VIDEO - Kama Haujaandikiwa Kufa..

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20

3962042.jpg


Ni ukweli usiopingika kuwa kama hujaandikiwa kufariki basi hutafariki kwa njia yoyote ile. Ukweli wa kauli hiyo unathibitishwa na mwanaume aliyenusurika katika tetemeko la ardhi la Haiti baada ya kufukiwa chini ya ardhi kwa siku 11.Waokoaji toka mataifa mbali mbali walikuwa ndio wanajitayarisha kuondoka nchini Haiti kurudi kwenye nchi zao baada ya zoezi la uokoaji kusitishwa baada ya matumaini ya kumuokoa mtu kutoka kwenye vifusi kuonekana ni finyu.

Kama miujiza mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Wismond Exantus mwenye umri wa miaka 26 aligunduliwa na mama yake kuwa bado yupo hai chini ya kifusi cha hoteli aliyokuwa akifanya kazi ambayo iliporomoka chini yote.

Kaka yake alifika kwenye hoteli hiyo kuuchukua mwili wake baada ya waokoaji kuondoka lakini alipoweka spika na kuita jina lake sauti ilisikika kwa mbali ikitoka chini kwenye kifusi cha hoteli hiyo.

Kazi ya kuwatafuta waokoaji ambao wengi wao walishafunga virago ilianza mara moja. Watumiaji wa tovuti ya twitter walianza kutumiana meseji wakiwatafuta waokoaji.

Hatimaye waokoaji toka mataifa mbali mbali ambao walikuwa bado nchini Haiti walijitokeza na kuanza zoezi la kumuokoa Wismond.

Iliwachukua masaa machache waokoaji wa Ugiriki na Ufaransa kuweza kumtoa Wismond toka kwenye kifusi akiwa hai lakini akiwa taabani kwa njaa.

Wismond amekonda ghafla kwa siku 11 alizokaa chini ya kifusi kiasi cha kuhitaji kamba kuishikilia suruali yake isianguke.

Wismond anasema kuwa tangia siku ambayo tetemeko la ardhi lilitokea, alikuwa hauoni mchana wakati wote akiwa kwenye giza kama usiku.

Wismond aliendelea kusema kuwa siku za mwanzo za tetemeko la ardhi alikuwa akinywa soda zilizokuwa chini ya meza ambayo alikimbilia kujificha wakati tetemeko la ardhi lilipotokea.

Lakini baada ya soda hizo kuisha alianza kuunywa mkojo wake mwenyewe kila alipokojoa.

Wismond ni miongoni mwa watu wachache sana wenye bahati ambao wamefanikiwa kunusurika maisha yao kwenye tetemeko hilo la ardhi.

Hadi sasa inakadiriwa jumla ya watu 120,000 wamefariki kutokana na tetemeko hilo kubwa la ardhi ambalo lilikuwa na ukubwa wa 7.0.

Angalia video ya tukio la kuokolewa kwa Wismond chini.
 
Back
Top Bottom