Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,667
- 698,561
Ni mkakati unaoratibiwa kwa usiri mkubwa sana! Kwa sehemu sio vibaya kuupongeza japo kuna makosa ya kibinadamu kwa kukosea target ama kuchomekewa asiye husika!
Siku hizi ukipelekwa polisi kwa kesi ya wizi hasa huu wa kupora, kukaba watu vichochoroni, ama kuiba majumbani ukifikishwa huko salama na kufanikiwa kupandishwa kizimbani katambike kwenu kwa mizimu yote yote ya kwenu na ukoo wenu Wote.
Wenye hali mbaya zaidi ni wale ambao tayari wana faili huko police... Watalala wakipumua lakini hawata amka tena...!!! Kuna ziraili mtoa roho hupita mahabusu usiku na kuondoka na watu wake!
Fundi wangu wa ujenzi Twalika kalala mahali pema huko makaburini .. Kumbe alikuwa na kazi nyingine ya overtime kiza kkiingia na wananchi wakiwa wameshalala kabisa
Alitoka kwenye pombe mida ya saa sita usiku lakini saa tisa alfajiri akakutwa kwenye dari ya watu na zana zake za overtime.. Wakamfinya kisawasawa lakini hawakummaliza.. Kulipopambazuka akapelekwa kituo kidogo
Akapatiwa huduma ya kwanza kwenye zahanati karibu na hicho kituo akipata nafuu kidogo.. Wakati ndugu wanajipanga kwa dhamana ya mchongo wakubwa kituoni wakaona ndugu wako mwendo wa kinyonga.. Ilitakiwa 150K
Wakapiga simu kituo kikubwa likaja difenda na wale ndugu wale.. Kufika hawakutaka la mwadhini wala la mnadi swala! Wakamtupia mtuhumiwa kwenye difenda kama kiroba wakaondoka naye..
Hiyo ilikuwa asubuhi ..kabla jua halijazama tukapokea habari za huzuni kubwa! Twaliha alizidiwa kituoni wakati wakijiandaa kumpeleka hospitali kubwa!
Inasemekana pale alikuwa na faili lenye kesi mbili!
Pombe
Kipigo
Njaa.... Hakuna wa kulaumiwa...!!!!
Ikaisha kama hivyo .. Tumezika juzi..
Zaidi soma

LICENSE TO KILL: Maslahi mapana ya taifa yanapozingatiwa!
Kutoa roho ya mtu ni tofauti kabisa na kutoa roho ya mnyama ama mdudu. Kwa mnyama sana sana unaweza kulipishwa fidia hasa kama mnyama mwenyewe ni kwa ajili ya utalii. Kutoa roho ya mtu ukiachana na ule ugomvi wa papo kwa papo kunahitaji maandalizi yake! Na wengi kwenye hayo maandalizi hukosea...
www.jamiiforums.com