Viatu vya Nyerere na MKapa havimtoshi Rais Wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viatu vya Nyerere na MKapa havimtoshi Rais Wetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kachanchabuseta, Mar 18, 2010.

 1. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Jamani naomba michango yenu nchi inapoelekea sijui, uchumi hauna muelekeo, ,maisha magumu ....
   
 2. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Pengine sikukuelewa vizuri maana kichwa cha habari na maelezo yana imply as if kipindi cha Mwalimu na Mzee Upara kilikuwa kizuri na huyu rais wa sasa anapwaya na ndiyo maana maisha ni magumu. Hivi unakumbuka kile kipindi [wakati wa mwalimu] maisha yalikuwa magumu kiasi kuwa mtu hutoka kwenda kazini lakini hata kama ameacha pesa hana uhakika atakula nini???
  Kwa maoni yangu maisha ni mapambano na kwa bahati mbaya sisi urbanites tunalalamika lakini heinecken ndiyo bia zetu, nyama choma chips mayai ndiyo usiseme na harusi tunachangia kama hatuna akili nzuri lakini elimu kazi kulalama tu. Ukipata vihela kidogo tu basi lazima ununue gari hata kama huihitaji kiasi hicho lakini 'status muhimu'.
  Dunia hii ni kuchacharika tuache kulalamika kwa kila kitu ila tuwe na malengo n na mipango inayotekelezeka na tuwe na determination na nidhamu ya kutekeleza.
  Tuache kuilalamikia serikali kwani siamini kuwa serikali itatufanyia kila kitu. Mfano mzuri ni marekana ambayo juu ya kuendelea kwake lakini hadi leo medicare siyo universal na social services zimeelemewa na serikali yao ina deficit ya trilioni 3.
  TUPAMBANE NA MAISHA INDIVIDUALLY COLLECTIVELY TUTAFIKA TUU
   
 3. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kweli viatu ni vikubwa mno kwake amevikimbilia bila kujiandaa nafikiri saizi yake inakaribia sawa na ya Mzee ruksa lakini si za Mchonga na mzee wa Uwazi na Ukweli
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hapo nimekukubari Abunwasi, but nyenzo za kupambana peke yako ndo hakuna
   
 5. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Mkuu luteni yu mean Mzee ruksa mpaka sasa wako level moja na mheshimiwa??
   
 6. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lakini jana niliangalia luninga ya Citizen kwenye nyumba ya jirani wakikariri taarifa za IMF wakitusifu kuwa uchumi wetu unakuwa kwa 6.2% tukiwaacha nyuma majirani zetu wa afrika Mashariki!
   
 7. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mwanalugali, unaweza kupata vigezo walivyotumia mpaka wanasema umapanda 6.2%? kama taarifa za IMF zimetolewa hapahapa chini ninakuwa na wasiwasi na taarifa hizo mana zinaweza kuwa za kupikwa kuwatuliza watanzania
   
 8. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Kama ni hivyo basi tuanzie hapo. Seriously tunahitaji nini.
  Kuna jamaa yangu mmoja ambaye alikuwa wa kawaida na sasa afadhali sana aliniambia kuwa siri ya mafanikio na mtandao wa anaowafahamu hiyo ndiyo ilikuwa asset kubwa na akaoanisha alichotaka kukifanya matokeo ya msaada hasa wa mawazo wapi aende/aende vipi basi jamaa akatengeneza BP yake na akaanza kidogo kidogo, akajenga uaminifu kwa wadau na matokeo ya struggle ya miaka kama 6 hivi jamaa sasa ana establishment nzuri naye ameweza kuajiri vijana na kuwa train wengine wameiga mfano wake hivi wanajitegemea na yeye anaendelea vizuri sana .
  Nimetoa huu mfano kuashiria kuwa inawezekana kufanikiwa iwapo kunda determination na discipline
   
 9. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2010
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Kila mtu na namba yake ya mguu, nyie mlipompa kiatu hicho mlianza kupima namba ya kiatu au mguu wake, tafakari kwa makini pengine sie wananchi ndo tulokosea kupima mguu, tuliangalia uzuri wa sura tuka assume kuwa na kiatu kitamtosha, kwan hao kiliowatosha walikitumiaje? tatizo la maji,umeme,ajira, miundombinu limeanza hata mama wa mheshimiwa hajachezwa, tatizo lipo kwa wapima viatu sio wavaaji,
   
 10. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Thanks Abunwasi, i wish watanzania wote wengekuwa wanastrugle like this man uchumi ingeinuka through individuals but watu siku hizi wanataka fasta fasta
   
 11. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #11
  Mar 18, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Kikwete anafanya kazi nzuri,amefanya kazi nzuri. Viatu havikumpwaya. Lakini hakuna sababu kwa nini atawale kipindi kingine cha miaka mitano. Kumleta Bush hapa siyo sababu ya yeye kuchaguliwa tena.
  Mtu mwingine achaguliwe kuwa Rais. Tanzanians must vote for change.
  Kikwete amefanya kazi nzuri kama Waziri wa Mambo ya Nje,kwa hiyo,naturally, ikashaniwa kwamba akichaguliwa kuwa Rais,atafanya kazi nzuri sana. Lakini haikuwa hivyo. Kazi ya Foreign Minister aliifanya vyema,and there was not a murmur against him. Lakini kazi ya Urais imekuwa tofauti kabisa.
  It is always like that,people are promoted to the level of their incomptence. Wakiwa promoted too much, wakiwa promoted beyond a ceratin levetheir level of competence;wanaanza kuwa incompetent.
   
 12. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Songoro acha siasa. Dhana hizo zimepitwa na wakati kuhusu umeme hivi unafahamu ongezeko la umeme ambao limeingizwa kwenye grid katika miaka minne iliyopita [zaidi ya 400MW] Jee hizo barabara unazoziponda jee unafahamu katika kipindi cha miaka 15 zimejengwa barabara mpya za lami urefu wake haujawahi kutokea hata enzi ya mkoloni??.
  Hivi Raisi anaendesha serikali kwa utashi wake binafsi ???? Hata mzee bakhressa hafanyi hivyo itakuwa serikali????? Matatizo tunayo tena mengi tuu lakini suluhisho la matatizo hayo tunatakiwa tatue kama technocrats na siyo wanasiasa maana hali ilivyo sasa kila mtu analalamika kama mwanasiasa [hata hao technocrats]
   
 13. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Naona JK yuko karibu sawa na mzee ruksa, Mzee ruksa yeye hakuwa na jinsi kwa hali aliyoikuta akaachia uchumi holela free economy/market huyu wa sasa yeye hajui hata anatakiwa afanye nini katika uchumi Mkapa alijua akakusanya kodi JK anatumia kodi ya Mkapa, unajua viongozi wakuu karibu wote/wengi duniani hupimwa kwa mafanikio katika uchumi si bla bla za kukutana na kina Ronaldo
   
 14. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #14
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mwanalugali hizo data za IMF na WB mbona tumeshazizoea kila siku wanasema uchumi wetu unapanda huyo mwakilishi wa IMF David Robinson alipata wapi data kama si kupewa na Mkulo alikwenda vijijini hata kunywa maji ya kisima aonje ladha yake kama si kunywa ya chupa tena si ajabu alikuja nayo toka ulaya mimi huwa naziita hizo data ni za kwenye mafaili ili faili lisiwe tupu is not on ground dataz
   
 15. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu ganesh hapo umenena, ili liko wazi

  Mkuu abunwasi sijakupata vizuri hapa, u mean miaka 15 kurudi nyuma au mpaka sasa?? kwa mm ninyoona pamekuwepo kasoro katika ujenzi wa barabara kuanzia kipindi cha 2005 to date, nenda sehemu ambazo mbuge wa hiyo sehemu hana mausiano mazuri na sirikali miundo mbinu itakuwa duni saaaan

  Mmmmh Luteni hapo umesema

  Kweli luteni
   
 16. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #16
  Mar 18, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Mheshimiwa yale aliyotegemea yamekuwa sivyo ndivyo ..
   
 17. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #17
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Nimepata mjibu ya kutosha but c unajua hapa JF kuna watu wamekaa kualibiana kuaribu trend ya thread
   
 18. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,650
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Mbona hueleweki aloo?
   
 19. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #19
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kaka i think hapo alikuwa anasema mhe. kafanya kazi kweli kweli
   
 20. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #20
  Mar 18, 2010
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kikwete anaimudu kazi yake pamoja na changamoto zilizopo.Kila awamu inakutana na changamoto tofauti kulingana na hali halisi ya wakati wake.

  Nyerere aliipigisha Tanzania mark time kwa miaka takriban 25 akiiacha nchi ikiwa haina mwelekeo mzuri kiuchumi.Bwana huyu ambaye kwa jina jingine aliitwa Haambiliki alikuwa akiongoza nchi kama akili yake ilivyokuwa ikimtuma.Kam unabisha muulize Edwin Mtei kwa nini alimwaga manyanga.Uzao wa sasa hauwezi kujua adha iliyokuwepo enzi za Nyerere na kwa ufupi Mungu apishe mbali enzi hizo zisirudi tena.Waliokufa kwenye kampeni a vijiji ambao idadi yao haitambuliki Mungu awalaze mahali pema Amin.Wale walioporwa nyumba zao walizozijenga kwa jasho lao poleni.Wale waliopoteza maisha yao kwa vita kwa sababu za kimtazamo na tofauti za viongozi poleni.Wale ambao walipambana na kampeni ya kupambana na walanguzi na kutupa mali zao porini au baharini poleni maskini.Na hatimaye hata wale waliolazimika kutembea nusu uchi kwa kukosa mavazi na kuvaa makatambuga kwa sababu ya ukiritimba wa Haambiliki poleni pia.Hatimaye mambo yalipofika shingoni mwake akaleta msamiati wa kizanaki...kung'atuka.

  Mzee Ruksa alikuwa katika hali ngumu sana lakini baada ya wiki moja akatangaza kuwa hakuna tena mgao wa mafuta ya petroli na baadaye hatua kwa hatua nchi ikafunguka na kwa mara ya kwanza watu wakaanza kuangalia tv!Magazeti yakaanzishwa pamwe na vituo vya TV na maisha yakawa tofauti kabisa na yale ya enzi za Mwalimu.Watanzania wakanza kuona nguo zinapatikana madukani na wakaanza kuvaa viatu na kununua kila walichokitaka bila kuuliza mtu.Hiyo lebo ya Ruksa ndipo ilipopatikana maana huko nyuma kila kitu hat betri za tochi ilibidi zipitie kamati ya ugawaji.Mwinyi alijikuta katika kipindi kigumu baada ya aliemtangulia kuona mafanikio yake na akaanza kumchora.Pamoja na hayo Mzee huyo Mstaarabu alikuwa mtulivu hadi kipindi cha Ufisadi Mkubwa kilipoingia.

  Mkapa aliyofanya hakuna haja ya kuyadondoa kwa sababu kizazi hiki kinayatambua.Makubwa ni kujenga barabara, kuua Wapemba na kuiba mali za umma.Hatuoini Nyerere au Mwinyi Towers hapa.Sijui waliogopa au hawakupata fursa?

  Kwa Kikwete hatujaona jambo la kushtua nchi kama mauaji ya Mazegenuka,Mwembechai na Wapemba! Vitisho dhidi ya Wananchi havipo na uhuru umezagaa kila pembe.Hali ya uchumi haijawa na unafuu lakini huwezi kuilinganisha na enzi za Mwalimu,Mwinyi na za Mkapa.Kuna matumaini ya Kikwete kupata kile ambacho waliomtangulia hawakuweza kukipata.JK amefanya kazi nzuri pamoja na changamoto zilizopo na siku hizi Watanzania wanamiliki vitu ambavyo zamani ilikuwa ndoto.Tatizo letu hatuyaoni mazuri ya JK kwa sababu hatujui mabaya ya Nyerere,Mwinyi na Mkapa.

  Si Nyerere,Mwnyi au Mkapa anaweza kugusa kiatu cha Kikwete.Jama huyu ni tofauti kabisa.Ni binadamu wa kuigwa na kiongozi wa kipekee kabisa.Tumshukuru Mungu!  Mwinyi naye
   
Loading...