Vichwa vya Samaki na Dagaa

Ngai Moko

JF-Expert Member
Mar 21, 2016
1,281
1,700
Toka nikiwa mdogo na mpaka sasa huwa naona katika matumizi ya samaki(kula) watu wengi huwa hawali vichwa vya samaki pia katika maandalizi ya dagaa(mboga) watu huondoa vichwa.

Mi naona kuondoa vichwa vya dagaa ni kupunguza mboga, ikiwa mtu ananunua dagaa kilo1 inakadiriwa robo yake ni vichwa, ni kwa nini vichwa vya dagaa huondolewa na katika vichwa vya samaki kuna nn mbona huwa haviliwi?

Kama kuna maelezo ya kiafya juu ya uondoaji wa vichwa vya dagaa na samaki ningeomba nifahamishwe, maana toka nkiwa mtoto nimezoea kuondoa vichwa.
 
Vichwa vya dagaa huondolewa kwa sababu vina mchanga sio kwamba haviliwi!

In short watu ambao wamekulia maeneo yasiyo na samaki hawajui kumla samaki!
 
Inategemea na maandalizi dagaa alievuliwa majini na kuanikwa mahala pazuri bila kugusana na mchanga huliwa hivyo hivyo bila kuondolewa kichwa,jambo la ajabu ni hilo la kutokula kichwa cha samaki hivi mtu unaanzaje kwa mfano kutokula kichwa kitaaaamu cha sato!
 
Dagaa wale wa mwanza ukipata anayejua kuwapika aisee utatamani ule kila siku...tena huna haja ya kutoa vichwa..
 
Vichwa vya dagaa huondolewa kwa sababu vina mchanga sio kwamba haviliwi!

In short watu ambao wamekulia maeneo yasiyo na samaki hawajui kumla samaki!

Miaka nenda rudi, bibi yangu hajawahi kutoa vichwa kwenye dagaa eti kwa nia ya Kuondoa mchanga.

Huwa anaziloweka kwenye maji ya moto, baada ya nusu saa anaanza kuziosha mpaka mchanga unatoweka. Na ukila huwezi kukuta hata tone la jiwe.

Hata hao wanaoondoa vichwa kisa watoe mchanga hata wakipika mchanga utaukuta tu.


Dawa ni kuosha vizuri na sio kutoa vichwa, Kwanza unapunguza mboga pili unatumia muda mwingi.
 
Vichwa vya dagaa huondolewa kwa sababu vina mchanga sio kwamba haviliwi!

In short watu ambao wamekulia maeneo yasiyo na samaki hawajui kumla samaki!
Wale wa Kigoma mbona huwa hawana mchanga ikiwa mchanga unakaa kichwani?
 
Vichwa vya samaki vitamu sana hasa sato.

Vichwa vya dagaa hasa za mwanza sipendi ni vichungu,naishi kanda ya ziwa dagaa hatununui kwa kilo bali kisado au fungu ila vichwa lazima niviondoe.
 
Back
Top Bottom