Panya Road, Serikali haiwatendei haki wazazi/ walezi

sheiza

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
7,570
11,492
Kinachoonekana ni serikali kuanza kushindwa na tatizo la panya road. Hili ni jeshi linalovamia kimya kimya na kufanya uhalifu mzito ndani ya muda mchache na kupotea.

Ni wazi serikali imechemsha na kuanzisha kampeni ya kuwatupia wazazi na walezi lawama. Hawa vijana inafahamika wazi wengi wao ni homeless na wengine walishaondoka nyumbani muda tu kutokana na changamoto mbalimbali za kimaisha ikiwemo hali duni za kifamilia, uyatima, manyanyaso na wengine wanajilea wenyewe.

Wengine walitoka mikoani kwa kudandia mabasi chini tena wakiwa wadogo tu na sasa ni wakubwa. Zamani kulikuwa na kituo kinaitwa dogodogo center kule posta kikikusanya watoto wasio na makazi. Wale watoto mchana walikuwa wanashinda feri jioni wanarudi kulala kituoni. Wengi wao baada ya kukua waliingia mtaani na wakawa wakabaji maeneo ya ocean road kule gymkhana.

Lakini pia mazingira huru ya kufanya biashara yalipunguza matukio mengi ya uhalifu. Badae serikali iliwaondoa bila utaratibu mzuri wakiamini wanatatua tatizo la machinga, kumbe wanatengeneza jeshi la panya road. Na wakaenda mbali wakajisifia kuwa wamefanya kazi ya kutukuka na sasa jiji lipo safi. Matokeo yake jiji limekuwa safi ila si salama tena.

Serikali isimtafute mchawi, hakuna mzazi anayemtuma mtoto kutoka mwanza au mara au kigoma aje dar kuua na kuiba. Yenyewe ishughulike na huo uhalifu kama matukio mengine. Tunachohitaji ni utulivu. Mbona enzi za kibiti, mkuranga, tanga na mwanza hatukusikia vitisho vya namna hiyo kuwa wazazi wanahusika na watoto wao kujiingiza kwenye matukio ya kuua na kuchinja watu kule.?

Kampeni ya kulaumu wazazi ni kuonyesha kushindwa kwa serikali. Maana mara ya kwanza walituaminisha wameshadhibiti hilo kundi na helicopta kutwa zilikuwa zikizunguka angani kucheki. Ila limerudi tena na bado watakuwepo sana tu kwa hali hii.
 
Back
Top Bottom