VIDEO: NOKIA 6, Hardware durability tests.

Complex

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
4,118
4,765
Wale ambao mlikuwa na shaka juu ya ujio wa nokia na kusema kuwa simu za Nokia chini ya HMD na FOXCON hazitakuwa na roho ya paka kama Nokia za enzi zile nadhani mnapaswa mfute mawazo hayo akilini mwenu.

Kwani kuna physical test mdau mmoja kaifanya juu ya NOKIA 6 na kuonekana simu hiyo itafuata ugumu wa nokia tulizozoea za watangulizi wake. Hii hapo chini nimeambatanisha video ikionesha test hizo. Test hizo zinajumuisha kuikwangua simu kwa kitu chenye ncha kali. Hapa walikwangua kioo, Camera, LED flash Light, body ya simu kuthibitisha kama kweli ni bati nk. Pia simu ilijaribiwa kupindwa na kuonekana ipo imara (Haikukatika kama Iphone 6 zilivyokuwa zinakatika). Na mwisho kioo chake pia kimejaribiwa katika moto na kuonekana kiko safi

Na hapa chini ni video ikionesha NOKIA 6 ikisasambuliwa na kuachwa uchi kabisa.

Kiufupi inaonekana NOKIA hayupo tayari kuona jina lake linaharibiwa, tutegemee simu mawe na roho ya paka toka nokia. So far kwa video hizo, tayari nokia atakuwa ameshawin wateja wapya ambao wanapenda vitu durable. Wale fans wa Nokia kitambo, Tukae mkao wa kula tukisubiri bidhaa bora na ngumu toka NOKIA.

Na hapa chini ni drop test ya NOKIA 6.

Tatizo OS yake ya window kama haijapokelewa vizuri kwa users wa simu zenye OS ya Window
 
ndio simu pendwa kwa sasa nchini china na ndio simu ambayo imeuza batch 14 yaani kila batch ikitoka inauzwa ndani ya dk 1 mzigo umeisha pia ndio simu nngumu kwasasa
jana wamefanya comparison between Nokia 6 vs samsung S8 hasa kwenye speed na bado nokia 6 imenya poa(kumbuka n6 ni midrange phone vs flagship)

naisubiri hii simu kwa hamu kubwa ninunue
 
Nokia-6-Silver-Nokiamob-2ed-768x432.jpg
 
sjajua ni kwanini ameng'ang'ana na chipset ya snapdragon 400series wakati top tier ipo 8xx sa ivi
 
sjajua ni kwanini ameng'ang'ana na chipset ya snapdragon 400series wakati top tier ipo 8xx sa ivi
mkuu hii ni mid-range phone ingawa wametumia chipset ya snapdragon 430 ya low-end phones lakini bado ipo vizuri kwenye speed na kuhandle gemu kubwakubwa.
8xx inatumika kwenye flagship,subiri itakapotoka nokia 9 itajuja snapdragon 830 yenye dual camera,bezell-less display,dualpixel chini ya carl zeiss
 
sjajua ni kwanini ameng'ang'ana na chipset ya snapdragon 400series wakati top tier ipo 8xx sa ivi

Utumiaji wa chipset hiyo umesaidia katika bei, kwani simu hiyo ni ya watumiaji wa kawaida. Angejaribu kuweka hingend chipset maanake na bei ingekuwa juu pia kitu ambacho kisingekuwa kizuri kwani ni direct angekuwa anagamble ukizingatia NOKIA amekuwa nje katika smartphone market kitambo. Na kurudi kwake na high end smartphone kwa bei kubwa huku akiwa hajui wateja wake wa zamani na wapya watamkaribishaje ingekuwa ni risk ya kutosha.

Kuanza hivi ni move nzuri kwake kuanza kuwakusanya upya wateja wapya na wa zamani.
 
ndio simu pendwa kwa sasa nchini china na ndio simu ambayo imeuza batch 14 yaani kila batch ikitoka inauzwa ndani ya dk 1 mzigo umeisha pia ndio simu nngumu kwasasa
jana wamefanya comparison between Nokia 6 vs samsung S8 hasa kwenye speed na bado nokia 6 imenya poa(kumbuka n6 ni midrange phone vs flagship)

naisubiri hii simu kwa hamu kubwa ninunue
Simu ngumu ilikuwa ni htc one x, hii unaweza kuigeuza nyundo ya kugongelea misumari
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom