Video: Edward Lowassa na hali ya kisiasa nchini

Video: Edward Lowassa na hali ya kisiasa nchini

mtangazaji una maana gani kumuita lowassa waziri mkuu mstaafu?? hajawahi kustaafu ila alijiuzulu kwa kashfa.

kwa kiingereza anaitwa disgraced former prime minister.
 
nashindwa kumuelewa huyu si alikuwepo katika mkakati wa kuwaondoa akina mangii pale a-town/ana umoja gani
 
Kwanza niseme recording ya hawa swahili TV ni mbovu sana. Sauti hazisikiki vizuri, matangazo yanachomekwa bila utaratibu

Pili, nadhani aliye muhoji Lowasa hana uelewa mzuri wa mambo yanavyokwenda nchini. Kwa mfano Lowasa amejinasibu kuwa alibeba bendera ya chama katika suala la shule za sekondari. Hiyo anasema ilikuwa sera ya chama cha Mapinduzi.
Halafu anasema mpango ule ulivurugwa na sera za kilimo kwanza, ambazo alianzisha Mh Pinda
(1)Nilitegemea Lowasa aulizwe kama shule za kata ilikuwa sera ya CCM kilimo kwanza ilikuwa sera ya nani?

(2)Baada ya yeye kuacha uwaziri mkuu ni kikao gani cha chama kilikaa na kubadili sera hiyo na kama alikuwa na concern wakati hilo likjadiliwa.

Tatu,Lowasa aliposema tuna ardhi ya kutosha na iliyotengwa kwa wawekezaji, swali lingekuwa je hii migogoro inayotokea inasababishwa na nini hasa kama tayari ardhi ipo tya kutosha na ziada kwa wawekezaji

Nne, Lowasa alitakiwa aulizwe ni mbinu gani na kwa bajeti ipi angeweza ku-accomodate mamia ya wanafunzi anaosema wamemaliza shule za kata.

Tano, alitakiwa aulizwe kipi kinatangulia kuandaa walimu wa kufundisha kwa kujenga vyuo au kujenga shule na wanafunzi kuendelea kuzurura.

Sita, angeulizwa kuhusu suala la mabilioni ya fedha Uswiss na nini mtazamo wake kuhusu suala hilo.

Saba,Lowasa angeulizwa je, amani ya nchi anayoongelea inaweza kustawi kwa kampeni za kisiasa makanisani na misikitini? na je hilo haliwezi kuwa sababu ya kuvunjika kwa amani.

Na maswali mengine mengi tu. Nadhani hao wanaoendesha vipi wana tatizo la kuelewa mambo, hilo si jambo baya kama watajifunza vinginevyo interview nzima ilikuwa ya kumuosha Lowasa.

Hivi kuna tatizo gani na waandaji wa mahojiano Tanzania? Hawa wa Washington hawana tofauti na wale wa nyumbani sasa tatizo lipo wapi kiasi mtu hafahamu hata swali linalofutailia swali la msingi
 
angalieni watanzania nchi tunakoipeleka mimi gamba lakini kwa huyu bwana hapana hata hawa kina membe hamna kitu tuweni makini 2015
 
Siku zote napomfatilia Lowasa sijawahi ona akiizungumza maneno yenye maana hivi hajui tatizo kwetu si Elimu wala Kilimo kwanza bali ni utekelezaji wa hizo kaulimbiuzao.
 
Back
Top Bottom