Wakuu.
Hivi karibuni Prof Muhongo amekutana na nguvu ya umma Musoma mkoani Mara baada ya wananchi kujitokeza huku wakiimba "...tunaka hela zetu...".
Prof Muhongo ni waziri wa nishati na madini ambaye amewekwa kiporo kwenye sakata la ubadhirifu wa fedha za umma kupitia akaunti ya Tageta Escrow yenye ufisadi ambao umeitikisa CCM na nchi mwishoni kwa mwaka 2014.
Hivi karibuni amefanya ziara mkoani Mara ambayo inatafsirika kuwa ni dharau na kejeli kwa wananchi wa mkoa huo na Tanzania kwa ujumla hasa kutokana na kauli za mara kwa mara kuwa nchi inaongozwa kwa misingi ya utawala bora.
Zomea zomea hiyo ni muendelezo wa zomea zomea kadhaa ambapo imefika hatua gari au wafuasi na wanachama wa ccm wamekuwa wakipigiwa kelele za mwizi wanapopita kwenye maeneo mbalimbali wakiwa na sare au bendera za chama.
Angalia video clip uone nguvu ya umma ilivyo jikusanya na kuimba kudai hela zao.
Bofya hapa
https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=10204633415888386&id=1024755191&_rdr