Very sorry Eliza, I lied to you huu ndio ukweli

Sasa baada ya lile picha, Eliza ulizungumza kwa furaha sana, nakumbuka ulikuwa ukitabasamu sana bila kuchelewa ulisema tuende Mwenge sehemu tulivu tupige stori mbili tatu, jamaa yangu na yule dada niliyekuwa nae walikuwa wameshaanza kuusoma mchezo sasa, bahati nzuri mchizi naye alikuwa mjanja sana hakubabaika kabisa, kila ulilomuuliza alisema yah yah na hakuweka neno la ziada as alikuwa hajui kabisa ajibu nini, tukiwa ndani ya gari jamaa alikuwa akinitumia text akinisihi sana nikwambie ukweli kwani nilimweka kwenye wakati mgumu sana, nilimwambia nitakuambia tukifika Mwenge.

Duh hali ilikuwa ngumu sana kwa jamaa yangu kwa sababu uliendelea kumpigisha stori azizozijua kabisa!!
Mbaya ni pale ulipompigia mdogo wako, ambaye niliwahi kuzungumza nae ukimsimulia jinsi ulivyoniona na jinsi nilivyo, maskini ulikuwa unaongea na mdogo wako juu ya mtu asiye sahihi na yule uliyezoea kuongea nae kila siku.
Bahati nzuri mimi na rafiki yangu ni warefu tuliendana ila kidogo tu.
Tulifika Mwenge ukatupeleka sehemu na ukasema tuseme chochote...
And that time nahisi ulikuwa umeshaanza kupata mashaka kwani kuna point ulimuuliza jamaa yangu akaikosea majibu kabisa,
Ulimlalamikia kidogo ukimuuliza umesahau haraka hivyo? Ulijitahidi sana kuelezea lakini mchizi ilibidi amute tu as alikuwa haelewi kabisa hiyo habari.
Ukimya ulitawala kidogo then ukatext ukasema ''Derick ur so handsome''...
Leo nimedhibitisha nilichokuwa nakiamini.
Roho na mwili wangu vimefurahi sana kukuona. Niliisoma kijanja wala siku ijibu.
Ulinitext tena ukiniambia ningekuambia mengi but not here coz of ur friends presence sitaweza, karibu sana nyumbani kwetu.
Hapa nilijibu tu thanks!
Tuliendelea na stori nyingi nyingi as ulikuwa main speaker ulituambia sana habari zako...
Hapo sisi wengine watatu tulikuwa wasikilizaji tu, jamaa yangu alinitumia ujumbe akaniambia nikusaidie kumwambia ukweli? Nilimzuia nikamwambia nitakuambia mwenyewe.
Yule dada mwingine alishauelewa mchezo tayari na aliniandikia pia akinisisitizia nikuambie ukweli ili mshikaji wangu awe huru.

Kuna muda ulipiga simu home kwenu kwa mdogo wako, na ukataka aongee na mimi, mshikaji alipata wakati mgumu na kiukweli sauti zetu hazikuwa zinaendana.
Nilijipanga kukuambia ukweli ila nilikosa kabisa gia yakuanzia. Eliza ulikuwa mwongeaji sana, ulitusifia sana ila ndiyo hivyo nilikudanganya, wakati wakuondoka ulifika na kwa mara nyingine ulimkumbatia tena jamaa yangu kwanza then ukatuhagi na sisi at last ulihag the right person.. wewe ukaelekea Boko sisi tulielekea Mlimani ( udsm) jamaa yangu alikuwa anasoma pale.
Nakumbuka dakika kumi na tano hazikuisha uliniandikia meseji ndefu kama waraka, ukielezea tu jinsi ulivyoniona na ulivyofurahi niliwaonyesha marafiki zangu ule ujumbe, kiukweli walinilaumu sana.

Niliujibu ujumbe wako kwa kifupi tu.
Uliandika tena ukiniuliza nimekuonaje then mbona hukuwa na raha most of the time?
Nilijibu nikijaribu kukusifia na mimi ili zile sifa ulizonipa ziendane kidogo...
Tuliendelea na mawasiliano na uliniomba sana nifike kwenu kabla sijarudi Dodoma...
 
Sikuweza kuja kwenu na bado sikuweza kukuambia ukweli.
Tulipoteza mawasiliano na mpaka sasa sijui ulipo na hujui nilipo.
Bahati nzuri nilishaajiriwa sasa sifanyi tena udeiwaka na siishi Dodoma tena.

Ninaamini Eliza unaweza kuwa member wa hili jukwaa na kwa sasa bila shaka utakuwa ushaolewa labda na una watoto kabisa.
Nisamehe Nilikuelekezea kwa mtu tofauti, na kwa sababu hii elewa sasa the another person was the right one.
Barikiwa sana na Asante kwa sababu utanisamehe.
 
Duh hivi tuzo za 'fala bora wa mwaka' zinatolewa na shirika gani!??

I would nominate and vote for you over and over...
 
Mkuu ulikua na Ban ya mwaka mzima au?

Story ya 2015 unaimalizia tunakoelekea 2017?
 
Mara nyingi hii Inatokea kama demu unakua hujaridhika nae ss mtoto kawafata kwa madoido yote halafu unampasia mshkaji au ulikua unafikiria deiwaka?????
 
Inaonekana hata hapo bado unaendelea kudanganya, tena safari hii umedanganya mbele yetu.
 
Mkuu......
Hukujiamini
Mwanaume wa kweli anajiamini kokote alipo
Kokote aendako.

Ulidanganya ili iweje
Kama angekukataa au kukubali ni juu yake

Na kwa jinsi ulivyoandika hii stori ina maanisha ulimpenda sana huyu binti Eliza.
Na umeamua kuipoteza nafasi hii kwa uwoga wako.
Na kutojiamini.

Next time usifanye makosa
Kama hayo mkuu.....

Jiamini, jithamini, jielewe,
Jitambue, jiongeze, jijali mwenyewe.
Ur a man be strong!!!!


Napita tu..........
 
Back
Top Bottom