Vichwa 3 na mabehewa 27 yaingia nchini; kuanza kufanyiwa majaribio hivi karibuni

Mabehewa na vichwa vyote hivyo sahizi vya nini wakati reli yenyewe ni kakipande tu?

Reli hii kukamilika, si chini ya miaka 8 ijayo. Inaonekana vichwa na mabehewa vinaletwa ili vipate kutu.

Kama ni kati ya Dar na Dodoma tu, robo ya vichwa na mabehewa, vingetosha. Miaka 8 ijayo, hayo mabehewa na vichwa vyake, vitakuwa nje ya modern technology.
Walete ugali na nyama?

Pumbavu sana wewe
 
Serikali imeingiza nchini Mabehewa 27 na vichwa vitatu vya treni kwa ajili ya kuanza majaribio ya SGR.

Ni yapi maoni yako kuhusu kasi ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati iliyoanzishwa na JPM? Je, waliolalamika kuwa mabehewa ya awali siyo ya SGR wanakauli gani leo? Hongera Mhe. SSH kwa hatua hii yautekelezaji wa miradi ya kimkakati.
---
Shirika la Reli Tanzania (TRC) leo December 30,2023 limepokea vichwa vipya vitatu vya treni za umeme vilivyoundwa na kampuni ya Hyundai Rotem na mabehewa mapya 27 ya abiria yaliyoundwa na kampuni ya ‘Sung Shin Rolling Stock Technology’ (SSRST) kutoka nchini Korea Kusini.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano- TRC, Jamila Mbarouk amesema “Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania ilifanya manunuzi ya vichwa vipya 17 na mabehewa mapya 59 ya abiria kwa ajili ya uendeshaji wa reli ya kiwango cha kimataifa - SGR, mpaka sasa Shirika limepokea vichwa vya treni ya umeme vinne kati ya 17 kutoka kampuni ya Hyundai Rotem na mabehewa 56 kati ya 59 kutoka kampuni ya ‘Sung Shin Rolling Stock Technology’ (SSRST) ya chini
Korea Kusini”

“Mabehewa matatu yaliyosalia yanatarajiwa kuwasili nchini Februari, 2024 na vichwa 13 vilivyobaki vinatarajiwa kuwasili kwa awamu ambapo vichwa sita vitawasili mwezi Machi na vichwa saba vitawasili April 2024”

“TRC itaanza kupokea seti ya kwanza kati ya seti 10 za treni za Kisasa (EMU) mwezi Machi 2024 Mei seti 2, Juni seti 2, Julai seti 2, Septemba seti 2 na seti ya mwisho mwezi Oktoba 2024”

“Vichwa vilivyopokelewa, kiutendaji vina mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa, mabehewa 27 katika madaraja ya uchumi na biashara, daraja la biashara (Business class) ni mabehewa 13, kila behewa lina wezo wa kubeba abria 45 na mabehewa ya daraja la uchumi ni 14, kila behewa lina uwezo wa kubeba abiria 78 kwa kuzingatia viwango vya kimataifa kumuwezesha abiria kusafiri kwa amani na salama”
Samia anaendelea kufunga mwaka Kwa kishindo
 
Both kwa uadilifu gani hapa bongo... Sometimes Unafiki na Uchawa ni bora ukauficha kwa kuacha kujibu watu wenye kujua nini cha kuhoji.
Actually ubwege wako ndio uufiche because it is stupid to think kila kitu hakiwezekani

Puuzi sana bwege wee
 
Actually ubwege wako ndio uufiche because it is stupid to think kila kitu hakiwezekani

Puuzi sana bwege wee
Chawa ni chawa tu
Siwezi kupoteza muda kubishana na mdudu.
Shame on you CHAWA.
 
Walete ugali na nyama?

Pumbavu sana wewe

Tambua jukwaa hili ni kwaajili ya watu wenye akili timamu, wanaochangia au kubishana kwa hoja.

Ninyi msio na uwezo wa kujenga hoja, na kuishia kutukana watu, hapa siyo mahali pema.

Mods, watu wanaotukana wachangiaji bila sababu za msingi, kanuni zisimamiwe.
 
kiukweli na bila kuacha chochote na nitakuwa nimekamilisha jf kwa sasa imekuwa ni jamvi la matusi bustani la kutukania tafadhalini tujirekebishe
 
Tutauza kwa kuvipima mizani boss!!!
Mabehewa na vichwa vyote hivyo sahizi vya nini wakati reli yenyewe ni kakipande tu?

Reli hii kukamilika, si chini ya miaka 8 ijayo. Inaonekana vichwa na mabehewa vinaletwa ili vipate kutu.

Kama ni kati ya Dar na Dodoma tu, robo ya vichwa na mabehewa, vingetosha. Miaka 8 ijayo, hayo mabehewa na vichwa vyake, vitakuwa nje ya modern technology.
 
Tambua jukwaa hili ni kwaajili ya watu wenye akili timamu, wanaochangia au kubishana kwa hoja.

Ninyi msio na uwezo wa kujenga hoja, na kuishia kutukana watu, hapa siyo mahali pema.

Mods, watu wanaotukana wachangiaji bila sababu za msingi, kanuni zisimamiwe.
ILA kuitwa chawa sio kutukanwa

Shelf your biased crap aisee

Tusifuatane fuatane
 
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano- TRC, Jamila Mbarouk amesema “Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania ilifanya manunuzi ya vichwa vipya 17 na mabehewa mapya 59 ya abiria kwa ajili ya uendeshaji wa reli ya kiwango cha kimataifa - SGR, mpaka sasa Shirika limepokea vichwa vya treni ya umeme vinne kati ya 17 kutoka kampuni ya Hyundai Rotem na mabehewa 56 kati ya 59 kutoka kampuni ya ‘Sung Shin Rolling Stock Technology’ (SSRST) ya chini
Korea Kusini”
Aweke picha hatununui mbuzi kwenye gunia
 
Hamna hata kapicha kidogo?

Hamsikii haya kila siku kudanganya? Unakumbuka mara ya kwanza mlisema ni lini hii treni ingeanza kazi?
Ili kumuelewa mwanasiasa chochote anachoahidi wewe geuza kiwe kinyume 🤔
 
Back
Top Bottom