VIDEO - Bibi Anayetesa Kwenye Bongo Fleva, Bi Cheka Atamba Uzeen

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,322
33,126
VIDEO - Bibi Anayetesa Kwenye Bongo Fleva, Bi Cheka Atamba Uzeeni
6303598.jpg

Bi Cheka Ndani ya Studio
Sunday, March 11, 2012 1:56 PM
'Namuogopa babu, Bibi ananichekea cheka bibi ananirembulia bibi cheka damu yangu changa utaniweza?' 'Nitakuweza bwana mtu mzima dawa' hiyo ni miongoni mwa mistari inayopatikana kwenye nyimbo ya bibi mtu mzima ambaye kipaji chake kimeanza kuonekana uzeeni akitamba kwa jina la Bi Cheka.
Bibi mwenye umri mara tatu ya umri wa wasanii wengi wa bongo flava, ambaye anajulikana kwa jina la Bi Cheka ameingia kwenye gemu la muziki wa kizazi kipya na kuwapagawisha watu kwa mistari yake.

Bi Cheka ametoa nyimbo mpya inayojulikana kwa jina la "Ni wewe" ambayo amemshirikisha mkali wa Bongo Flava. Mheshimiwa Temba.

Bi Cheka mbali ya umri wake mkubwa sana ameonyesha uwezo wake wa kuchana mistari na kutishia amani ya wasanii vijana ambao wanalegalega katika fani.

Bi Cheka anasema mwenyewe kuwa bongo flava iko kwenye damu na anataka afike mbali sana kwenye anga hii ya muziki.

Swali ambalo watu wengi watakuwa wakijiuliza ni "Alikuwa wapi siku zote mpaka aibuke sasa hivi akiwa mzee".

Jibu analijua mwenyewe Bi Cheka ambaye ametamba kuwa ataendelea kuchana mistari kama vile "Nafanya Ninavyotaka, sifanyi mnavyotaka nyinyi, mnaonigeza nazidi kuwapoteza, mistari yangu iko juu, sihitaji majungu sipendi roho mbaya, beba kipaji changu na wala sibahatishi, msemayo siyo moto kamwe hamunitishi".


Angalia video za bi Cheka chini kujionea kipaji chake.





<tbody>
</tbody>




chanzo. VIDEO - Bibi Anayetesa Kwenye Bongo Fleva, Bi Cheka Atamba Uzeeni
 
Last edited by a moderator:
Singo ipo fresh tu. Bibi vocal yake imetulia vilevile ila kwa ushauri wangu, angefanya background music/voice over sijui jina lake la kitaalamu kwenye santuri za mashalobalo ingekuwa bomba zaidi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom