Ungekutwa na kisa hiki ungejitetea vipi?

May 22, 2017
65
298
House girl alitandika kitanda cha bosi wake Kama Sehemu ya jukumu lake la kila siku. Alipomaliza akakitazama sana kile kitanda cha bosi wake akasema naweza kufa bure bila ya kulalia kitanda kama hiki. Akasema ngoja nijaribu kulala angalau kidogo.

Akavua nguo zote akaziweka chini, akabaki na gagulo tu akawasha AC akajifunika brangeti gubigubi akalala. Kwa bahati mbaya usingizi ukampitia kweli akalala fofofo.
Ghafla Mume wa bosi akarudi na haikuwa kawaida yake kurudi Muda huo.

Alipoingia chumbani, akajua hakika huyu ni mke wangu na kwa kuwa jana tulikwaruzana atakuwa amekasirika tu. Akaogopa kumwamsha. Mwanamme akasaula, akabaki na msuli naye akajifunika hilo hilo blanketi kwa taratibu sana kwa hofu ya kumwamsha mke wake. Kwa bahati mbaya naye usingizi ukampitia, akalala fofofo .

Bosi aliporudi, akaingia chumbani, akakuta watu wawili wamelala fofofo. Akafunua blanketi kwa nguvu, akawakuta wote wawili; yaani yule mfanyakazi na mume wake wamelala pamoja. Walipoulizwa kila mtu akaeleza ukweli wake.

1. Je, kama wewe ungekuwa ndiyo yule mke wa bosi ungewaelewa?

2. Je, kama wewe ungekuwa ndiyo yule mfanyakazi ungejitetea vipi?

3. Je, Wewe ungekuwa ndiyo yule bosi ungejitetea vipi?

4. Je hapo ugomvi utakuwa umesababishwa nani? Mke, mume au mfanyakazi?

3. Story inawafunza nini mabosi, wake za mabosi na ma hausigeli?
 
Mimi ningekuwa ndio bosi, ningesema ni bahati mbaya tu kisha namfukuza dada wa kazi kwa kulala chumbani kwangu.

Na huyo mama ningemwambia, kwanini ameruhusu dada wa kazi aingie chumbani kwetu kutandika wakati hayo ni majukumu ya mke.
 
Japokuwa hakunaga usingizi wa namna hy lkn sawa nmekuelewa mtoa mada.

Mm kama mwanaume ntaeleza ukweli wote na ntahakikisha huyo binti hapati madhara yoyote kutokana na tukio hilo
 
Kwanza kabisa ningeji laumu kwanini sikujua mapema kama huyo ni beki 3 maana ningemtafuna mapema ili nipate kesi ya ukweli.
 
House girl alitandika kitanda cha bosi wake Kama Sehemu ya jukumu lake la kila siku. Alipomaliza akakitazama sana kile kitanda cha bosi wake akasema naweza kufa bure bila ya kulalia kitanda kama hiki. Akasema ngoja nijaribu kulala angalau kidogo.

Akavua nguo zote akaziweka chini, akabaki na gagulo tu akawasha AC akajifunika brangeti gubigubi akalala. Kwa bahati mbaya usingizi ukampitia kweli akalala fofofo.
Ghafla Mume wa bosi akarudi na haikuwa kawaida yake kurudi Muda huo.

Alipoingia chumbani, akajua hakika huyu ni mke wangu na kwa kuwa jana tulikwaruzana atakuwa amekasirika tu. Akaogopa kumwamsha. Mwanamme akasaula, akabaki na msuli naye akajifunika hilo hilo blanketi kwa taratibu sana kwa hofu ya kumwamsha mke wake. Kwa bahati mbaya naye usingizi ukampitia, akalala fofofo .

Bosi aliporudi, akaingia chumbani, akakuta watu wawili wamelala fofofo. Akafunua blanketi kwa nguvu, akawakuta wote wawili; yaani yule mfanyakazi na mume wake wamelala pamoja. Walipoulizwa kila mtu akaeleza ukweli wake.

1. Je, kama wewe ungekuwa ndiyo yule mke wa bosi ungewaelewa?

2. Je, kama wewe ungekuwa ndiyo yule mfanyakazi ungejitetea vipi?

3. Je, Wewe ungekuwa ndiyo yule bosi ungejitetea vipi?

4. Je hapo ugomvi utakuwa umesababishwa nani? Mke, mume au mfanyakazi?

3. Story inawafunza nini mabosi, wake za mabosi na ma hausigeli?
Haiwez kutokea scenario ya hvyo labda muv za kibongo
 
Hai make sense
Urudi nyumbani usijue housegirl yupo wapi
Uende straight kulala bila kutaka kujua?
Millango utaacha wazi?
Under assumption Tu kuwa housegirl yupo
But hujui Yuko wapi??

Na miili inafanana??
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom