VIDEO - Mtu Mwenye Bahati Kuliko Wote Duniani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VIDEO - Mtu Mwenye Bahati Kuliko Wote Duniani

Discussion in 'International Forum' started by MziziMkavu, Nov 21, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  VIDEO - Mtu Mwenye Bahati Kuliko Wote Duniani
  [​IMG]
  Mtu mwenye bahati kuliko wote duniani Saturday, November 21, 2009 2:31 AM
  Kuna watu wana bahati duniani lakini huyu jamaa wa nchini Mexico ana bahati kuliko watu wote duniani. Alinusurika mara mbili kimiujiza ndani ya sekunde chache kugongwa na treni mbili zenye spidi kali zilizokuwa zikimkaribia toka pande mbili tofauti. Angalia VIDEO mwisho wa habari hii uone jinsi alivyonusurika kimiujiza. Mwanaume huyu wa nchini Mexico ambaye inasemekana alikuwa amelewa, alinusurika mara mbili kugongwa na treni mbili tofauti zilizokuwa zikija toka pande tofauti.

  Mwanaume huyo alikuwa akikatiza kwenye maungano ya reli nyingi wakati treni la kwanza lililokuwa kwenye spidi lilipomkaribia na ili kunusurika maisha yake alijirusha upande wa pili wa reli na kukoswa koswa na treni hilo.

  Akiwa bado na mawenge ya kukoswa koswa na treni la mwanzo, treni jingine lililokuwa likija toka upande wa pili nalo lilianza kupiga honi likimkaribia kwa kasi na kumfanya ajirushe tena kwa mara nyingine kurudi upande aliokuwa mwanzo.

  Kweli siku hiyo haikuwa siku yake ya kufa, jamaa alinyanyuka na kujikongoja taratibu toka eneo hilo.

  Chini ni VIDEO mbili za tukio hilo.


  VIDEO Namba 1- Mtu Mwenye Bahati Kuliko Wote Duniani


  VIDEO Namba 2 - Mtu Mwenye Bahati Kuliko Wote Duniani

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3584154&&Cat=2
   
 2. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mbona video hazionekani? au mpaka uwe na bahati ndo uzione?
   
 3. s

  staloneg Member

  #3
  Nov 22, 2009
  Joined: Oct 11, 2009
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo sio bahati bwana, mbona unataka kupotosha maana? Mi sikuelewi huyo mtu kabahatika vipi kiulevi, hizo video zenyewe ziko wapi??
   
 4. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  we nawe what are the odds of a dunken buffoon surviving two speed trains. Trust me bookies wata iweka in millions wakijua jama aponi.

  Hila sijui kama anabahati kushinda watu wote duniani, kuna couple majuzi wamelamba £45 million pounds tax free. Now hii ndio bahati kwangu.
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Nov 22, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  [ame="http://www.youtube.com/watch?v=q9cB5ENkJz4"]VIDEO Namba 1[/ame]


  [ame="http://www.youtube.com/watch?v=TFsa3kB5FP8"]VIDEO Namba 2 [/ame]
   
 6. Keynez

  Keynez JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 640
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 80
  Oooh shit! What's up with all these people nowadays 'playing' on train tracks, some even throwing their babies infront of incoming trains? Why they only release these videos when nobody gets hurt? Hopefully hatutayaona haya wahindi wakitujengea hizi treni za kasi!

  Take a look at this.
  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=-qfuowJQMu0&feature=related[/ame]
   
Loading...