Mambo Jambo
JF-Expert Member
- Jul 11, 2008
- 1,100
- 83
Imekuwa ni jambo la kawaida katika jiji la Dar es salaam kuona wasichana wadogo(ndizi kisukari) wakiwa na wazee wakizungu, wasichana hao ambao wengi wao ni wa miaka chini ya ishirini wamekuwa wakitembea na vibabu vivyo vya kizungu huku vijana wadogo wa kizungu wakiwa wamejaa tele, chakushangaza ni kwamba vibabu vivyo vingi huwa vinafamilia zao huko vitokako na jambo jingine ni kuwa hao ndizi kisukari huwa wanakuwa na vijana wadogo wa kibongo (boy friends) ambao wengi wao huwa wanajua kuwa ma-girlfriend zao wanatembea na vibabu vya kizungu na imefikia kiasi cha hao vijana wa kiume kutambulishwa kwa hivyo vibabu vya kizungu kama ndugu i.e kaka au cousin na wakati mwingine hupewa hata ajira na hivyo vibabu roho zao haziwaumi hata kidogo, sasa nilikuwa nataka kujuzwa na wana JF ambao wako nchi nyingine za Africa, jee utaratibu huu hata huko upo?..
NDIZI KISUKARI:- Ni ndizi ambazo huwa zinakuwa zimeiva lakini umbo lake ni dogo.
MJ
NDIZI KISUKARI:- Ni ndizi ambazo huwa zinakuwa zimeiva lakini umbo lake ni dogo.
MJ