Viatu vya Kanye West vyauzwa kwa $1.8m

kamikaze

JF-Expert Member
Jan 25, 2011
422
610
1619515318204.png
Viatu ambavyo mtindo wake ulibuniwa na kuvaliwa na mwanamuziki Kanye West vimeuzwa kwa $1.8m (£1.3m) katika mnada ikiwa ni bei ya juu zaidi kuwahi kununuliwa .

Viatu hivyo aina ya Nike Air Yeezy 1vilivunja rekodi iliowekwa na viatu vya Nike Air Jordan 1s vilivyouzwa kwa $615,000 mwaka uliopita.

Mauzo hayo pia yanamaanisha kwamba ndio viatu vya kwanza aina ya sneakers kuuzwa kwa bei ya juu ya $1m," lilisema jumba la minada la Sotheby siku ya Jumatatu.

Kanye West kwa mara ya kwanza alivalia viatu hivyo katika tamasha la Grammy mwaka 2008 .Viatu hiyo ni saizi 12 au 11 ya Uingereza.

Vilinunuliwa na RARES, mtandao wa kuwekeza viatu visivyo vya kawaida.

Wanachama wake wanaweza kununua hisa katika viatu sawa na jinsi wawekezaji hununua hisa katika kampuni.

Viliuzwa na aliyevichukua viatu hivyo Ryam Chang katika mauzo ya faragha, ikimaanisha kwamba mnunuzi na bei yake haiwezi kuchapishwa hadi mnunuzi atakapokubali kujitokeza.

‘’Mauzo hayo yanaadhimisha bei ya juu kuwahi kuchapishwa hadharani ‘’,ulisema mnada huo katika taarifa yake. (Chanzo cha habari, BBC SWAHILI).
 
Hizo hela bora ningezichoma moto kuliko kununulia hivyo viatu.

Point ni umasikini mbaya hata iweje na uupambe vipi.


Baba, sisi sio masikini, sema tunapambana na hali zetu tu. Masikini gani analipa kodi? Sema sio haki kabisa, wao wanazo nyingi lakini hiki kidogo chetu bado wanang'ang'ania tugawane tu. Yaani we acha tu
 
Mkuu tupambane sana haya maisha hayako fair.
Wakati mm napambana kutafuta milioni 2 mtaji tu kumbe kuna kibaka kanunua pair ya viatu kwa bilioni tatu😒😒


Baba haya maisha hayako fair kabisa. Ndio maana zimejengwa jela ili tuwe na limit kwenye mawazo yetu. Unafikiri sisi ni mafala, no! Tunakubaliana na matokeo tu ili maisha yaendelee. Lakini sio haki kabisa.
 
Baba haya maisha hayako fair kabisa. Ndio maana zimejengwa jela ili tuwe na limit kwenye mawazo yetu. Unafikiri sisi ni mafala, no! Tunakubaliana na matokeo tu ili maisha yaendelee. Lakini sio haki kabisa.
Jela? Hahahahaa, umewaza mbali sana brother.
Ungepata fursa ya kuvunja na kuiba benki bila shaka ungeitumia

Jitoe kafara uishi vyema kwani vipi (kidding)
 
Jela? Hahahahaa, umewaza mbali sana brother.
Ungepata fursa ya kuvunja na kuiba benki bila shaka ungeitumia

Jitoe kafara uishi vyema kwani vipi (kidding)


Baba mimi nafahamu jela vizuri sana. We acha niwe mpole tu, haraka haraka haina baraka. Maisha yenyewe mafupi tu haya. Bora tukubali matokeo tu.
 
Back
Top Bottom