Ha ha ha, acha tu, enzi za utoto nilikuwa nacheza sana playstations soccer games mpaka washkaj wakaniita king of pes(ni famous football game) sasa hizo mbwembwe nilizokuwa nazo ni balaa maana kila napoalikwa nicheze na mtu nashinda kwa kishindo,,
Sasa kipindi nipo chuo kuna mshkaji school mate alirud toka majuu na sister wake kama kawaida akatualika kwao mikochen tukacheze league tujikumbushe enzi si unajua mambo ya kualikana kwa friends wa mjini, basi bana kule tukakutana na wadada wa mikocheni jiran zake huku wamekaa sana majuu ( si unajua ulaya hakuna kuzurula unashindia games tu na tv).. Kumbe nao wanajua balaa..
Mtu mzima nikaanza majitambo yangu kama kawa ikawa zamu yangu na sister mmojawapo,,, kitu ps3 imefungwa kwenye plasma full high definitions
Mtu mzima nilikula 5-O kama nimesimama na kuzidiwa kila kitu ambayo haijawai tokea for almost 13 yrs of playing football games..
Yaan huyo dada kuanzia kupanga team mpaka kucheza ni balaa,, ikabid baada ya mechi watu wamuweke mtu kati na kuanza stories za soka za kawaida,, yaan anajua mpira humdanganyi kitu anafatilia hadi copa libertadores ( champions league ya america kusini)
Baada ya pale washkaji walinicheka kwamba kuwanyanyasa tangu utoton nimevuliwa ubingwa na mdada kwa kuzidiwa kila kitu.. Niliondoka mdogo kama pirton