VICHAPO vya MAN UTD vinaniharibia UHUSIANO Wangu! Wapi RVP?

Ok...Nilifikiri unambembeleza babamkwe asilie...akikomaa na wewe itakuwaje? teh teh teh...hakuna mzee mjini Dar. Uzee mwisho Chalinze.

Hahahaaaaaa! Nimesema hapo ni MKOLONI full! Hawezi labda atakuwa anijisevia MIJIMAMA ya enzi zile!
 
Hahahaaaaaa! Nimesema hapo ni MKOLONI full! Hawezi labda atakuwa anijisevia MIJIMAMA ya enzi zile!

Tena wale wa moshi ndo kabisaa...au hujui mambo yalivyokuwa yanakwenda? Uzee mwisho chalinze...kaa chonjo mjini hapa.
 
Tena wale wa moshi ndo kabisaa...au hujui mambo yalivyokuwa yanakwenda? Uzee mwisho chalinze...kaa chonjo mjini hapa.

Hahahaaaa! Nashukuru kwa ONYO ila NAJIAMINIA hawezi kunizidi akili, Nimezaliwa hapa hapa MUJINI sikuja na mabegi!!! LOL! na NIMENGANGANIA SO FAR, pamoja na kupata kazi shirika kubwa MKOA nimegoma kwenda!!!! TUTABANANA HAPA HAPA!!!!
 
Khabari Wanajamviii!!!

Mie mzima, ila ndo hivo tena husikeni na kichwa cha habari hapo juu!!!

Mi ni mdada kati ya wadada wachache wanazi wa soka, si la nje si la ndani, yote nimo. Huko nje niulize Ligi gani nisiyofatilia Si Premier League, La Liga, Seria A, Bundensliga (Unabisha nini?) hadi League 1 bila kusahau FA na UEFA!!!! Njoo bongo mimi Yanga Damuuu!

Kijamii haipendezi binti kuwa shabiki wa mpira namna hiii! Unaweza kukosa mume atiii hasa akiwa timu pinzani!!! LOL! Kama mjuavyo mpira gharama sana, DST ya SS chanel si mchezo, hivo siku za ball inabidi kutafuta ustaarabu! Kuna mtu wangu tuna date bana! Kwao mambo poa, Kitu LG Flat Screen, Nchi kibao, LED, High Definition, Crystall Clear, DST full Package afu hakuna kelele za bar, ila shurti tuangalie mpira na Dingi yake a.k.a Bamkwe!!!! Mpo Hapo?

Mi nikakubali, kwani Babamkwe anang'ata? Simba mkali ila anazaa vile vile! Ila Dingi Mchaga Mkoloni Haswaaaa! Mi kufika pale na vitenge vyangu (niliombwa nizingatie itifaki ya kwenda ukweni!!! LOL!) Dingi kaniuliza mama wewe timu gani? Machale yakanicheza!!! Mi chelsea Damuuuu, afu inafatia Arsenal! Ila nikamtega Mkwe! Baba kwani we timu gani? Dingi kafunguka Mi Man UTD damuuu! Nilisoma textiles Manchester sijui chuo gani, BLAH! BLAH! BLAH!

Nikaona ishakuwa soo, ngoja NIHAMIE KUSHABIKIA MAN UTD kwa MKOPO, basi nikajifanya MAN U damu, full kuwataja kina Andy Cole na Dwight York, sio Robie Kean, hadi mkongwe Teddy Sherigham, scholes ndani, bonge nyanya Rooney ndani, hadi Sung Park nikamtaja, hata Rafael na mwenzi wale madogo mapacha mmoja kahamishwa kwa mkopo, ndani ya story, Beckham Hakusahaulika hadi Peter Shmichael alikumbukwa!!! RVP nae ndani ya stori. Basi Dingi akanidhibitisha pasi shaka lolote mie ni MAN UTD Damuu! (CHEZEA KUMUIPRESS MKWEO KIFOOTBALL?)

Ball likanzaa kama kawa Totenhama Hot Spurs wakawa wanagawa DOZI NENE, Bonge nyanya Rooney hoi, nafurahije, japo usoni nipo kihuzuni!! Ikaendelea, Dingi anasunya tu, hadi akaanza kujidunga mzinga wa konyag, mie roho kwatuuuu! Kimbembe THS walipo piga bao la tatu ikawa 3-1 nikajisahaa si NIKARUKA JUUU ! Yeaaaaaah! nikiwa juu nikakumbuka hili soo basi nikamalizia YEAHHHHHH! SHIIIIIIIIIT! STUPID KABISA! Bahati yangu nikiwa katika kuzuga MAN UTD wakarudisha moja!! Salaleeeeee! LOLEST!

Kosa kosa zilivoanza dingi akawa ashanitilia shaka MIMI NI MAMLUKI wa CHELSEA!!! LOL! 5minutes baada ya kurudisha la 2 dingi AKAZIMA TV YAKE NA KUINGIA NA REMOT CHUMBANI. Akamwbia mwanae mpleke hapo Bar mkamalizie kuangalia!!! IMAGINE!!!!! Umamluki wote ukanitoka! LOL! BF alinilaumuje!!! Hadi leo kanuna!! Nikamalizia kwa kucheki score LIVE SCORE na kwa SHAFII DAUDA BLOG!!!

Hapa sina pa KUANGALIA BALL TENA WADAU!! WENYE BIG SCREEN MNIOKOE!!! Mpaka league iishe mbona nitakuwa sina Bwana!!!!

Nimepapenda hapo Baba mkwe aliposema anaipenda Man U damu damu becausea alisoma Leeds Varsity mambo ya Textiles hahaha:biggrin:
 
Hahahaaaa! Nashukuru kwa ONYO ila NAJIAMINIA hawezi kunizidi akili, Nimezaliwa hapa hapa MUJINI sikuja na mabegi!!! LOL! na NIMENGANGANIA SO FAR, pamoja na kupata kazi shirika kubwa MKOA nimegoma kwenda!!!! TUTABANANA HAPA HAPA!!!!

Kwani hujui ndege mjanja ndio ananaswa na tundu bovu? Kuja na mabegi inaweza kuwa faida kuliko kuzaliwa mjini na kuendelea kuishi kwa mazoea wakati mambo kibao yanabadilika.
 
Nimepapenda hapo Baba mkwe aliposema anaipenda Man U damu damu becausea alisoma Leeds Varsity mambo ya Textiles hahaha:biggrin:

Sikumbuki kama alisema Leeds Varsity au jina gani, coz i wasnt realy lisening. Ila mwenzio sijawahi KUVUKA BAHARI nyie wa huko ndo mwayajua, ila yeye alisomaga 70s na 80s huko! Yawezekana ni hicho chuo au hata ukute alisomaga certificate ya Textiles! LOL!
 
Kwani hujui ndege mjanja ndio ananaswa na tundu bovu? Kuja na mabegi inaweza kuwa faida kuliko kuzaliwa mjini na kuendelea kuishi kwa mazoea wakati mambo kibao yanabadilika.

Mambo twayabadilisha sie atiiiii!!!! Haya ya mujini yanatuchosha twaamua kimix na ya NG'AMBO YA BAHARI HUKO!!!! Ndo mabadiliko yenyewe. Mgeni mgeni tu! Kuku mgeni hakosi KAMBA mguuni atiiiii!
 
Duh lara nakukubali

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mi sina time na mpira hata kidogo wala sijui chochote ila ulivyohadithia nimecheka hadi machozi nimejiamulia nikitaka kufurahi naangalia thread zako maana dah
 
Washabiki wa mpira kazi mnayo. Mpira ni moja kati ya vitu ambavyo havininyimi usingizi kabisaaa.
 
lara 1 bana..lol ..yaani msredi wako unavyoupamba utadhani movie vile..
Ndio taabu ya kudanganya hiyo aisee..Kuna siku Jamhuri Morogoro nilikaa jukwaa la Ndala huku mie Msimbazi ebwanaee..nilijikaushausha mwanzoni ila baadaye wachache walinistukia..sema sikuwa na midadi kama yako vinginevyo wangeniua...
 
Last edited by a moderator:
nimecheka sana....though sisi si wakufungwa hovyo mkuu...badilisha heading yako iwe kichapo si vichapo...
 
nimecheka sana....though sisi si wakufungwa hovyo mkuu...badilisha heading yako iwe kichapo si vichapo...

Msimu huu MTACHAPWA SANA, kwa kiwango mlichoonesha jmosi? Aisee ni VICHAPOS!!!!
 
lara 1 bana..lol ..yaani msredi wako unavyoupamba utadhani movie vile..
Ndio taabu ya kudanganya hiyo aisee..Kuna siku Jamhuri Morogoro nilikaa jukwaa la Ndala huku mie Msimbazi ebwanaee..nilijikaushausha mwanzoni ila baadaye wachache walinistukia..sema sikuwa na midadi kama yako vinginevyo wangeniua...

Ungekula NAKOZZZZ za hatari, wasingechelewa kukuita MWANGA!!!!!
 
teh teh teh, lara 1 umenikosha sana. mnimeupenda mtiririko wa stori. Haya hebu niambie huko ligue 1 unashabikia timu gani?
 
Last edited by a moderator:
mimi arsenal damu damu
nina bahati mbaya mpenzi wangu man u na ninavoichukia man u...huwa najisahau namchanganya humohumo
na ole wake man u watufunge
mapenzi yetu yataisha siku hiyo hiyo
 
teh teh teh, lara 1 umenikosha sana. mnimeupenda mtiririko wa stori. Haya hebu niambie huko ligue 1 unashabikia timu gani?

Olympic Marseil wenyewe tunaiita (Olymique de Marseille). si unajua tena zamani nilikuwa nawazimikia MABAHARIA, wakirudi kitaa KINOCLAIN baada ya kuiona Bahari na swagga za kibrother man!!! LOL! Hata PSG (Paris Saint Germain) yanikoshaga mwisho namalizia na Vallencia!!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom