House girl alitandika kitanda cha bosi wake kama sehemu ya jukumu lake la kila siku. Alipomaliza akakitazama sana kile kitanda cha bosi wake akasema naweza kufa bure bila ya kulalia kitanda kama hiki akasema ngoja nijaribu kulala walau kidogo, akavua nguo zote akaziweka chini akabaki na gagulo tu akawasha AC akajifunika brangeti gubigubi akalala.
Kwa bahati mbaya usingizi ukampitia kweli akalala fofofo. Ghafla mume wa bosi akarudi na haikuwa kawaida yake kurudi muda huo. Alipoingia chumbani akajua hakika huyu ni mke wangu na kwakuwa jana tulikwaruzana atakuwa amekasirika tu. Akaogopa kumwamsha.
Mwanamme akasaula akabaki na msuli nae akajifunika hilohilo brangeti kwa taratibu sana kwa hofu ya kumwamsha mke wake. Kwa bahati mbaya naye usingizi ukampitia akalala fofofo.
Bosi aliporudi akaingia chumbani akakuta watu wawili wamelala fofofo akafunua brangeti kwa nguvu akawakuta wote wawili yaani yule mfanya kazi na mume wake wamelala pamoja walipoulizwa kila mtu akaeleza ukweli wake.
1. Je, Kama wewe ungekuwa ndiyo yule mke wa bosi ungewaelewa?
2. Je Kama wewe ungekuwa ndiyo yule mfanyakazi ungejitetea vipi?
3. Je, Wewe ungekuwa ndiyo yule bosi ungejitetea vipi?
4. Je, Hapo ugomvi itakuwa umesababishwa na nani? Mke,mume au mfanyakazi?