zote mbili za wa-vietnam zilihitaji kitu kimoja, Vietnam yenye umoja na nguvu, lakini wakati huo huo bwana Ho Chi Minh na wafuasi wake wakiitaji taifa kusimamia katika misingi ya kikomunisti kama ilivyo kwa uchina na Soviet, huku Mfalme Bao na wafuasi wake wakiitaji Vietnam iendeleze uhusiano wa karibu wa kiuchumi na kitamaduni wa kimaghalibi yaani kule kwa watawala wao.
Hapo sasa ndipo msuguano ulipoanzia, baada ya Majeshi ya kikomunisti ya Bwana Ho kudhibiti eneo la kaskazini mwa Vietnam, migigoro na mapigano yalizuka baina ya Majeshi ya kaskazini ba kusini, vita hivyo viliendelea hadi mwezi Mei 1954 ambapo vilimalizika kwa kushindwa kwa vikosi vya mfalme Bao. Hivyo Kufanya mfalme Bao na mshirika wake mkubwa ufalansa kushindwa vita huko Indochina.
lakini licha ya kushindwa kwa Mfalme Bao, mkutano wa pamoja wa wa-vietnam uliweka mkataba uliosainiwa mnamo julai 1954 kati ya makubaliano ya Ho kudhibiti kaskazini na Bao kudhibiti kusini, pia mkataba huo ulitaka kufanyike uchaguzi wa kitaifa wa kuunganisha ambapo ungefanyika mwaka 1956.
Lakini kabla ya mwaka huo wa uchaguzi wa pamoja uliopangwa ufanyike mwaka 1956,mwaka 1955 mwanasiasa mkuu wa kupambana na kikomunisti bwana Ngoja Doing alimfukuza Mfalme Bao na yeye kuwa Rais wa serikali ya Jamuhuri ya Vietnam kusini (GVN) hivyo kukawa na Jamuhuri mbili kinzani.
Hapa sasa ndipo msingi wa vita vya Vietnam kupamba moto kwa miaka mingi baada ya ndugu zetu wale wa America First kuona fursa dhidi ya kuvunja umoja wa usoviet popote pale duniani utakapo jitokeza. Kama utakuwa ulipitia Thread yangu iliopita iliyobeba jina la Patrice Lumumba utakuwa umefahamu kidogo jinsi ya Marekani na washirika wake walivyojitahidi kudhibiti jitihada za Patrice katika kule kuomba kwake msaada kwa Soviet, maana wakati huo kulikuwa na sekeseke kubwa la cold war hivyo kuifanya Marekani kuwa macho na taifa lolote au mtu aliejaribu kuunganisha nguvu na usoviet, na katika jitihada zake kuna maeneo waliyoweza kuyaendesha vyema ila hapa kwa wa-vietnam waliipata joto ya jiweView attachment 840974"Bwana Ho Chi Minh akiwa na wafuasi wake"
( Itaendelea katika sehemu ya pili, pale ambapo vita rasmi vilipoanzia na kwa pamoja tutaingia hadi ndani kabisa ya uwanja wa vita) #La Nuit


"Si kazi rahisi"
#SEHEMU YA PILI INAPATIKANA KATIKA POST NAMBA 26:
Saaaafi tunasubiri episode 2
 
Back
Top Bottom