Vietnam wanaijua thamani ya korosho zetu, sisi tunasubiri serikali ifanye kitu fulani

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Kwa mujibu wa hotuba ya rais muda mfupi baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa, ni kwamba Vietnam ilikuja kuchukua zao la korosho kutoka kwetu, miaka mingi iliyopita. Leo hii wanajulikana ulimwengu kwa kilimo hicho cha korosho.

Nadhani tuna tatizo lililo ndani kabisa ya DNA zetu, tatizo la kudhani kuwa kuna mtu fulani kaumbwa ili aje kuyatatua matatizo yetu. Tunazielekeza lawama kwa serikali, lakini tatizo ni kubwa zaidi ya hizo lawama, nahisi limo ndani kabisa ya asili yetu. Tumefanana na mtoto ambaye wazazi wake wamemnunulia vitabu vyote kwa ajili ya masomo lakini anaviacha vikipigwa na vumbi halafu ghafla mtoto wa jirani anajenga tabia ya kuitembelea nyumba anayoishi. Akifika yeye hajihangaishi na michezo bali anakwenda moja kwa moja kwenye vitabu vya rafiki yake. Unapokuja mtihani yule mtoto ambaye wazazi wamemhangaikia kumnunulia vitabu asome, anafeli, halafu yule ambaye alikuwa anadoea vitabu kila anapomtembelea rafiki yake ndio anayefaulu, tena kwa kiwango cha juu kabisa.

Rais JPM hataki uvivu kabisa, lakini wenye kupenda lawama wameshaanza kuilaumu serikali eti ndiyo yenye kupaswa kuwatafutia fursa zote wananchi kwa asilimia mia moja!. Hao wavietnam wanaoendelea kufaidika na korosho ambazo walizipata kutoka kwetu wameumbwa na Mungu gani na sisi watanzania tumeumbwa na Mungu gani?.
 
Back
Top Bottom