VIDEO: Zimbabwe imemtuma Waziri wake kuja kujifunza mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART)

Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,164
5,762
Waziri wa tawala za serikali za mitaa Zimbabwe amekuja Tanzania akiongozana na waatalamu mbalimbali wa nchi hiyo kuangalia na kujifunza jinsi mradi wa Mabasi ya mwendokasi unavyofanya kazi.

Mradi huu haukuanzia Dar au Tanzania. Hakuna cha kujifunza. Anayetaka aulize World Bank, na kwa nchi kama Colombia, mradi ulianza zamani sana na uko fit kuliko hapa TZ
 
Akitoka Dar aende UDOM tena akacheki flyover iliyojengwa kuunganisha lecture rooms mbili pale kwenye coleji ya infomatikia. Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwetu
 
Kununua mikate tu wanashindwa, wanataka kujenga DART, Mugabe please, ionee huruma nchi yako.
 
Ndio maendeleo hayo.
Ndivyo watu wanavyotaka badala ya vurugu za matamko.
 
Kipya ni nini hapa, system kama hizi zipo Ulaya from time immemorial , leo eti wanakuja kujifunza hapa na ugoro wote tunaoufanya katika kuendesha mradi huo! Zimbabwe, nchi maiti bado kuoza tu, au imeshaoza bado kunuka tu!
 
Mshaurini aende Lagos. Huko mabasi yana AC muda wote, hayapishani muda mrefu na nauli ni ndogo maradufu ya za kwetu!
 
Habari kama hizi za eti kuna nchi inayokuja kujifunza kwetu TZ huwa naona kama ni zakutunga tu,YAANI KABISA KUNA NCHI ZINATUONA SISI TUNA VITU VYA KUJIFUNZIA KWA AJILI YA WENGINE ........ Kweli nimeamini, thamani ya kitu ulichonacho anaiona ASIEKUWA NACHO SIO WEWE ULIYENACHO.
 
Mradi huu haukuanzia Dar au Tanzania. Hakuna cha kujifunza. Anayetaka aulize World Bank, na kwa nchi kama Colombia, mradi ulianza zamani sana na uko fit kuliko hapa TZ
Yeye kaamua kuja kujifunza hapa Tanzania! Hajasema amekuja hapa kwakua ndipo mahali mradi ulikoanzia! Wala miradi haifanyiki ili tuonekane kuwa sisi ndio wa kwanza! Huko Colombia nenda wewe na ukawa wenzako mkawe wakwanza!
 
Mradi huu haukuanzia Dar au Tanzania. Hakuna cha kujifunza. Anayetaka aulize World Bank, na kwa nchi kama Colombia, mradi ulianza zamani sana na uko fit kuliko hapa TZ
Hata Africa kusini upo tokea kipindi cha Ubaguzi wa rangi
 
Wazimbabwe wana ya msingi ya kujifunza kutoka Tz, kwa mfano raisi kuamua kusema kama nchi hii kuna njaa au hakuna.
 
Yeye kaamua kuja kujifunza hapa Tanzania! Hajasema amekuja hapa kwakua ndipo mahali mradi ulikoanzia! Wala miradi haifanyiki ili tuonekane kuwa sisi ndio wa kwanza! Huko Colombia nenda wewe na ukawa wenzako mkawe wakwanza!
Nani kasema kila anaewakosoa ni Ukawa? Tambua kuwa wapo wananchi wasio na vyama wengi sana na kwa sasa njaa imeowaongeza kwa idadi kubwa zaidi.
 
Habari kama hizi za eti kuna nchi inayokuja kujifunza kwetu TZ huwa naona kama ni zakutunga tu,YAANI KABISA KUNA NCHI ZINATUONA SISI TUNA VITU VYA KUJIFUNZIA KWA AJILI YA WENGINE ........ Kweli nimeamini, thamani ya kitu ulichonacho anaiona ASIEKUWA NACHO SIO WEWE ULIYENACHO.
ni kweli kwa kiasi fulani Tanzania vingi vilivyopo si vya kujifunza kwani hata wakijifunza huenda kufanya vizuri zaidi ya Tanzania tena kwa kasi,mfano wa live ni juu ya kuhamia Dodoma miaka ilee.. Nigeria,malawi walijifunza kule CDA jinsi ya kuhamia miji mipya cha ajabu wao wamehamia tayari hata Brazil,india nk wamehamia miji mipya,lakini Tanzania bado inasua sua,hakuna dalili
 
Back
Top Bottom