SI KWELI Video hii inaonesha watu wakikimbia baada ya kushuka kwenye kivuko Kigamboni

SI KWELI Video hii inaonesha watu wakikimbia baada ya kushuka kwenye kivuko Kigamboni

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Wakuu nimekutana na hii video mtandaoni mara nyingi na inadaiwa kuwa ni kivuko cha kigamboni ambapo watu wakishuka huwa wanakimbia kwa spidi kama inavyoonekana kwenye video hiyo. JamiiCheck uhalisia ni upi?
1746599119131.png
 
Tunachokijua
Kumekuwapo na video inayosambaa mtandaoni ikiwaonyesha abiria wakishuka kwenye kivuko huku wakikimbia kwa kasi, ikidaiwa kurekodiwa maeneo ya Kigamboni, Dar es Salaam.

Ukweli wa video

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google Reverse Image Search ulibaini picha ya kivuko kutoka Kenya, inayofanana na ile iliyo kwenye video inayodaiwa kutoka Kigamboni. Picha hiyo ilichapishwa kwenye ukurasa wa Ferry Kenya , ambao hutoa huduma za feri katika vivuko vya Likoni na Mtongwe - Bandari ya Kilindini, Mombasa.

1746772907122-png.3328553
Rejea picha hii ili kubaini ufanano wa vivuko hivi.
img_20250509_215811_973-png.3329106


Zaidi ya hayo, video iliyochapishwa kwenye mtandao wa TikTok na mtumiaji anayetumia jina la @soljaboyib inaonyesha eneo baada ya kushuka kwenye kivuko ambapo gari la rangi ya njano linaonekana, ambalo awali lilionekana upande wa kushoto wa video hiyo, ambayo inadaiwa kutoka Kigamboni.
1746781859531-png.3328642
1746781893135-png.3328643


Kadhalika, kwa kutumia Google Earth , ikibainishasha kuwa ni Mombasa nchini Kenya, inaonyesha kuonekana kwa eneo hilo mwaka wa 2023 wakati hapakuwa na mmea, ambayo ni sawa na eneo lililoonyeshwa na mmea kwenye video.

1746782651246-png.3328656


Kwahiyo video ya kivuko hicho, abiria wakishuka huku wakikimbia, si ya Kigamboni, Dar es Salaam bali ni kutoka Mombasa, Kenya.​

Attachments

  • 1746599098549.png
    1746599098549.png
    147.2 KB · Views: 24
Hicho kivuko hakina uhalisia wa eneo la kigamboni kipo katika ferry ya KENYA.
Aidha, hali ya kukimbia kwa abiria eneo lile la ferry ni kitu cha kawaida.
 
Walau sasa watz tunaanza kusoma mambo ya msingi kama saikolojia ya makundi fulani.
Jumuisho la jumla ni kuwa tuna uinafsi mwingi na kila mtu anataka kuwa mbele ya mwenzie bila kujali unafikaje
 
Walau sasa watz tunaanza kusoma mambo ya msingi kama saikolojia ya makundi fulani.
Jumuisho la jumla ni kuwa tuna uinafsi mwingi na kila mtu anataka kuwa mbele ya mwenzie bila kujali unafikaje
Hiyo ni likoni ferry Mombasa Kenya
 

Attachments

  • Screenshot_2025-05-07-15-33-24-46_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
    Screenshot_2025-05-07-15-33-24-46_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
    406.3 KB · Views: 24
Hapa sio Kigamboni, hapana kivuko kikubwa kinachobeba watu wengi kama hao, pia hapana paving blocks
 
Back
Top Bottom