VIDEO: CHADEMA wavuruga jimboni kwa Naibu Spika Job Ndugai

Haki ya Mungu CHADEMA mnatisha. Mtaacha watu wafe kwa high blood pressure. Wanadhani wamewakomoa kumbe ndio chart limepanda. Tena jimboni kwa Naibu Speaker na michango juu. Naibu Speaker akiwapa za kuwatuliza mzuka wa hasira, wanazipeleka kwenye M4C. Yes, hii ni nouma.
 
Ndugai kinachomkalisa kwenye ubunge ni ndumba alizoachiwa na mama yake ...

Mkuu!

Hizo ndumba kwa CHADEMA zimebuma. CHADEMA ni mpango wa Mungu. Na kwa Mungu ndumba hazifui dafu. Ingekuwa hivyo basi wale wanao pishana pale karibu na ferry wangemsaidia mpangaji kuweka mambo yake sawa. Ila mambo yameshindikana ndio maana anajiliwaza na u-FastJet.
 
Mkuu Dingswayo tafadhali hebu weka mkanda mzima utupe raha ndani ya roho. Dakika mbili ulizoweka ni fupi mno kutokana na unyeti wa jambo lenyewe. Mkuu zingatia ombi hili tafadhali.

Mkuu, mimi nazipata hizi video moja kwa moja zilivyotengenezwa na zinawekwa youtube. Labda tuwaombe waliotengeneza waweze kutupatia mkanda mzima.
 
namba muweke still picture kama mlivyofanya kwa mikutano mingine.wengine tunatumia simu za kichina jama!!
CHADEMA YATOSHA,
NYINGINE YA NINI??
 
naomba muweke still picture kama mlivyofanya kwa mikutano mingine.wengine tunatumia simu za kichina jama!!
CHADEMA YATOSHA,
NYINGINE YA NINI??
 
Ndugai kinachomkalisa kwenye ubunge ni ndumba alizoachiwa na mama yake ...
Sasa hivi kwisha kazi. Na huko aliko ameshaanza kuhisi tofauti. Na ameshajua kinachoendelea kwamba kuanzia sasa uchawi na ndumba zote anazotumia ndungai hazitafanya kazi tena.Na mimi ninasema kama ifuatavyo:-"Baba katika Jina la Yesu. Ninasimama katika maneno yako unayoyaheshimu, ambayo unayaangalia upate kuyatimiza. Ulisema umetupa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge, na juu yakazi zote za yule mwovu. Kwa Jina La Yesu, Jina lenye mamlaka, ninaharibu uchawi wote anaotumia huyu mtu aliyetajwa hapa. Ninadhoofisha na kufisha kazi zote za ushirikina, nalegeza nguvu za wakuu anaowategemea, navunja madhabahu zote alizosimika na nafisha nguvu za makafara aliyoyatoa katika madhabahu zile. Ninabatilisha viapo vyote vilivyofanyika kusimika ufalme wake katika misingi ya giza. Na kuanzia sasa naagiza Roho ya ufahamu imrudie ili akatambue Wema na Ukuu wako Mungu ili akatende haki na Kukucha wewe Mungu wa Kweli uliyezifanya mbingu na nchi.Nimeomba nikiamini wewe ni Mungu uliyeagiza haya. Kuwafungua waliofungwa, kuwaweka mateka huru na kuwapa tumaini waliovunjika moyo. Katika Jina la Yesu Kristo aliyehai milele nimeomba. AMEN".Kila mtu aseme Amina.NDUGU ZANGU WANA JF. MAOMBI HAYA YAKO HAI. YATAFANYA KAZI KWA MTU YEYOTE AMBAYE ANATENDA MACHUKIZO KWA NGUVU ZA UCHAWI AMA MSUKUMO WA NGUVU ZA GIZA. YACHUKUE NA UYAWEKE CHINI YA JINA LA MTU YEYOTE UNAYEMKUSUDIA AMA AMBAYE UNAPENDA MUNGU AMFUNGUE NA YATAFANYA KAZI. KISHA UTAKUJA KUSEMA.MUNGU WETU NI BABA WA UPENDO. HANA MASHART KAMA WANGANGA WA KIENYEJI. YAFANYIE KAZI HAYA NA UTAONA MATOKEO YAKE.
 
Kwenda jimboni kwa mama makinda pia kwa ndugai ni mkakati mzuri.
Pia mngekuwa manweka na clip zao ili wananchi ambao hawkuona waone tena
"Tundu Lissu kila siku wewe tuu,,,,,,,.............askali to anje"
 
Mkuu, mimi nazipata hizi video moja kwa moja zilivyotengenezwa na zinawekwa youtube. Labda tuwaombe waliotengeneza waweze kutupatia mkanda mzima.
Huwa najiuliza kuna ugumu gani wa kurecord mikutano hii mwanzo mwisho na kuturushia Youtube??? Kwann chama kisiweke watu maalumu wa kucapture mkikutano yake mwanzo mwisho ili itumike kama darasa maeneo ambayo bado hayajafikiwa na habari njema a ukombozi???

Aidha, naunga mkono hoja ya wenzangu kuwa dakika mbili hazitoshi maana wengine tupo Tutition ya kuhutubia wananchi, tunajifunza namna ya kuongea na wapigakura ili mbinu hizo tuzitumie kwenye majukwaa ya kisiasa 2015 hivyo doze ya dakika 2 kwakweli haitoshi.
 
Back
Top Bottom