Vibaka na waharifu wengine wameachwa wakitamalaki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vibaka na waharifu wengine wameachwa wakitamalaki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntemi Kazwile, Nov 23, 2011.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Eneo la Vingunguti viwandani majira ya saa sita mchana lori lililosheheni mbolea linapakuliwa na vibaka, naambiwa hii ndiyo sababu malori ya wa wazi hulazimika kuvunja sheria za barabarani kwa kuweka walinzi kwenye mizigo yao ingawa kwa kufanya hivyo wanahatarisha maisha ya walinzi wale.Saa saba mchana mkuu wa jeshi la polisi anaamrisha vijana wake wapambane na raia wema wanaodai haki kupitia maandamano ya amani.Ni mapambano makubwa, naona magari na vifaa vingine vya jeshi letu la polisi vilivyobora na maridadi kuliko vyote nilivyowahi kuviona, hata katika sinema.Natoka hapa naelekea polisi makao makuu nakutana na kikosi kazi kinachotangaza kukamilika kwa uchunguzi uliohusu udhalilishaji aliofanyiwa mtoto wa waziri wa uswazi eti wamemsingizia anatembea na mke wa waziri wa ufukara. Wanajisifia kwa kukamilisha kazi ile ndani ya dakika 10 na mtuhumiwa yuko chini ya ulinzi.Mama watoto ananiamsha niwahi nisije nikakikosa hata hicho kidogo ninachokiita ujira, kumbe zilikuwa ni ndoto tu
   
 2. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Whaaaat???
   
Loading...