VICHAPO vya MAN UTD vinaniharibia UHUSIANO Wangu! Wapi RVP? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VICHAPO vya MAN UTD vinaniharibia UHUSIANO Wangu! Wapi RVP?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by lara 1, Oct 2, 2012.

 1. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  Khabari Wanajamviii!!!

  Mie mzima, ila ndo hivo tena husikeni na kichwa cha habari hapo juu!!!


  Mi ni mdada kati ya wadada wachache wanazi wa soka, si la nje si la ndani, yote nimo. Huko nje niulize Ligi gani nisiyofatilia Si Premier League, La Liga, Seria A, Bundensliga (Unabisha nini?) hadi League 1 bila kusahau FA na UEFA!!!! Njoo bongo mimi Yanga Damuuu!

  Kijamii haipendezi binti kuwa shabiki wa mpira namna hiii! Unaweza kukosa mume atiii hasa akiwa timu pinzani!!! LOL! Kama mjuavyo mpira gharama sana, DST ya SS chanel si mchezo, hivo siku za ball inabidi kutafuta ustaarabu! Kuna mtu wangu tuna date bana! Kwao mambo poa, Kitu LG Flat Screen, Nchi kibao, LED, High Definition, Crystall Clear, DST full Package afu hakuna kelele za bar, ila shurti tuangalie mpira na Dingi yake a.k.a Bamkwe!!!! Mpo Hapo?

  Mi nikakubali, kwani Babamkwe anang'ata? Simba mkali ila anazaa vile vile! Ila Dingi Mchaga Mkoloni Haswaaaa! Mi kufika pale na vitenge vyangu (niliombwa nizingatie itifaki ya kwenda ukweni!!! LOL!) Dingi kaniuliza mama wewe timu gani? Machale yakanicheza!!! Mi chelsea Damuuuu, afu inafatia Arsenal! Ila nikamtega Mkwe! Baba kwani we timu gani? Dingi kafunguka Mi Man UTD damuuu! Nilisoma textiles Manchester sijui chuo gani, BLAH! BLAH! BLAH!

  Nikaona ishakuwa soo, ngoja NIHAMIE KUSHABIKIA MAN UTD kwa MKOPO, basi nikajifanya MAN U damu, full kuwataja kina Andy Cole na Dwight York, sio Robie Kean, hadi mkongwe Teddy Sherigham, scholes ndani, bonge nyanya Rooney ndani, hadi Sung Park nikamtaja, hata Rafael na mwenzi wale madogo mapacha mmoja kahamishwa kwa mkopo, ndani ya story, Beckham Hakusahaulika hadi Peter Shmichael alikumbukwa!!! RVP nae ndani ya stori. Basi Dingi akanidhibitisha pasi shaka lolote mie ni MAN UTD Damuu! (CHEZEA KUMUIPRESS MKWEO KIFOOTBALL?)

  Ball likanzaa kama kawa Totenhama Hot Spurs wakawa wanagawa DOZI NENE, Bonge nyanya Rooney hoi, nafurahije, japo usoni nipo kihuzuni!! Ikaendelea, Dingi anasunya tu, hadi akaanza kujidunga mzinga wa konyag, mie roho kwatuuuu! Kimbembe THS walipo piga bao la tatu ikawa 3-1 nikajisahaa si NIKARUKA JUUU ! Yeaaaaaah! nikiwa juu nikakumbuka hili soo basi nikamalizia YEAHHHHHH! SHIIIIIIIIIT! STUPID KABISA! Bahati yangu nikiwa katika kuzuga MAN UTD wakarudisha moja!! Salaleeeeee! LOLEST!

  Kosa kosa zilivoanza dingi akawa ashanitilia shaka MIMI NI MAMLUKI wa CHELSEA!!! LOL! 5minutes baada ya kurudisha la 2 dingi AKAZIMA TV YAKE NA KUINGIA NA REMOT CHUMBANI. Akamwbia mwanae mpleke hapo Bar mkamalizie kuangalia!!! IMAGINE!!!!! Umamluki wote ukanitoka! LOL! BF alinilaumuje!!! Hadi leo kanuna!! Nikamalizia kwa kucheki score LIVE SCORE na kwa SHAFII DAUDA BLOG!!!

  Hapa sina pa KUANGALIA BALL TENA WADAU!! WENYE BIG SCREEN MNIOKOE!!! Mpaka league iishe mbona nitakuwa sina Bwana!!!!
   
 2. Emmadogo

  Emmadogo JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 4,162
  Likes Received: 3,384
  Trophy Points: 280
  ha ha ha ha nimeipenda hiyo, RAHA YA MECHI ANGALIA YA MWENZAKO.........we usingemdanganya......ushangilie vzr
   
 3. Emmadogo

  Emmadogo JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 4,162
  Likes Received: 3,384
  Trophy Points: 280
  mimi mbona angelia na U-LIVERPOOL WANGU DAMU..........ANGEBEBA TV KABISA
   
 4. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  lara 1 du kaazi kweli2, ila mashbiki wa mpira wa kike 2po wengi, binafc ni mnazi namba 1 wa mpira wa miguu, ila twapishana interest 2, kwa premier lig inanikosha arsenal, c umeona kitu tulowauzia RVP? kwa la liga barca ndo mpango mzima, ukirudi home wekundu wa msimbazi ucpime moto!! ila ucife moyo we endelea kupretend kuifagilia man u usijeukapigwa kibuti bana, kwani hawa wanaume wa kibongo wengi wanathamini mpira kuliko hata mke, na kama ndo favorite timu yao then akiona unamzingua dingi aweza kukupiga ban kwa muda,so keep on pretending, ila man u watarudi 2 kwenye level zao c unajua full kubebwa !!angekuwa arsenal sasa huyo mkweo ingekuwa vipi?? manake huku gonjwa la moyo full presha
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  Angeona mie ndo nimetia kigundu, afu asingekubali tucheki wote kuogopa nitachonga NGENGA SANAA akifungwa, kama ilivotokea!!! LOL!
   
 6. Emmadogo

  Emmadogo JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 4,162
  Likes Received: 3,384
  Trophy Points: 280
  WE LARA mi nakwambia bora ujiachie tu, unazi hauna kujipretend, haya siku chelsea na man u itakuaje, utajikuta umenyanyuka kitini bila ya kupenda torres akikaribia lango, mi shabiki kweli ndo maana nakwambia hv. vile vitu viko damuni so pretending ni ngumu sana, kama mwenywe umesema uliruka dempsey alivyokandamiza la tatu ......
   
 7. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  Hahahaaaaaa! Nabembeleza NDOA mwenzio atiiii!!!! Afu ndo maana wenye DSTV hawakaribishagi watu majmbani waje wacheki ball!!!!
   
 8. Emmadogo

  Emmadogo JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 4,162
  Likes Received: 3,384
  Trophy Points: 280
  unaweza kuhama dini sio TIMU YA KUSHABIKIA. FOOTBALL IS A NEW RELIGION
   
 9. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #9
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  Mwenzangu huoni nimepigwa BAN ya kujiachia kwenye LED, Crystal Clear, Nahaha tu hapa, jmosi sijui naenda angalia Wapi kwenye vikwapa bar huko!!!!
   
 10. Emmadogo

  Emmadogo JF-Expert Member

  #10
  Oct 2, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 4,162
  Likes Received: 3,384
  Trophy Points: 280
  Raha ya mpira ndo uangalie huko kwenye bar/ wapinzani wengi, full kutaniana ndo raha ya kuchek mpira, but peke yako au na baba mkwe meeeeeeeen!!!!!! Siwezi coz si unajua mara beki katoa boko naweza kutukana mie
   
 11. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #11
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  Mie nikianzaga kuchonga NGENGA mtindo wa KINOCLAIN, Nanusurika kupewaga NAKOZZZ!!!! Mpaka kuna siku mtu akapiga NDO MAANA ARABUNI WANAWAKE NO KUCHEKI BALL, sababu hii hii ya kuleta MISUTANO kwenye BALL!!! Mwendo ispite hata MENU ya Ball Poseeion, Sijui Coner, NK NK lazima NIROPOKE SOMA MENU! SOMA MENU! Watu wananunaje????
   
 12. The Don

  The Don JF-Expert Member

  #12
  Oct 2, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 3,455
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Yan nimejenga picha ulivokuwa especialy ulivonyanyuka na kuropoka nimecheka sana,kweli you made my day,ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu eeeeh.
   
 13. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #13
  Oct 2, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,956
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Na huyo anayetaka kukuoa inabidi awe makini sana, maana unaweza kuwa unamzuga kuwa unampenda kumbe wewe ni mamuluki wa chelsink! Ningekuwa mimi ningekupiga chini kwa kosa la kusema uongo, tena hadharani.
   
 14. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #14
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,092
  Likes Received: 11,227
  Trophy Points: 280
  Ingekua liverpool, angebomoa tv
   
 15. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #15
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  Bwana weeeeee! Acha tu, niliumbuka! hata ushindi sikuufaidi sana.
   
 16. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #16
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,312
  Likes Received: 1,783
  Trophy Points: 280
  lara 1 una kazi kweli kweli. Unasema unabembeleza ndoa? teh teh teh! Kila la kheri..ndoa ndoano ati.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #17
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  Huyo BF yeye ni MAN CITY japo alihamia kutoka MAN UTD, ila anogopa kumwambia Dingi yake kuwa AMENYEA KAMBI!!! LOL! Tulikuwa wote PARTNERS IN CRIME ila mimi midadi ikanizidi NIKAUZA CD.
   
 18. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #18
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  Hasa babamkwe akiwa timu pinzani ndugu!!!!
   
 19. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #19
  Oct 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  asante sana sana kwakuwa anti manure from old trashford nakupa tano karibu mtaani kwetu kuna bar kibao mabanda ya kuonesha mpira kwa big screen aka projector yapo ya kumwaga...

  pole sana kwa kukosa mume mujanja...
   
 20. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #20
  Oct 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  malizia na nyagi za bure bure from bamkwe..
   
Loading...