Vidoe Clips za Matukio ya Arusha

Vidoe Clips za Matukio ya Arusha

Gurudumu

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2008
Posts
2,349
Reaction score
264
nimepata CD mbili kutoka source tofauti ambazo watu wamefanya compilation ya matukio ya Arusha kuanzia maandamano, mahakamani, na mazishi. inaonekana ni clips zilizochukuliwa kutumia vyombo mbali mbali lakini wote siyo wataalamu wa kufanya hiyo kazi. pia inaonekana ni matukio ambayo yamechukuliwa katika mazingira mbali mbali, yaani huku watu wakikimbia, wamesimama, labda wengine walikuwa majumbani au madukani au ofisini mwao, n.k

binafsi nimevulia kofia matumizi ya technolojia ya kisasa, yaan simu, digital camera, na vyombo vingine. Pia nimevulia kofia waliounganisha hivyo vipande kiasi kwamba hatuhitaji kuandika historia ya jambo fulani kwa kutegemea kilichoripotiwa na vyombo vya habari tu au vyombo vya dola.

kwa ujumla ni hali ya kutisha. lakini ni ishara kwamba serikali bado iko kwenye karne ya nyuma sana. karne ambayo ni serikali tu ndiyo iliyokuwa na mamlaka ya kuchukua kumbukumbu za tukio. kwamba tukio lisipochukuliwa na waandishi wa habari basi halikutokea. kwamba waandishi wa habari tu ndio wanaoweza kutoa habari. karne ambayo kwamba kauli ya serikali ilikuwa ya kweli daima!
 
Mkuu Gurudumu...If you dont mind Weka hapa huo mkanda mkuu, ili tuuone!
 
Tundika hapa Mungu atakulipa. Ila ukitaka kulipwa sema hapa hapa.
 
Mkuu tuwekee hapa basi tuzipakue na sisi.

fanya tu jitihada zako mkuu kutafuta kwa machalii na wadau (hasa wafanya kazi wa maofisi ya serikali). kuna vitu ambavyo nikibandika hapa naamini nitatafutwa kama yule jamaa aliyepost ile picha ya mkulu kwenye ze utamu.
 
Mkuu Gurudumu...If you dont mind Weka hapa huo mkanda mkuu, ili tuuone!

wewe PJ najua uko arusha, utapata tu. jaribu kufanya kama wakati ule ulipokuwa unatafuta DVD za porno..

nikudokeze tu kwamba tafuta kwa watu ambao ni official, kwani ndio wanaweza kutumia rasilimali za ofisi kufanya hiyo kazi, na wengi wao ndio waliokuwa na uwezo wa kurekodi
 
Mimi nina cd moja ya video na audio clip ya hotuba za siku ya mazishi. Jinsi ya kuziapload zimenishinda kwa kweli.
 
sasa si wa mbali ndo tumekosa uhondo huo??? gurudumu tafadhali tafuta namna nyingine ya kupost kiusalama ili tupate hiyo taarifa muhimu
 
Mimi nina cd moja ya video na audio clip ya hotuba za siku ya mazishi. Jinsi ya kuziapload zimenishinda kwa kweli.

Thanks: Wana jf wataalam waelekeze namna ya ku upload ili taarifa hiyo muhimu tuipate jamani
 
wewe PJ najua uko arusha, utapata tu. jaribu kufanya kama wakati ule ulipokuwa unatafuta DVD za porno..

nikudokeze tu kwamba tafuta kwa watu ambao ni official, kwani ndio wanaweza kutumia rasilimali za ofisi kufanya hiyo kazi, na wengi wao ndio waliokuwa na uwezo wa kurekodi
Du...mkuu, dvd za porno kwani zilikuwa na shida sasa?..wakati huo niko dar (nikiwa barubaru) tulikuwa tunaenda pale round-about ya msimbazi na uhuru(kama unaelekea Mnazi-1, ukizuga dakika 3 pale tayari masela washatokeza wanakuvuta uchochoro, unaonyeshwa za wabongo(Magomeni, Tandale brands etc), waasia, wakenya unajisevia mwenyewe..ha ha haaaa!..(thats History now)!
Anyway, weka hapa kwaajili ya wale wasio na njia ya kuziona, ok mazee?
 
sasa si wa mbali ndo tumekosa uhondo huo??? gurudumu tafadhali tafuta namna nyingine ya kupost kiusalama ili tupate hiyo taarifa muhimu

kwa kweli sijui namna ya kufanya kwani mimi siyo mtaalamu wa kukata na kupunguza size ya resolution. ni vigumu ku share elecronically.

lengo langu lilikuwa kuwatangazia wadau tu kwamba there is this creativeness and one can find a copy, ili mtu uweze kupima mwenyewe kama vyombo vya harabri, polisi, na chadema ni nani aliyetoa version ya ukweli ya haya matukio. hasa lile tukio la 5 January
 
wewe PJ najua uko arusha, utapata tu. jaribu kufanya kama wakati ule ulipokuwa unatafuta DVD za porno..

nikudokeze tu kwamba tafuta kwa watu ambao ni official, kwani ndio wanaweza kutumia rasilimali za ofisi kufanya hiyo kazi, na wengi wao ndio waliokuwa na uwezo wa kurekodi

apo red sijapenda.

PJ ni mtu wa hoja, kama ulivyo wewe Gurudumu.

unge-m-PM tu.
 
Du...mkuu, dvd za porno kwani zilikuwa na shida sasa?..wakati huo niko dar (nikiwa barubaru) tulikuwa tunaenda pale round-about ya msimbazi na uhuru(kama unaelekea Mnazi-1, ukizuga dakika 3 pale tayari masela washatokeza wanakuvuta uchochoro, unaonyeshwa za wabongo(Magomeni, Tandale brands etc), waasia, wakenya unajisevia mwenyewe..ha ha haaaa!..(thats History now)!
Anyway, weka hapa kwaajili ya wale wasio na njia ya kuziona, ok mazee?
Una backup copy unitumie.....plz....
apo red sijapenda.

PJ ni mtu wa hoja, kama ulivyo wewe Gurudumu.

unge-m-PM tu.
hell noooooooo.....
 
Nitumie kwenye email gurudumu nitatundika.....ivisible siku hizi kawa academyInvivisible
 
Nitumie kwenye email gurudumu nitatundika.....ivisible siku hizi kawa academyInvivisible

wewe yo yo? ni kubwa wewe huwezi ku-attach. jaribu kufikiri matukia ya siku nne kutoka source mbali mbali siyo mchezo. nadhani nakala zinasambaa tu kama ilivyonifikia mimi. cha msingi ni kuanza kuulizia, siyo hapa janvini, bali katika maeneo yako ya kazi na marafiki na jamaa.
 
Back
Top Bottom