Video: Lalamiko la Kocha wa Yanga halijaja "gafla" limeandaliwa. FF wasiliache lipite tu

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,632
2,413
Baadhi ya viongozi wa timu hizi kubwa hasa Simba na Yanga wamekuwa na desturi ya kutengeneza mazingira ya kuonyesha kuwa wanaonewa pale mambo yanapoanza kuwaendea kombo kwenye mashindano mbali mbali kwa lengo la kutafuta huruma ya Mashabiki wao.

Huu mkakati umesadia kuleta amani ya mda ndani ya klabu ya Yanga hasa hasa kwenye msimu wa ligi iliyoisha mwaka jana baada ya kuona mambo yanawaendea kombo wakaelekeza shutuma zao kwa Marefa na TFF na kufanikiwa ‘’kuwateka” mashabiki wao katika hilo na ndio maana hata baada ya kumaliza ligi bila kombe waliweza kuvumilika.

Baada ya kutambua kuwa Msimu huu mashabiki na wanachama wa timu hizi kubwa hasa Simba na Yanga hawataki tena visingizio hivyo visivyokuwa na miguu wala kichwa na wamejitambua na kugundua kuwa sababu ya kukosa ubingwa mwaka jana ilitokana ni makosa ya uongozi wa Yanga kushndwa kujipanga vyema na kuelekeza nguvu zaidi katika kufanya biashara ya kuuza jezi zaidi jambo ambalo limeonekana pia kufanywa mwaka huu na kupelekea kutolewa mapema katika mshindano ya Club bingwa Africa. Lakini vile vile ukiangalia jinsi walivyoanza ligi mwaka huu hata mechi zao mbili walizoshinda kwa goli (1-0) dhidi ya Kagera na Geita (iliyopanda ligi mwaka huu) ni ushindi wa "kulazimisha" kama walivyoanza wenzao Simba pia siwatetei lakini wenzao wa Simba wanaoekana kufanya vizuri katika ligi ya Club bingwa na kuna mwangaza unaonekana wa kufanya vyema tena katika ligi kuu ya mwaka huu.

Sasa kwa kuona hilo viongozi wa Yanga wanataka kutumia njia ile ile ya mwaka jana ya kupata huruma ya washabiki wake pale watakaposhindwa hivyo kuanza kuleta visingizio (ANGALIA VIDEO HAPO CHINI YA KOCHA WA YANGA).

Maswali machache ambayo nilitegemea waandishi wa habari wamuulize jana kocha wa Yanga ni

1. Kwani hiyo idadi ya wachezaji wa kigeni wanaoruhusiwa kucheza hapa nchini ni kwa Yanga tu au timu zoote zimeathirika?

2. Nini lilikuwa lengo la Yanga , Simba, Azam na club nyingine kusajili wachezaji wengi wa kigeni. Je ni kwa ajili ya ligi ya ndani au ligi ya Kimataifa?

3. Je ni kweli Yanga wanawahitaji hao wchezaji wa kigeni (kumi) kwa msimu huu mara baada ya kutolewa katika hatua za mwanzo kabisa za mashindano ya Afirca?

OMBI: Inaonekana TFF wamepunguza makali yao hasa baada ya “kutekwa” kiakili na “janja janja” ya Club hizi kubwa hasa SImba na Yanga kwa malalamiko yao katika ligi ya msimu uliopita kutokana na adhabu walizokuwa wanatoa hasa kwa viongozi wa Club hizi mbili.

Wanatakiwa kurudi katika mstari na kurudishwa makali yao vinginevyo ligi ya msimu itawashinda kwani tayari dalili zimeanza kuonekana…..(Mfano; wa jinsi walivyo “handle” ile kesi ya Yanga kutakiwa kulipa fine ya 11miliion kutoka CAF)

 
Wakati kanuni zinapelekwa kwa wadau kabla ya kujadiliwa utopolo ni klabu pekee waliopeleka maoni, hivi hawakuliona hili tatizo, inawezekana kifurushi kimekata na mashindano wanayoshiriki hayalipi wanatafuta vijisababu.
 
Malalamiko fc mmeshaanza mapema yote hii.

Kwani kucheza dhidi ya Rivers si mliruhusiwa kuchezesha wote vipi mpo makundi saivi?

Utopolo ni takataka tupa kwenye dustbin.
 
Back
Top Bottom