Vicent Mritaba Meja Jenerali Mstaafu wa JWTZ Apelekwa South Africa kwa Matibabu

Mzalendo80

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
2,508
1,338
Wakati Rais wa TLS na Mbunge wa Singida Mashariki Mh. Tundu Lissu akitibiwa huko Nairobi kwa Gharama ya Chadema pamoja na Michango ya Watanzania. Serikali imeamua kumpeleka na kulipia gharama zote za Meja Vicent Mritaba.

Meja Jenerali Mstaafu wa JWTZ Amepelekwa leo asubuhi South Africa kwa Matibabu. Meja Vincent inasemekana hali yake sio nzuri tangu ajeruhiwe kwa risasi maeneo ya Ununio, Dar Es Salaam.

Meja Jenerali Vincent Mritaba anapata matibabu katika Hospital ya Unitas iliyopo Centurion nje kidogo ya Mji mkuu wa South Africa, Pretoria.

Netcare_Unitas_Hospital_main.jpg
 
Wakati Rais wa TLS na Mbunge wa Singida Mashariki Mh. Tundu Lissu akitibiwa huko Nairobi kwa Gharama ya Chadema pamoja na Michango ya Watanzania. Serikali imeamua kumpeleka na kulipia gharama zote za Meja Vicent Mritaba.

Meja Jenerali Mstaafu wa JWTZ Amepelekwa leo asubuhi South Africa kwa Matibabu. Meja Vincent inasemekana hali yake sio nzuri tangu ajeruhiwe kwa risasi maeneo ya Ununio, Dar Es Salaam.

Mwanzo mlisema hakushambuliwa lilikuwa ni igizo sasa hivi mnakuja na hoja nyingine!

Utaratibu wa kugharimiwa Huduma za Matibabu nje ya Nchi na Serikal upo na lazima ufuatwe!

Kibali cha kutibiwa nje ya Nchi hutolewa na Jopo la Madaktari sio Wanasiasa Kama unataka hizo Gharama zibebwe na Serikal!
Absalom Kibanda alipojeruhiwa Rostam Azizi alimpeleka South Africa kwa Gharama zake kwa kuwa hakuwa na kibali cha Rufaa toka Kwa Madaktari

Saed kubenea alipomwagiwa Tindikal alipelekwa India kwa Kibali cha Madaktari Sio Wanasiasa
 
Umemaliza kila kitu
 
Habari yako ingekuwa haina chembechembe za lawama kwa Serikali juu ya suala la Tundu Lissu ingekuwa na ' mantiki ' na ' mashiko ' sana Kimjadala ila sasa umesababisha huu ' uzi ' wako ujadiliwe ' Kisiasa ' zaidi na kuna ' mihemko ' itajitokeza ya hapa na pale jambo ambalo naona halitakuwa na ' tija ' sana kwetu kama Great Thinkers.

Hofu yangu ni kwamba tunaweza kusema kwamba labda Serikali ndiyo imempeleka kutibiwa huko South Africa kumbe ikaja kuwa ni JWTZ lenyewe limeamua kubeba hilo jukumu la ' Kumtibia ' kutokana na ' Unyeti ' wake huyo Afande Mritaba. Kikubwa hapa ni kwamba tuwaombee wote Tundu Lissu na Mritaba wapone na warudi katika hali zao za kawaida ili michango yao iendelee kuisaidia Tanzania hasa katika nyanja mbalimbali za ' Ubobezi ' wao.

Kuna Wakubwa wengi ambao wameitumikia nchi hii sana tena katika Vipindi vigumu hadi kuhatarisha maisha yao lakini wakiugua hiyo Serikali yako haiwajali wala kuwahudumia na sijawahi kusikia hata siku moja Wanafamilia wao wakilalama kuwa Serikali imewatupa. Ni vyema sana haya mambo tukayaangalia kwa umakini mkubwa mno ili tusije tukaharibu hii ' tunu ' yetu ya amani na upendo kwasababu tu ya hizi ' Siasa ' zetu za ' majitaka ' ambazo binafsi sioni kama tukiendelea kuzikumbatia zitaweza kuitoa Tanzania Kimaendeleo hapa ilipo.

Pole sana Mbunge Tundu Lissu.
Pole sana Rtd. Major General Mritaba.
 
acheni UONGO na utoaji wa huduma za matibabu nje ya nchi/
spika Job ndugai alitoa ufafanuzi kuwa Serikali inatoa malipo kwa Hospitali ya Apollo India tu alikopelekwa yeye, Zitto z. Kabwe. Mbatia, Mrema na wengine hajaitaja afrika kusini
acheni 2standard
 
Mwanzo mlisema hakushambuliwa lilikuwa ni igizo sasa hivi mnakuja na hoja nyingine!

Utaratibu wa kugharimiwa Huduma za Matibabu nje ya Nchi na Serikal upo na lazima ufuatwe!

Kibali cha kutibiwa nje ya Nchi hutolewa na Jopo la Madaktari sio Wanasiasa Kama unataka hizo Gharama zibebwe na Serikal!
Absalom Kibanda alipojeruhiwa Rostam Azizi alimpeleka South Africa kwa Gharama zake kwa kuwa hakuwa na kibali cha Rufaa toka Kwa Madaktari

Saed kubenea alipomwagiwa Tindikal alipelekwa India kwa Kibali cha Madaktari Sio Wanasiasa
Madaktari wa kitanzania katika hospitali ya serikali huko Dodoma naweza kusema ndiyo waliookoa maisha Lissu, halafu wanatokea watu wanasiasa wanaamua kubeba gharama za matibabu yake inje ya nchi baada ya kukataa kufuata taratibu ili serikali ibebe gharama zote za matibabu kwa kuhofia usalama wa Lissu. Cha ajabu baada ya siku chache wanaanza kulalamika kila kona.

Cha ajabu zaidi wanataka vyombo vya ulinzi na usalama vilishughulikie swala la Lissu kikamilifu wakati watu mhimu wa kusaidia katika uchunguzi wanakwenda kuwaficha nje ya nchi nakubaki wanachat kwenye social media.
 
Wakati Rais wa TLS na Mbunge wa Singida Mashariki Mh. Tundu Lissu akitibiwa huko Nairobi kwa Gharama ya Chadema pamoja na Michango ya Watanzania. Serikali imeamua kumpeleka na kulipia gharama zote za Meja Vicent Mritaba.

Meja Jenerali Mstaafu wa JWTZ Amepelekwa leo asubuhi South Africa kwa Matibabu. Meja Vincent inasemekana hali yake sio nzuri tangu ajeruhiwe kwa risasi maeneo ya Ununio, Dar Es Salaam.
taratibu zilizotumika kumpeleka huyo afande unazijua?nani mlipaji?lisu kupelekwa nairobi taratibu zilifanyika kichama na kifamilia na si kitaasisi.
tueshimu jamani wastaafu ili vijana wapate hamu ya kuitumikia nchi.sasa kila msomi siasa posho na mishahara za wanasiasa ni nyingi kuliko watumishi wa kawaida,hatuombei mabaya hata la kutibiwa nalo twajenga hoja,hata kwa mtu aliefikia a two star general?
lisu kashambuliwa na kulikuwa na option zaidi ya moja kutibiwa,kwa kutumia bunge,kutumia chama cha siasa,kutumia TLs,kutumia familia na jamii kwa ujumla,au serikali.
jenerali ana option chache za kuwa na maamuzi nani abebe gharama,inawezekana jeshi kwa kuwa alilazwa hosp ya jeshi,inawezekana serikali kwa kuzingatia utu cheo na madaraka alioshika.
wote ni binadamu wanahitaji kutibiwa,lazima tufanye kazi kwa utaratibu,kupanga ni kuchagua.
 
Habari yako ingekuwa haina chembechembe za lawama kwa Serikali juu ya suala la Tundu Lissu ingekuwa na ' mantiki ' na ' mashiko ' sana Kimjadala ila sasa umesababisha huu ' uzi ' wako ujadiliwe ' Kisiasa ' zaidi na kuna ' mihemko ' itajitokeza ya hapa na pale jambo ambalo naona halitakuwa na ' tija ' sana kwetu kama Great Thinkers.

Hofu yangu ni kwamba tunaweza kusema kwamba labda Serikali ndiyo imempeleka kutibiwa huko South Africa kumbe ikaja kuwa ni JWTZ lenyewe limeamua kubeba hilo jukumu la ' Kumtibia ' kutokana na ' Unyeti ' wake huyo Afande Mritaba. Kikubwa hapa ni kwamba tuwaombee wote Tundu Lissu na Mritaba wapone na warudi katika hali zao za kawaida ili michango yao iendelee kuisaidia Tanzania hasa katika nyanja mbalimbali za ' Ubobezi ' wao.

Kuna Wakubwa wengi ambao wameitumikia nchi hii sana tena katika Vipindi vigumu hadi kuhatarisha maisha yao lakini wakiugua hiyo Serikali yako haiwajali wala kuwahudumia na sijawahi kusikia hata siku moja Wanafamilia wao wakilalama kuwa Serikali imewatupa. Ni vyema sana haya mambo tukayaangalia kwa umakini mkubwa mno ili tusije tukaharibu hii ' tunu ' yetu ya amani na upendo kwasababu tu ya hizi ' Siasa ' zetu za ' majitaka ' ambazo binafsi sioni kama tukiendelea kuzikumbatia zitaweza kuitoa Tanzania Kimaendeleo hapa ilipo.

Pole sana Mbunge Tundu Lissu.
Pole sana Rtd. Major General Mritaba.
Mkuu kumbe ukitulia unakuwa na maono ya mbali sana,hongera zako,muda mwingine cjui uwa kinakupata kitu gani!
 
Back
Top Bottom