VIDEO: Death By Stoning | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VIDEO: Death By Stoning

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kichuguu, Jul 6, 2010.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Jul 6, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
 2. M

  Mutu JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  noma duh
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  Kwa Nchi kama Pakistan,IRAN ana Somalia Hukumu hiyo ni halali kutopkana na sheria zao walivyopanga. Kwa Nchi kama ya kwetu hakuna sheria hiyo.

  Kumbukumbu la Torati/ Chapter 22
  22. Akifumaniwa mtu mume amelala na mwanamke aliyeolewa na mume, na wafe wote wawili, mtu mume aliyelala na mwanamke, na yule mwanamke naye; ndivyo utakavyoondoa uovu katika Israeli.


  23. Pakiwa na kijana aliye mwanamwali ameposwa na mume, na mwanamume akimkuta mjini, akalala naye;
  24. watoeni nje katika lango la mji ule, mkawapige kwa mawe hata wafe; yule kijana, kwa kuwa hakupiga ukelele, naye yu ndani ya mji; na yule mume, kwa kuwa amemtweza mke wa mwenzake; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.
   
 4. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2010
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  ...wokovu ukaletwa na Yesu Kristo, maandiko katika Agano Jipya yanaonyesha mabadiliko baada y akuja Yesu Kristo. Kundi lingine lilipotaka kumpiga mtu mawe Bwana akawaambia kati yenu asiye na dhambi awe wa kwanza kurusha jiwe, hakubaki mtu!
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Jul 6, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  .............yaani nilishindwa kuangalia video yote. Sikuamini kama binadamu wanaweza kuwa wakatili kwa binadamu wenzao namna ile.
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  / Mathayo/ Chapter 5 - 17. Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
  18. Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie.

  Mkuu MNDEE Unamsikia BWANA YESU Anavyosema hapo juu? hakuja kuibadilisha TORATI Ya Manabii bali Kuitimiliza. Sasa Wewe unaifuata TORATI Ya Manabii? Au Unamfuata Mtume Paulo Asiyefuata TORATI YA Manabii?

  Bwana Yesu Anasema tena soma hapa> / Mathayo/ Chapter 5-27. Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;
  28. lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
  29. Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
  30. Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.

  Mkuu MNDEE angalia leo siku nzima kuanzia sasa mpaka usiku utawaangalia wanawake wangapi wewe mkuu MNDEE na Wakristo wenzako? Na bwana yesu anasema hivi nanukuu ( 28. lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.)

  Haya utanipa jibu usiku Mkuu MNDEE umewaangalia Wanawake wangapi siku ya leo ? Na itabidi uling'owe jicho lako uliloangalia wanawake ili usipate kwenda nalo Jehanamu. Kuna Wakristo wangapi waliyoyatowa macho yao kwa ajili ya kuwaangalia wanawake kwa njia ya kuwatamani? Kuna Wakristo wangapi Waliokata Mikono yao iliyowakosesha?naomba jibu toka kwako mkuu MNDEE.
   
 7. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #7
  Jul 6, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Hicho kifungu cha 28 ndicho kinachofanya iwe ni vigumu kuwatupia mawe wote wanaozini, kwani wale wanaotamani tu nao wanafanya zinaa lakiini hawatatupiwa mawe.
   
 8. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2010
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
   
 9. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #9
  Jul 7, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,198
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Torati(sheria) ilikuwa ni kivuli cha mambo mema yaliyotarajiwa kuja, na Yesu kristo ndie sura au ujjuzi wa kweli wa kile kivuli cha kweli kilichoakisiwa na torati(sheria). Hivyo Yesu hakuja kukamilisha torati bali kutimiliza(fulfilment). Ndio maana katika injili sura ya mwishi ndani ya kitabu cha luka, Yesu anasema imempasa kutimiza yale yote aliyoandikiwa ndani ya sheria(torati) na manabii. Hivyo aiwafungua watu kwamba sheria ya kumhukumu mwingine inapaswa kufanywa na mtu asie na hatia yeyote, na hivyo kulibakisha suala hilo mikononi mwa Mungu pekee kwani hakuna binadamu aliye safi hata mmoja. Tunapewa haki kwa kura ya Mungu mwenyewe na hii tunaiita neema. Jambo hili linatendeka kwa yeyote mwenye kuzisadiki habari za mwana pekee wa Mungu yaani Yesu. Kinyume chake laana(hukumu) zote zilizopo katika torati(sheria) zinakuhusu na hazitanguki milele. Mungu ni pendo na amri iliyo kuu ni Upendo. Hivyo kwa mwenye upendo humpenda hata alie adui na kumwombea mema, maana huenda huyo mbaya leo ni mzuri kesho. Rejea kisa cha ngano na magugu. Ni nani awezae kunionyesha mtu aliye safi na ambae hana hatia yeyote hapa TZ ili awekwe kuzihukumu hukumu za Mungu? Epushia mbali hao wafanya biashara wa dawa za kulevya huko Iran na Pakistan waliojisimika wenyewe kuwa wahukumu wa mahakama wanayoiita ya Mungu.
   
Loading...