KWELI Video hizi kuhusu Askofu Ruwa'ichi kuomba radhi zimetengenezwa kwa Akili Unde

KWELI Video hizi kuhusu Askofu Ruwa'ichi kuomba radhi zimetengenezwa kwa Akili Unde

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #2
View Source #2




1767251122239.png
 
Tunachokijua
Desemba 22, 2025 Vijana waliodai kuwa ni waumini wa kanisa katoliki nchini katika mkutano na waandishi wa habari walieleza kuwa waliwasilisha barua kwenda kwa balozi wa Vatikani nchini Tanzania kueleza kuhusu mwenendo wa Padri Dkt. Charles Kitima ambaye ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Wakatoliki Tanzania (TEC). Vijana hao waliweka bayana kuwa matamko yanayotolewa na Padri Kitima kuhusiana na kilichotokea Oktoba 29 yamekuwa sehemu ya kubeba hisia zake binafsi za kisiasa jambo ambalo limekuwa likichafua na kuharibu taswira nzima ya waumini wa Kanisa Katoliki nchini.

Akitoa homilia wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu Sherehe ya Kuzaliwa kwa Kristo Yesu katika Parokia ya Bikira Maria Mama wa Kanisa, Goba, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa'ichi OFMCap kuhusu Wakatoliki kumshtaki Padri Kitima, alimuita 'mwakilishi' huyo lofa, na kwa ulofa wake amethubutu kuwa mnafiki kwa kuvaa rozali shingoni ili wadhani ni Mkristo kweli, akisema huyo sio Mkristo kweli bali ni Kibaraka, Ndumilakuwili na msaliti ambaye anatenda maovu, anashabikia uongo na anajidai kwamba anamuwakilisha Kristo.

Madai

Kuanzia Desemba 27, 2025 kumekuwapo na vipande vya video vinavyosambazwa mtandaoni na kupata watazamaji wengi. Video ya kwanza inamuonesha mtu mmoja aliyetajwa kama "Padre Deo" akiwa kanisa akikosoa kauli ya Askofu Ruwa'ichi akibainisha kuwa kauli hiyo ni ishara ya kanisa kutokuwa na maadili. Lakini video ya Pili inamuonesha Askofu Ruwa'ichi akiomba msamaha na kwamba ni mihemko yake ya kutaka kuonekana kwenye mitandao.

Je, video hizi ni halisi?

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia nyenzo za kidigitali umebaini kuwa video hizo si halisi bali zimetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde. Vilevile sauti inayosikika haifanani na Sauti ya Askofu Ruwa'ichi.

Aidha Desemba 27, 2025 Askofu Ruwa'ichi aliongoza adhimisho la misa takatifu sikukuu ya Noeli na utoto mtakatifu ambapo hakutoa kauli yoyote ya kuomba msamaha kwa watanzania. Vilevile mavazi aliyoyatumia katika misa hiyo hayafanani na yanayoonekana kwenye video iliyotengenezwa kwa Akili Unde.​
1766936103667-png.3521842
Back
Top Bottom